Monday, April 15, 2013

Mahakama yaamuru Mubarak asizuiliwe tena

15 Aprili, 2013 - Saa 12:36 GMT

Mahakama ya rufaa nchini Mirsi imeamuru rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak hapaswi kuzuiliwa tena kuhusiana na vifo vya waandamanaji waliofariki
 wakati wa mapinduzi yake.

Lakini Mubaraka atasailia kizuizini huku uchunguzi ukifanywa kuhusiana na kesi ya ulaghai dhidi yake. Hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali Misri
Mahakama ya rufaa mjini Cairo iliamuru hilo ikisema kuwa Mubaraka amezuiliwa kwa miaka miwili kipindi kinachoruhusiwa cha mshukiwa yeyote kuzuiliwa kabla ya kesi kusikilizwa na kuamuliwa.
Kesi dhidi ya Mubarak itasikilizwa tena huku akitaka uamuzi wa kufungwa maisha jela kubatilishwa.
Aidha Mubarak,aliyetawala Misri kwa miongo mitatu aling'olewa mamlakani katika mapinduzi ya kiraia mwaka 2011.
Amekuwa akizuiliwa tangu Aprili mwaka 2011 baada ya kuhusishwa na vifo vya mamia ya waandamanaji waliofanya maandamano ya amani wakimtaka aondoke mamlakani Januari kati ya tarehe 25-31.
Pia anakabiliwa na kesi ya ufisadi.
Mawakili wake walitaka mahakama kumwachilia Mubaraka kwani amezuiliwa kwa miaka miwili sasa na kulingana na sheria anapaswa kuachiliwa ikiwa kesi yake haijaamuliwa.