Saturday, April 20, 2013

WANAOTUMIA ARDHI KWA SHUGHULI MBALI MBALI WANAPASWA KUZISAJILI-BALOZI SEIF

 Photo: ZANZIBAR                        20/4/2013. 

WANAOTUMIA ARDHI KWA SHUGHULI MBALI MBALI WANAPASWA KUZISAJILI-BALOZI SEIF 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewataka Wananchi wote wanaotumia ardhi popote pale walipo hapa Zanzibar kwa shughuli za ujenzi au kilimo wanapaswa  kuzisajili kupitia mrajisi wa Ardhi ili kuwepuka usumbufu mapema.

Alisema katika utaratibu maalum uliowekwa mfumo maalum umendaliwa kuwatambua watumiaji wa ardhi kama wananchi walipewa eka tatu, mashamba binafsi, mashamba ya Serikali pamoja na maeneo ya wazi.

Balozi Seif alitoa kauli hiyo wakati akiahirisha Mkutano wa kumi na moja wa Baraza la Wawakilishi uliokuwa ukiendelea kwenye ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alisema katika kulitafutia ufumbuzi wa kudumu suala la migogoro ya ardhi linaloonekana kushamiri katika maeneo mengi Nchini Serikali imeamua kusajili ardhi kwa utaratibu uliowekwa na sheria nambari 10 ya mwaka 1990 ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alieleza kwamba ipo tabia ya baadhi ya wananchi wakiwemo pia Viongozi kuuza ardhi kiholela bila ya hata kufuata sheria na taratibu zilizowekwa hali inayosababisha kujichomoza kwa migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo.

Balozi Seif alionya kwamba Mtu ye yote anayeuziwa au kununua ardhi aelewe kuwa anafanya kosa na kwa mujibu wa sheria anapaswa kuadhibiwa kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

“ Ardhi ni rasilimali  muhimu katika maendeleo ya Nchi na Wananchi wake kiuchumi na Kijamii. Kwa mujibu wa sheria, rasilimali hii bado itaendelea kuwa mali ya Serikali. Hivyo Wananchi na Taasisi zitapewa ardhi kwa matumizi yao tuu na haitoruhusiwa kuuzwa “. Alifafanua Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameiagiza Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati kusimamia vyema sheria ya ardhi bila ya kumuonea haya mtu ye yote Yule.

 Akizungumzia sheria ya mfuko wa maendeleo ya Jimbo ya mwaka 2012 iliyoanzishwa na Serikali kwa lengo la kurahisisha maendeleo ya haraka ya wananchi, Balozi Seif alisema kwamba fedha kwa ajili ya shughuli hiyo tayari zimeshakabidhiwa kwa waheshimiwa wawakilishi kwa mwaka 2012 ambazo zilikuwa shilingi Milioni 10,000,000/-.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kuwa Serikali imeamua kuongeza  kima hicho na kufikia shilingi Milioni 15,000,000/- ili kuwawezesha Wawakilishi kuwaunga mkono wananchi wao kwenye miradi yao midogo midogo walioianzisha kwa mujibu wa vipaumbele wanavyoviweka.

Hata Hivyo Balozi Seif  alikumbusha kwamba hakutakuwa na  mwakilishi atakayepatiwa fedha nyengine hadi atakapowasilisha marejesho ya fedha alizopokea kwa mwaka 2012 kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

“ Haitokuwa jambo la busara kuja kuonyeshana vidole humu ndani kwani sisi ni viongozi na tunatakiwa tuwe mfano mzuri kwa Jamii. Kwani hayo ni matakwa ya sheria ambayo tumeijadili na kuipitisha kwa pamoja ndani ya Baraza letu hili “. Alitahadharisha Balozi Seif.

Akikumbushia  suala la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la kununua Meli ya abiria Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameliarifu Baraza la Wawakilishi kwamba maandilizi yote juu ya ujenzi wa meli hiyo pamoja na michoro ya meli yenyewe yamekamilika.

Alisema Fedha zilizokusanywa na Serikali zitatumika kulipia sehemu ya gharama ya ujenzi wa meli hiyo ambapo matarajio ya utiaji saini na kampuni itakayojenga meli hiyo yatakamilika ndani ya mwezi ujao wa Mei mwaka huu wa 2013.

Balozi Seif alisisitiza kwamba ujenzi wa meli hiyo itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 pamoja na mizigo isiyopunguwa tani 200 na kuhimili pia mawimbi mazito unatazamiwa kuchukuwa miezi 18 baada ya utiaji saini.

Miswaada mitano ya sheria iliyowasilishwa  na Mawaziri mbali mbali  imejadiliwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na Maswali 82 ya msingi na 167 ya nyongeza yaliulizwa na kujibiwa katika Kikao hicho.

Miswaada hiyo ni ule wa Sheria ya kuanzisha mamlaka ya udhibiti wa huduma ya maji na nishati Zanzibar { zura }na mambo mengine yanayohusiana na hayo pamoja na  Mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya shirika la Bandari Zanzibar na mabo mengine yanayohusiana na hayo. 

Mwengine ni Mswada wa sheria ya kuanzisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na kuweka utekelezaji wa Majukumu na Uwezo na mambo mengine yanayohusiana na hayo, Mswada wa Sheria ya Mahkama ya Biashara Zanzibar na Mambo mengine yanayohusiana na hayo pamoja na Kuwasilishwa kwa Ripoti za utekelezaji wa maagizo ya Kamati za kudumu za Baraza kwa Wizara kwa mwaka 2011/2012 na zile za mwaka 2012/2013.

Baraza la Wawakilishi Zanzibar limeahirishwa hadi Jumatano ya Tarehe 12 Juni Mwaka 2013 saa Tatu za Asubuhi.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
20/4/2013.

Balozi Seif afungua rasmi Semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Z'bar kuhusu uimarishaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

20/4/2013.

 Photo: ZANZIBAR                                                     20/4/2013

 Balozi Seif  afungua rasmi Semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Z'bar kuhusu uimarishaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Watendaji wa Jeshi la Polisi Nchini wanapaswa kuendelea kutekeleza majukumu kwa nguvu zao zote ili kuwapa fursa Wananchi kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku bila ya bughdha zozote.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiifungua semina ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyoandaliwa na jeshi la Polisi Nchini Tanzania kuhusu maboresho ya jeshi hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Juu wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif alisema Jamii mara nyingi hujenga hofu wakati inapokabiliwa na matokeo tofauti yanayohatarisha maisha na mali zao na hii husababishwa  na matendo mabaya ya ujambazi wanayokuwa wakiyashuhudia katika baadhi ya maeneo yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyatolea mfano matukio ya hivi karibuni ya ujambazi yaliyotokea Zanzibar ambayo mbali ya kujenga hofu kwa raia lakini pia yameitia dosari Zanzibar katika harakati zake za kuimarisha Sekta ya Utalii.

Alifahamisha kwamba kitendo hicho kimeleta mshituko kwa wawekezaji wa sekta hiyo ya utalii jambo ambalo linaonekana kuhatarisha biashara ya utalii inayoweza kuporomosha mapato ya Taifa.

Alilikumbusha Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi kuelewa kwamba wana dhima ya kulinda maisha na mali za raia na kulitaka Jeshi hilo kujizatiti katika kutumia mbinu za Kisayansi wakati wanapokabiliana na wahalifu popote pale Nchini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa Maaskari hao kuendelea kulinda siri za raia wema wanaojilotea kutoa taarifa za watu wanaohusika na ujambazi ili wajenge imani ya kulisaidia zaidi Jeshi hilo.

Balozi Seif alisema Wananchi walio wengi hivi sasa wanashindwa kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kuhofia nusalama wao kutokana na wahalifu wanaowatolea taarifa vituoni kurejea ma majigambo mitaani huku wakitishia usalama wa maisha yao.

“  Wahalifu wanashikwa na kupelekwa vituoni kwa kutokana na msaada wa taarifa za Raia wema lakini baada ya saa chache unawakuta wahalifu hao wamerejea mitaani na majigambo kwa kuwatambia waliopeleka taarifa hizo kituoni. Sasa tujiulize usalama wa Raia hao wanaotoa taarifa hizo uko wapi “. Aliuliza Balozi Seif.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alilipongeza Jeshi la Polisi Zanzibar kwa hatua yake ya kuanzisha mpango maalum wa kushirikisha Jamii latika Ulinzi wa  pamoja { Polisi Jamii } { Ulinzi shirikishi } ambao unaonekana kuleta mafanikio kiasi.

Balozi Seif alisema mpango huo unafaa kuendelezwa zaidi kwani zipo dalili zinazoashiria kuwepo kwa hatua kubwa ya kiulinzi ambayo inaweza kupunguza au kuondosha kabisa matukio ya uhalifu katika maeneo mbali mbali hasa zile sehemu za Vitega uchumi.

“ Tumeshuhudia ndani ya maeneo yetu tunayoishi kupunguwa kwa matukio ya wizi, unyang’anyi na hata kuwepo kwa Vijana wanaojihusisha na matumizi ya  dawa za kulevya kutokana na uanzishwaji wa Vikundi hivi kwenye shehia tofauti Nchini “. Alifafanua Balozi Seif.

Naye akitoa shukrani zake kwa niaba ya Watendaji wa Jeshi la Polisi Nchini Mkuu wa Jeshi hilo Tanzania IGP Said Mwema alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya jeshi hilo baada ya kuanzishwa  mfumo mpya wa ushirikiano { Smart Partnership } ndani ya jeshi hilo.

IGP Said Mwema alisema lengo la uanzishwaji wa mfumo huo ni kuona Jeshi la Polisi Nchini linaboreka katika harakati zake za kulinda maisha na mali za wananchi hapa Nchini.