Tuesday, June 4, 2013

Wanasiasa Misri watoa vitisho kwa Ethiopia


Bwana ambalo Ethiopia inajenga kwenye mto Blue Nile hatua inayopingwa vikali na Misri
Msaidizi wa rais wa Misri ameomba radhi kwa kukosa kuonya wanasiasa kuwa mapendekezo yao kuhusu jinsi ya kuizuia Ethiopia kujenga bwawa katika mto Nile,ikiwemo kuchukua hatua za kijeshi yalikuwa, yalikuwa yakipeperushwa moja kwa moja kupitia televisheni.
Msaidizi huyo Bakinam al-Sharqawi, aliomba radhi kwa aibu yoyote waliyopata viongozi hao ambayo huenda ilitokana na kitendo hicho.
Matamshi hayo yalitolewa Jumatatu wakati wa mkutano na Rais Mohammed Morsi. Mependekezo yaliyotolewa ni pamoja na kutumia nguvu za kijeshi kuharibu bwawa hilo pamoja na hata kuunga mkono makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya serikali ya Ethiopia.
Rais Mnorsi aliitisha mkutano huo kutathmini athari za ujenzi wa bwawa la Ethiopia katika sehemu ya maji ya mto Nile yanayomilikiwa na Misri.
Washiriki wa mkutano huo hawakujua kuwa walikuwa wanatizamwa kwenye runinga wakati wakitoa matamshi yao bila ya kujali.
Mapendekezo yao yalikuwa pamoja na kuonya Ethiopia kuwa inatutumia nguvu za kijeshi dhidi yake ikiwa itaendelea na mpango wake wa ujenzi wa Bwawa kwenye mto Blue Nile.
Moja wa wanasiasa, alipendekeza kutuma kikosi maalum kuharibu bwawa hilo, mwingine akisema kuwa watatuma ndege za kivita kutisha Ethiopia wakati wa tatu akisema kuwa wangeunga mkono waasi wanaopambana na serikali ya Ethiopia.
Misri ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu Mashariki ya Kati na hutegemea sana maji ya mto Nile ambao ndio mto mrefu zaidi duniani.

Kesi dhidi ya Pistorius yaakhirishwa


Pistorius anakana kumuua mpenzi wake Reeva kwa maksudi nyumbani kwake
Kesi inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius Imeakhirishwa na mahakama hadi tarehe 19 mwezi Agosti.
Pistorius, alirejea mahakamani hii leo baada ya kupewa dhamana wakati kesi yake iliposikilizwa mara ya kwanza mapema mwaka huu.
Oscar anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi Februari.
Anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake kwa maksudi akisema alikosea kwa kudhani kuwa alikuwa jambazi kavamia nyumba yake.
Viongozi wa mashtaka wameomba muda zaidi kuweza kukusanya ushahidi dhidi ya mwanariadha huyo aliyeshiriki michezo ya Olimpiki mjini London.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa ushahidi mwingi katika kesi hiyo utatokana na uchunguzi wa kisayansi unaofanywa ndani ya bafu ambamo Reeva Steenkamp aliuawa.
Kesi hiyo kwa upana wake huenda isianze kusikilizwa hadi mwaka ujao.
Mwanariadha huiyo alichiliwa kwa dhamana na amekuwa akiishi katika nyumba ya jamaa wake mjini Pretoria

Misri yawafunga jela wafanyakazi wa kigeni


Wafanyakazi wa kigeni waliofungwa jela Misri
Mahakama mjini Cairo imewahukumu jela wafanyakazi 43 wa mashirika ya misaada kwa kufanya kazi Misri kinyume na sheria.
Wafanyakazi hao walihukumiwa hadi miaka mitano gerezani baadhi hukumu ikitolewa huku wakiwa hawako mahakamani.
Pia iliamuru kufungwa kwa ofisi zao na kupigwa tanji kwa mali ya mashirika waliyokuwa wanafanyia kazi.
Kesi hiyo iliyoanza mwaka 2012 , imetatanisha uhusiano kati ya serikali ya Misri na Marekani.
Maafisa wa Marekani, wametishia kubana msaada kwa Misri ambao unatumia dola bilioni moja nukta tano pesa za msaada ambazo hutolewa kwa Misri kila mwaka.
Jumanne mahakama ya Misri iliwahukumu washukiwa 27 miaka mitano gerezani. Wengine watano walifungwa miaka miwili na wengine 11 walifungwa mwaka mmoja kila mmoja.
Washukiwa watano pekee wakiwemo raia mmoja mmarekani walikuwepo mahakamani wakati hukumu ikitolewa.
Wanasema kuwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.
Mahakama nchini Misri pia iliamuru kufungwa kwa mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi nchini humo likiwemo shirika la Marekani la IRI
Mwaka jana wakati Misri ilipokuwa chini ya utawala wa kijeshi,kufuatia kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais Hosni Mubarak, polisi walivamia ofisi za mashirika kadhaa ya kigeni na mengine ya Misri.
Mashirika hayo yanatuhumiwa kwa kufanya kazi bila leseni na kupokea msaada kutoka kwa mashirika yasiyojulikana.

Kesi dhidi ya Ruto kusikilizwa Septemba


William Ruto ni mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya
Mahakama ya kimataifa ya ICC, imetangaza kuwa kesi zinazowakabili washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya, naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang zitasikilizwa mwezi Septemba.
Mahakama hiyo pia imependekeza baadhi ya vikao vya kesi hiyo kufanyika Tanzania au Kenya.
Ruto anakanusha kuwahi kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007 nchini Kenya, sawa na Rais Uhuru Kenyatta.
Mahakama ya ICC pia imesema kuwa ushahidi uliotolewa dhidi ya aliyekuwa rais wa Ivory Coast , Laurent Gbagbo, hautoshi kuhimili kesi dhidi ya mshukiwa.
Matangazo hayo mawili, yanakuja baada ya wiki kadhaa za shinikizo kutoka kwa nchi kadhaa za Afrika kuwa mahakama hiyo itupilie mbali kesi hizo dhidi ya Kenyatta na Naibu wake.
Mataifa ya Muungano wa Afrika yalisema kuwa mahakama ya ICC ina ubaguzi wa rangi kwa kuwa inawawajibisha viongozi wa Afrika pekee , madai ambayo yamekanushwa na kiongozi mkuu wa mashtaka Fatou Bensauda.
Daima Fatou Bensouda amekuwa akisisitiza kuwa washukiwa ghasia za Kenya lazima wawepo katika mahama hiyo wakti kesi zao zikisikilizwa.Lakini majaji wameamua kuwa haki huenda ikatendeka zaidi ikiwa wataruhusu kesi za washukiwa wawili hao kusikilizwa Kenya au Tanzania.
Upande wa utetezi pia huenda ukalazimika kutoa ombi hilo kwa niaba ya mshukiwa Uhuru Kenyatta.
Lakini pigo kubwa zaidi kwa kiongozi wa mashtaka ni ambavyo umeshughulikia ushahidi dhidi ya Laurent Gbagbo,kwani mahakama inasema hautoshi kuweza kuhimili kesi.
Mahakama inataka hilo kurekebishwa kabla ya kusikiliza tena kesi hiyo mwezi Novemba. Gbagbo amekaa ICC sasa kwa miaka miwili huku kesi yake ikiwa bado haijasikilizwa.
Moja ya sababu ya kuundwa kwa mahakama ya ICC ni kuonyesha kuwa hakuna ambaye anaweza kuhujumu sheria bila kuwajibishwa.
Kwa sasa jukumu kubwa la viongozi wa mashtaka ni kuonyesha ushahidi wa kutosha utakaoweza kuwashawishi majaji kuwa bwana Gbagbo ana kesi ya kujibu.
Kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Ujao.

Kesi dhidi ya Pistorius yaakhirishwa



Pistorius anakana kumuua mpenzi wake Reeva kwa maksudi nyumbani kwake
Kesi inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius Imeakhirishwa na mahakama hadi tarehe 19 mwezi Agosti.
Pistorius, alirejea mahakamani hii leo baada ya kupewa dhamana wakati kesi yake iliposikilizwa mara ya kwanza mapema mwaka huu.
Oscar anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi Februari.
Anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake kwa maksudi akisema alikosea kwa kudhani kuwa alikuwa jambazi kavamia nyumba yake.
Viongozi wa mashtaka wameomba muda zaidi kuweza kukusanya ushahidi dhidi ya mwanariadha huyo aliyeshiriki michezo ya Olimpiki mjini London.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa ushahidi mwingi katika kesi hiyo utatokana na uchunguzi wa kisayansi unaofanywa ndani ya bafu ambamo Reeva Steenkamp aliuawa.
Kesi hiyo kwa upana wake huenda isianze kusikilizwa hadi mwaka ujao.
Mwanariadha huiyo alichiliwa kwa dhamana na amekuwa akiishi katika nyumba ya jamaa wake mjini Pretoria

Uzinduzi Wa Rasimu Ya Katiba Mpya Ya Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionesha Rasimu ya Katiba mpya ya Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionesha Rasimu ya Katiba mpya ya Tanzania.
62.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na haki zote juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa mamlaka hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya ushirikiano na mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawa kwa ajili ya ustawi ulio bora kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akipokea nakala ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Jaji Mstaafu Joseph Warioba akishuhudia
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akipokea nakala ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Jaji Mstaafu Joseph Warioba akishuhudia.
62.-(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika wa Muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa Muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd  akipokea nakala ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda akishuhudia  akishuhudia
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd akipokea nakala ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda akishuhudia akishuhudia.
62.-(3) Mshirika wa Muungano anaweza, wa kati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Ibara ndogo ya (2), kuomba mashirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kimataifa au kikanda, na Serikali ya Jamhuri Muungano inaweza kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itakavyohitajika. - Mamlaka ya Washirika wa Muungano
Pata nakala kamili ya Rasimu ya Katiba mpya hapa: Rasimu