Waandishi wa habari walitishia kusimamisha kutoa habari za bunge Jumatano (tarehe 5 Juni) baada ya Ofisa wa bunge Justin Bundi kuwafukuza kwenye kituo cha habari katika bunge.
"Hatua kama hiyo haijawahi kutokea katika Kenya huru," Mwenyekiti wa
chama cha Wahariri cha Kenya Macharia Gaitho alisema kwa mujibu wa
gazeti la Daily Nation la Kenya. "Wamerudi kwenye zama za kale za
kutwezwa, udikiteta na haitegemewi kabisa katika jamii ya kisasa, yenye
maendeleo na yenye demokrasia."
Gaitho na wanachama wa chama hicho walitia saini taarifa inayosema
watavitaka vyombo vya habari kusimamisha kuchukua matukio ya habari za
bunge hadi ufikivu wa vyombo vya habari uliozuiliwa urejeshwe.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Alphonce Shiundu alisema
kuzuia vyombo vya habari kuchukua habari za matukio kutaipeleka Kenya
"kwenye zama za siku za giza", kwa mujibu wa Capital FM ya Kenya.
"Wakenya wanahitaji kuwasikiliza viongozi wao. Waandishi wa habari
wanahitaji kuwaambia Wakenya nini viongozi wao wamesema katika bunge."
No comments:
Post a Comment