Kenya na Somalia zimeunda kikundi kazi cha pamoja kuanzisha njia ya
kuwarejesha nyumbani na upataji wa makaazi mapya kwa wakimbizi wa
Somalia nchini Kenya, gazeti la Daily Nation la Kenya liliripoti
Jumatano (tarehe 15 Juni).
Kikundi kazi, kilichoundwa kufuatia kikao cha Nairobi baina ya Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud,
kitatoa vigezo kwa ajili ya majadiliano kwenye mkutano huo kuhusu
wakimbizi uliopangwa kufanyika mwezi Agosti.
Kenyatta alitoa wito kwa jumuiya za kimataifa kusaidia jitihada za
upataji wa makaazi mapya kwa wakimbizi, akisema uwepo wa idadi kubwa ya
Wasomali nchini Kenya kumekuwa na athari hasi kwenye uchumi wa nchi,
usalama na mazingira.
Mohamud aliishukuru Kenya kwa mchango wake kwenye Misheni ya Umoja wa
Afrika nchini Somalia, akitoa salamu zake za rambirambi kwa vifo vya
Wakenya na askari wengine.
No comments:
Post a Comment