Thursday, May 9, 2013

David Moyes Kocha Mpya wa Man United.

 9 Mei, 2013 - Saa 15:08 GMT

David Moyes kocha mpya wa Manchester United

Uongozi wa Old Trafford umetangaza rasmi na kuthibitisha kuwa David Moyes atakuwa meneja mpya wa timu hiyo kuchukua nafasi ya Sir Alex Ferguson atakayestaafu mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Old Trafford mchana wa leo, David Moyes amepewa mkataba wa miaka sita wa kuifundisha Manchester United kuanzia msimu ujao.
David Moyes mwenye umri wa miaka 50,ametangazwa kuwa mrithi wa Ferguson ambaye alitangaza kustaafu kuifundisha Manchester United mwishoni mwa msimu huu baada ya kuifundisha United kwa karibu miaka 27.
"Tumekubaliana kwa pamoja bila kipingamizi kupitisha jina la David Moyes" alisema Ferguson.
"David ni mtu ambaye ana uadilifu wa hali ya juu na mwenye maadili makubwa ya kazi. Nimeipenda kazi yake kwa muda mrefu tangu mwaka 1998 wakati tulipomjadili kama kocha msaidizi.
"Hakuna maswali juu yake na ana viwango ambavyo tulikuwa tunavihitaji kwa meneja wa klabu hii." aliongeza Ferguson.
Naye David Moyes amesema " Najua ni vigumu kurithi na kufikia mafanikio kama ya kocha bora zaidi duniani, lakini nafasi ya kuifundisha Manchester United sio jambo ambalo linakuja mara mbili hivyo nina matumani mazuri nikiwa kocha wa klabu hii msimu ujao."
David Moyes amekaa Goodison Park kwa miaka 11 na hajawahi kushinda taji la ligi kuu lakini ameweza kuifanya Everton kuwa miongoni mwa klabu zenye mafanikio ya wastani kwenye ligi kuu soka nchini England.
Akiwa na Everton, Moyes ameifikisha fainali ya kombe la FA mwaka 2009 katika mechi waliyofungwa na Chelsea 2-1, na pia mwaka 2005 aliweza kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya England lakini waliondolewa kwenye hatua za mwanzo za kusaka nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.
Licha ya kuwa na bajeti ndogo ya usajili, Moyes aliiwezesha Everton kuonekana miongoni mwa timu zenye kiwango bora cha soka ambapo mara kadhaa amekuwa akitoa upinzani mkubwa kwa Manchester United ambapo katika mechi ya kwanza ya ligi kuu msimu huu, Everton waliifunga United kwa bao moja kwa bila.
Kibarua kikubwa ambacho anatarajia kukikabili kama meneja mpya wa United msimu ujao itakuwa ni kuhakikisha mchezaji wake wa zamani aliyemuibua Wayne Rooney anasalia kwenye klabu hiyo baada ya kutangaza kuwa anataka kuondoka.
Meneja wa Wigan, Roberto Martinez na bosi wa Swansea, Michael Laudrup wanatajwa kama warithi wa Moyes kwenye klabu ya Everton.
Mechi ya kwanza ya David Moyes kama kocha mpya wa Manchester United inatarajia kuwa ya ngao ya jamii watakapo pambana na watani zao Manchester City ama Wigan hapo tarehe 11 mwezi wa nane kwenye uwanja wa Wembley.

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA HUKUMU YA PONDA TOKA MAHAKAMA YA KISUTU

Akitetra jambo na baadhi ya watu!
Akihojiwa na mmoja wa waandishi wa habari!
Mhadhiri Maarufu wa Kiisilamu Sheikh Habibu Mazinge (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiliwa huru.

Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
"Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhulma tunayofanyiwa waisilamu nanyie ni mashuhuda hapa leo." Alisema.

Safari ikaanza!

Akaingia kwenye gari!

Msafara ukavamiwa na wafuasi baada ya dereva wa garilake kusimamisha awasalimie wafuasi hao jambo ambalo polisi walikuwa hawalitaki na kuzua mabishano mazito lwenye mataa ya Maktaba Squire. 

Wafuasi wakajimwaga barabarani!

Wafuasi wakivamia gari kumsalimia baada ya dereva wagari hilo kulisimamisha huku polisi wakimvamia aliondoe gari hilo haraka.
Waliufukuza msafara huo hadi pale ulipotokomea!
Msafara uliendelea kukimbizwa hadi walipotokomea mbali kwa spidi ya kuwakimbia.
Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kkusikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu juu mmoja wa wafuasiwake ambao walishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili. ...

Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.
Mara baada ya kutolewa hukumu hiyo mahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.

Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.
 
1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya ardhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo la umiliki.
 
2.Upande wa Serikali haukuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.
 
3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.
 
4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.
 
5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. 

Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.

Tumewashinda!
Furaha!
Machozi yalitiririka, Jazba na ahawali zikapanda!
Safari ya kuelekea Mtambani Kinondoni Ikaanza.

Mmoja wa ndugu wa mtuhumiwa akilia baada ya kumkumbatia nduguyake kutokana na kushinda kesi hiyo.
"Pole ndio safari ya kusaka haki" Ndugu alisikika kabla ya kulia.
Waliopo kwenye majengo ya karibu wakatoka nnje kushuhudia!

Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote litakalotokea.

Waandishi nao walifanya mahojiano na baadhi ya washtakiwa na ndugu wa washtakiwa hao.
Ulinzi wa Ponda wakati wa kuondoka mahakamani hapo baada ya kuachiliwa.
Msafara wa ulinzi ukiondoka Kisutu!
Kama kawaida walikuwepo pia!

CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (SUZA) KIMEBAHATIKA KUWA MWENYEKITI MKUTANO WA OIC

CHUO Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA kinatarajiwa kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Umoja wa Nchi za Kiislamu Duniani OIC ambao utafanyika Septemba 2, mwaka huu.

Mkutano huo wa kimataifa utafanyika Zanzibar kwa mashirikiano ya Nchi ya Omani, Umoja wa OIC na Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA.
Taarifa hiyo imekuja kupitia Ziara ya siku nne ya Maafisa wa Nchi ya Omani walioambatana na Maafisa wa Jumuiya ya OIC iliyonza leo mjini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kumbumbuku na Nyaraka ya Nchi ya Oman Dkt. Hamed Mohammed Al dhawiyaniy amesema Zanzibar imepata nafasi hiyo kutokana na kuwa na Mahusiano mema na Nchi nyingi ulimwenguni na hasa katika nchi za kiarabu.

Amesema Historia na Utamaduni wa Kiislamu wa Zanzibar na namna ulivyotumika katika kusambaza Uislamu Nchi nyingine umekuwa kigezo muhimu cha Zanzibar kupata nafasi hiyo.

“Kwa vile Zanzibar ina historia nzuri katika kusambaza Uislamu nchi nyingine tunaimani kuwa hata malengo ya Mkutano wetu huo yatafikiwa kwa kiasi kikubwa ” Alisema Dkt Al dhawiyaniy ambaye pia ni Mkuu wa Msafara huo.

Kwa upende wake Mkurugenzi Mkuu wa OIC katika Kitengo cha Utafiti na Utamaduni Dkt. Halit Eren amesema Mkutano huo utakuwa fursa adhimu kwa Zanzibar kujitangaza katika mataifa mbalimbali na kuendelea kujiongezea umaarufu Kimataifa.

Amesema kwa vile Watakuja Washiriki kutoka Mataifa mbalimbali kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya OIC, Zanzibar itakuwa ni nafasi yake muhimu kufahamika kimataifa na kujipatia nafasi za masomo Duniani.

Amefahamisha kuwa Watoa Mada 164 kutoka Nchi mbalimbali tayari wameshapeleka maombi yao ili kuwasilisha katika Mkutano huo na kuwataka Wazanzibari nao kupeleka Maombi yao.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha SUZA Dkt. Haji Mwevura Haji amesema Vyuo mbalimbali kutoka nchi tofauti viliomba kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo lakini Chuo cha SUZA kimeamuliwa kuwa Mwenyeji kutokana na historia ya Zanzibar.

Amefahamisha kuwa licha ya Zanzibar kutokuwa Mwanachama wa Jumuiya ya OIC lakini kigezo hicho hakiizuii Zanzibar kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo wa Kimataifa.

Amegusia kuwa Mkutano huo unaweza kuwa fursa Adhimu kwa Zanzibar kunufaika kupitia Jumuiya hiyo kama ambavyo Nchi ya Uganda ilifaidika kwa kujengewa Chuo Kikuu cha Mbale.

“Wenzetu Uganda walifaidika na OIC kwa kujengewa Mbale University nasi pia tuna matarajio mengi ilikwemo kuitangaza SUZA na kupata Scholarships duniani” Alisema Dkt. Haji

Dkt Haji amewahakikishia Maofisa hao ushirikiano wa kutosha ili Mkutano huo uweze kutimiza malengo yaliyopangwa.

Umoja wa Nchi za Kiislam Duniani OIC unajishughulisha na mambo mbalimbali ikiwemo kusaidia Nchi wanachama wa Umoja huo katika huduma za kijamii ikiwemo ujenzi wa Taasisi za Kielimu, Afya na Miundombinu ambapo Mkutano mkuu uliopita ulifanyika Nchini Omani.
SUZA KUWA MWENYEKITI  MKUTANO WA OIC