HABARI

 

FEZA WA TANZANIA AGONGANISHA MABWANA BAADA YA KUINGIA KUOGA NA NJEMBA IKIWA UCHI BAFUNI


Shemeji yetu Mbotswana, Oneal amechukizwa na kitendo cha Feza Kessy kwenda kuoga na mwanaume mwingine.

Jana jioni, Feza ilimlazimu amuombe msamaha mpenzi wake huyo aliyeoneshwa kuumizwa roho na kitendo hicho.

“Umefanya tena leo asubuhi. Umeniacha kitandani na kwenda kuoga na mwanaume aliye UCHI. I was so disappointed”, alisema Oneal ambaye hata hivyo hakumtaja mwanaume huyo.

“What was wrong with this particular shower”, aliuliza Feza ambaye alijibiwa na Oneal,”He was naked”.

Wasiwasi wa Oneal ni kama vyombo vya habari vya Tanzania vikipata picha hizo zinazomuonesha Feza akioga na mwanaume mwingine bafuni na kuzitumia, jambo ambalo linaweza kutia doa mapenzi yao.


Mrembo huyo wa Tanzania alimuomba msamaha mpenzi wake na kisha kumkumbatia na kumbusu huku wakijifunika shuka gubigubi, kitu kilichomaliza hasira za Mtswana huyo

Siku 100 za serikali ya Kenyatta. Nini changamoto?


Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya ICC
Mgomo wa walimu, kuzorota kwa usalama na uhasama wa kikabila, ndizo zimekuwa changamoto kubwa kwa siku miamoja za serikali ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na muungano wake wa Jubilee.
Mgomo wa walimu wa wiki nne ambao ulisitishwa Jumatano, ulikuwa umetishia kuvuruga mpango wa masomo na zaidi mitihani ambayo inaanza wiki hii.
Mitihani hiyo ilitarajiwa kuwaanda wanafunzi kwa mitihani ya kitaifa inayoanza katika muda wa miezi miwili.
Changamoto nyingine kubwa,iliyomkabili Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto, ulikuwa mgawanyiko uliosababishwa na uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Machi.
Kura ya maoni zilizochapishwa mwezi huu zilionyesha kuwa asilimia 51 ya wakenya wana imani na serikali ya Kenyatta huku asilimia 48 wakiwa na imani na Bwana Ruto.
Serikali ya Kenyatta pia imekuwa na wakati mgumu kukabiliana na utovu wa usalama unaosababishwa na magenge ya wahalifu pamoja na uhasama wa kikabila.
Ingawa mauaji yamepungua katika wiki chache zilizopita, wakati mmoja Kenyatta alionya kuwa angetuma jeshi katika maeneo yaliyokuwa yanatokota kutokana na mapigano ya kikabila.
Zaidi ya watu 100 waliuawa kwenye mapiganao hayo na kutia dosari siku 100 za kwanza za utawala wa Kenyatta.
Wadadisi wa kisiasa walisema kuwa baadhi ya vurugu zilitokana na Kenyatta kuchelewa kumteua waziri wa usalama.
Licha ya serikali hiyo kuahidi kupunguza gharama ya maisha, bado hapajakuwa na juhudi za kutosha kupunguza bei za bidhaa muhimu.
Bei za bidhaa badala yake zimepanda huku wananchi wakilalamika kuwa gharama ya maisha imepanda sana chini ya utawala wa Jubilee. Kwa upande mwingine, serikali imetimiza ahadi ya kutoa huduma za uzazi bila malipo kwa wanawake kote nchini.
Licha ya kuwepo changamoto kubwa katika mpango huo ikiwemo ukosefu wa hospitali, idadi ndogo ya wauguzi , akina mama wamefurahia huduma hizo.
Serikali ya Kenyatta pia imekuwa na kibarua kigumu kudhibiti ajali za barabarani ambazo zimesababisha vifo vingi, nyingi ya ajali hizi zimesababishwa sana na polisi wa trafiki kutokuwa wakali katika kukabiliana na madereva wanaokiuka sheria za barabarani.

"TANZANIA HAIWEZI KUIOMBA RADHI NCHI YA RWANDA"......BENARD MEMBE


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema kamwe Tanzania haitaiomba radhi Rwanda, baada ya Rais Jakaya Kikwete kuishauri nchi hiyo kufanya mazungumzo na upinzani ili kumaliza vita katika eneo hilo la Maziwa Makuu.
 
Serikali ya Rwanda iliitaka Tanzania iombe radhi kwa madai kuwa kauli ya Rais Kikwete ni kama tusi kwao na kwamba wao hawawezi kukaa na kuzungumza wapinzani ambao ni wauaji.
 
“Kama Rwanda haitaki kufuata ushauri wa Rais Kikwete inatakiwa kuuacha na siyo kumtaka aombe radhi,” alisema.
 
Membe alitoa ufafanuzi huo bungeni jana wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika mjadala wa makadirio ya matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka 2013/2014.
 
Tamko hilo la Serikali limekuja ikiwa zimepita takriban siku sita tangu Serikali ya Rwanda kutoa tamko la kupinga ushauri huo uliotolewa na Rais Kikwete wakati akiwa katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika (AU), uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
 
Akijibu pendekezo hilo la Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo alisema kuwa Rwanda haiko tayari kufanya mazungumzo na watu ambao walishiriki kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, dhidi ya Watutsi na kwamba kufanya hivyo ni sawa na kuhalalisha mauaji kwa wananchi wake.
“ Wale wote wanaodhani kuwa Rwanda itaanzisha majadiliano na waasi wa FDLR nadhani kwa ukweli hawajui kile wanachozungumza. Rwanda haiwezi kujadiliana na wauaji,” alisema waziri huyo wakati akizungumza na Idhaa ya Kimataifa ya Radio Ufaransa.
 
Alisema kuwa wakati serikali ya Rwanda imefaulu kuzika mienendo inayopalilia mauaji ya halaiki, lakini bahati mbaya kumesalia makundi ya watu ambayo bado yanahubiri itikadi zinazokumbusha uchungu na kutonesha kidonda kilicholeta maafa makubwa kwa wananchi.
 
“ Kumbe kuna wasemaji wengi wa kundi la FDLR. Wengine wao wanaendelea kufungamana na itikadi za kundi hili. Rwanda ilifaulu kutokomeza mauaji ya halaiki lakini hatukutokomeza itikadi za kundi hili,” alisema waziri huyo.
Kauli ya waziri huyo imeungwa mkono na baadhi ya wasomi pamoja na wanaharakati waliosema kuwa kuiomba Rwanda ianzishe majadiliano na kundi hilo, wanapaswa kufikiri mara mbili.
 
Katika ufafanuzi wake Membe alimnukuu Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Isaack Rabin kwamba mwaka 1995 aliwahi kutoa tamko lililosema, ‘Tunajenga amani na tunajadiliana na maadui zetu na si marafiki’.
 
Alisema kama Serikali ya Rwanda itakuwa imesikia kauli hiyo inatakiwa kufanya mazungumzo ya amani na maadui, na wasingoje kufanya mazungumzo ya amani na Tanzania, ambayo wana uhusiano mzuri na ni nchi rafiki kwa muda mrefu.
“Sijui kwa nini wanaliepuka suala hili. Israel na Palestina wanazungumza, sasa wao ni nani mpaka wakatae kufanya mazungumzo? Sasa watapigana mpaka lini wakati wameshindwa kutatua tatizo hilo kwa miaka 16?” alihoji Membe na kuongeza;
 
“Sijui kwa nini wanaona aibu kufanya mazungumzo na upinzani. Ningependa serikali ya Rwanda ijue kuwa kwa tabia yetu tangu uhuru tunatoa kipaumbele kwa mazungumzo ya amani. 

 Tumekwenda katika kikundi cha M23 na tumemhimiza Rais Yoweri Museveni wa Uganda afanye mazungumzo.

HUDDAH TOKA KENYA AYAAGA MASHINDANO YA BIG BROTHER..... MWAKILISHI WA TANZANIA ALIA NA WAVUTA BANGI

Maneno  huumba....!!!  Huddah  ameliaga  shindano hilo...------------------------  
Huddah ambaye ni mshiriki kutoka Kenya   alijikuta akibubujikwa na machozi  jana wakati akimuelezea Angelo (SA) kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi ambao ni wa ku-beep yani vuta nikuvute ambao amekuwa nao nchini kwao.

Mrembo huyo hakutaja jina la mpenzi wake lakini inahisiwa alimaanisha kuwa katika mahusiano na Rapper Prezzo wa Kenya. Kwa muda sasa kumekuwa na umbea mtaani kuhusiana na uhusiano wa kimapenzi kati ya wawili hao lakini haijafahamika kinaga ubaga kama Huddah alimaanisha kum-miss Mr. President. ..

Mrembo huyo akizidi kufunguka, alielezea jinsia anavyo-miss mabusu motomoto, anavyo-miss kung'atwa shingoni n.k. “I miss the way that he kisses me. I miss him biting my neck”.. 
LEO  MACHOZI  YAKE  YAMELIPWA  BAADA  YA  MREMBO HUYO  KUONDOLEWA  NDANI YA  JUMBA  HILO....Mashabiki  wamepiga  kura  ya  kumwondoa  ili  asiendelee  kumlilia  mpenzi wake.....
Mshiriki mwingine  aliyeaga  mashindano  hayo  ni  Denzel wa Uganda....

KWA UPANDE MWINGINE, mrembo wa Tanzania ,Feza anayeiwakilisha Tanzania alijikuta katika simanzi kali wakati alipoelezea kuhusu jinsi ambavyo kaka yake aliteseka kutokana na kujihusisha na madawa ya  kulevya .. 'drugs'.
Feza alitumia fursa hiyo kuwasihi watu hasa vijana kujiepusha kabisa na madawa ya kulevya kwani ni hatari sana katika jamii inayotuzunguka..

 

LEO MAHAKAMANI" HUKU LADY JD NA RUGE" KULE "LWAKATARE NA KESI YA UTEKAJI"

WAKATI kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare ikitarajiwa kusikilizwa leo Mei 27 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Kesi ya msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judith Wambura (Lady JayDee) pia inatarajia kusikilizwa tarehemu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  
Kesi hizo zinatarajia kuvuta hisia za watanzania kutokana na mvuto na aina ya kesi hizo,Lwakatale atapanda kizimbani kwa mara nyingine huku akitarajia kupata dhamana ya kesi yake baada ya Mahakama Kuu kumfutia mashtaka ya Ugaidi yaliyokuwa yakimkabili awali na kubaki na shitaka la kula njama ya kumdhuru Denis Msacky ambayo inadhaminika. 
 Kwa upande wa Lady JayDee anatarajia kupanda kizimbani kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa hati ya mashtaka na kutakiwa kurudi mahakamani hapo kesho mei 27 .
Waandishi wa habari walishuhudia barua kutoka mahakamani hapo pamoja na nyakara zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwamo blogu zilizoelezea ugomvi wake kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba.
“Hili ndilo shtaka lenyewe kwa hivyo sisi hatuwezi kusema chochote kwa sasa tunaelekea kwa mwanasheria wetu ili kuanza kuishughulikia kesi hii,” alisema Gadna Habash mume wa mwanamuziki huyo. 
Kabla ya kufika mahakamani hapo mchana, mwanamuziki huyo alitoa mada katika jukwaa la sanaa Basata ambako alizungumzia changamoto nyingi zilizopo katika kufikia mafanikio kwenye sekta ya muziki.
 
Wakati kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Mei 27, siku nne baadaye Jaydee anasherehekea miaka yake 13 tangu aingie rasmi katika sekta ya muziki.

"BABY NIMEKWAMBIA NIPELEKE CHOONI"....ILIKUWA NI KAULI YA MPENZI WANGU KABLA HAJAVAA NGUO NA KUONDOKA


Nimekuwa    katika  mahusiano  kwa  muda  mrefu na binti  mmoja ambaye siku  zote  huwa  tunafurahia  mahusiano  kama  kawaida  na  hajawahi  niambia  mambo  ya   chooni...

Kilichonichanganya  ni  hili  tukio la  jana  ambalo  limenifanya  nivunje  ukimya...

Wakati  tunavunja amri ya sita baada tu ya kumaliza first round tulipumzika  kama  kawaida  ili kujiandaana second round....
Wakati   niko tayari kwa second round, mrembo wangu  aliomba  nimpeleke  chooni..."BABY NIPELEKE CHOONI"...
Nikamwambia "afadhali umesema mapema kabla sijaanza second round maana ungenikata stimu, haya baby twende..."
Nilivyo  mwambia  hivyo huku nikiwa nimesimama , mwenzangu aligoma, akarudia tena, "BABY NIMEKWAMBIA NIPELEKE CHOONI"....!!
Nikamwambia :"sasa si uamke twende? ..Nilivyosema  hivyo, binti alianza kuniangalia kwa jicho la hasira  na baadae akavaa nguo zake akatoka kwa jazba...
Kusema  kweli  nilipigwa na butwaa huku  nikiwa  sielewi  kinachoendelea.Baada ya muda kidogo alinitumia  text  inayosema hivi:

    "Mwanaume gani wewe  huelewi...!!!  siamini kama ni mshamba kiasi hicho. Next time nikikwambia NIPELEKE CHOONI maana yake ubadilishe mlango"

 Kumbe  maana  yake  ilikuwa kumpeleka chooni ni kumuingilia kinyume na maumbile,kitu  ambacho  niliapa  kutotenda  maishani  mwangu....

Naombeni  ushauri  au mtazamo  wenu.Binti  bado  nampenda  na  tuna share  vitu  vingi  sana...Najaribu  kuachana  naye  lakini  nashindwa  na  Kumpeleka  chooni  siwezi  hata  kwa  dawa..!!


Upinzani walaani uvamizi Uganda


Ofisi za Gaeti la Daily Monitor zilizovamiwa na polisi wa Uganda
Mkuu wa majeshi wa zamani nchini Uganda ambaye sasa ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for democratic Change FDC Meja Generali Mustaafu Mugisha Muntu amelaani hatua ya sasa ya serikali ya amiri jeshi mkuu wake wa zamani ya kuandama na kuzingira ofisi za magazeti ya The Daily Monitor pamoja na Redpepper.
Akiongea na waandishi wa habari nchini Uganda, Bwana Muntu alisema kuwa Rais Museveni anahofia kuwa udhibiti aliokuwa nao kwa vyombo vya usalama na ulinzi umeanza kusambaratika na hivyo kumtia hofu zaidi Museveni.
Polisi nchini Ugandan waJumatatu walivamia ofisi za magazeti kufuatia taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais.
Vituo viwili vya Redio pia vilivamiwa na kuzimwa , hii ni kwa mujibu wa gazeti la serikali la New Vision.
Wiki iliyopita magazeti ya Uganda yalidai kuwa kuna njama za kuwaua wale watakao pinga mpango wa Rais Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda.
Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji yalitolewa na Mkuu fulani wa jeshi la Uganda.
Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung'atuka uongozini mwaka 2016.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni anamuandaa mwanawe Muhoozi Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini kushikilia uongozi wa Uganda.
Lakini serikali ya Museveni imekanusha kwamba kuna mipango kama hiyo.

Mwanawe Museveni Brig. Kainerugaba.

Wiki iliyopita gazeti la, the Daily Monitor,na jengine la , Red Pepper, lilichapisha barua ya siri ikidai ilikuwa imeandikwa na Jeneral David Sejusa, ikitaka uchunguzi ufanywe kuthibitisha madai kwamba kuna mipango ya kuwauwa wote watakao piga mipango ya Rais Museveni kumpachika mwanawe uongozini.
Uvamizi huo wa polisi umeidhinishwa na mahakama ya Uganda na ulikuwa unalengo la kutafuta barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na mkuu huyo wa Jeshi akifichua njama za mauaji.
Vituo viwili vya Redio vinavyohusiana na Daily Monitor, Dembe FM na KFM, pia vilivamiwa na kuzimwa.

Rais Yoweri Museveni
Mkurugenzi Mkuu wa Daily Monitor Bwana Alex Assimwe aliambia BBC kwamba Chumba chao cha Habari kilivamiwa na polisi wapatao 50 waliojihami kwa silaha.
Lakini wachanganuzi wa maswala ya kisiasa wanadai kuwa ikiwa barua ya Jenerali Sejusa ni ya kweli basi ni dalili kuwa kuna hali mvutano ndani ya jeshi huku ikidhaniwa kuwa wanajeshi wakongwe huenda wanapoteza uwezo kwa wanajeshi chipukizi wanaoongozwa na mwanawe Museveni Brigadia Kainerugaba.
Jenerali Sejusa ni mwanajeshi mkongwe aliyekuwa katika vita vya ukombozi uliyomuweka Rais Museveni madarakani mwaka1986.
Kwa muujibu wa taarifa za AP kamanda mmoja wa jeshi Jenerali Aronda Nyakairima amenukiliwa akisema kuwa Jenerali Sejusa kwa wakati huu anachunguzwa kutokana na barua anayodaiwa kuiandika.


 Uvamizi kwa "kumfichua" Museveni


Ofisi za Gaeti la Daily Monitor zilizovamiwa na polisi wa Uganda
Polisi nchini Ugandan wamevamia ofisi za magazeti kufuatia taarifa kwamba Rais Yeweri Museveni anamuandaa mwanawe wa kiume kumrithi urais.
Vituo viwili vya Redio pia vamiwa na kuzimwa , hii ni kwa muujibu wa gazeti la serikali la New Vision.
Wiki iliyopita magazeti ya Uganda yalidai kuwa kuna njama za kuwaua wale watakao pinga mpango wa Rais Museveni kumuandaa mwanawe kuchukua madaraka ya Uganda.
Magazeti hayo yalidai kuwa mipango hiyo ya mauaji yalitolewa na Mkuu fulani wa jeshi la Uganda.
Bwana Museveni, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986, anatarajiwa kung'atuka uongozini mwaka 2016.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kwamba Museveni anamuandaa mwanawe Muhoozi Kainerugaba,ambaye ni brigadier jeshini kushikilia uongozi wa Uganda.
Lakini serikali ya Museveni imekanusha kwamba kuna mipango kama hiyo.

Mwanawe Museveni Brig. Kainerugaba.

Wiki iliyopita gazeti la, the Daily Monitor,na jengine la , Red Pepper, lilichapisha barua ya siri ikidai ilikuwa imeandikwa na Jeneral David Sejusa, ikitaka uchunguzi ufanywe kuthibitisha madai kwamba kuna mipango ya kuwauwa wote watakao piga mipango ya Rais Museveni kumpachika mwanawe uongozini.
Uvamizi huo wa polisi umeidhinishwa na mahakama ya Uganda na ulikuwa unalengo la kutafuta barua hiyo inayodaiwa kuandikwa na mkuu huyo wa Jeshi akifichua njama za mauaji.
Vituo viwili vya Redio vinavyohusiana na Daily Monitor, Dembe FM na KFM, pia vilivamiwa na kuzimwa.

Rais Yoweri Museveni
Mkurugenzi Mkuu wa Daily Monitor Bwana Alex Assimwe aliambia BBC kwamba Chumba chao cha Habari kilivamiwa na polisi wapatao 50 waliojihami kwa silaha.
Lakini wachanganuzi wa maswala ya kisiasa wanadai kuwa ikiwa barua ya Jenerali Sejusa ni ya kweli basi ni dalili kuwa kuna hali mvutano ndani ya jeshi huku ikidhaniwa kuwa wanajeshi wakongwe huenda wanapoteza uwezo kwa wanajeshi chipukizi wanaoongozwa na mwanawe Museveni Brigadia Kainerugaba.
Jenerali Sejusa ni mwanajeshi mkongwe aliyekuwa katika vita vya ukombozi uliyomuweka Rais Museveni madarakani mwaka1986.
Kwa muujibu wa taarifa za AP kamanda mmoja wa jeshi Jenerali Aronda Nyakairima amenukiliwa akisema kuwa Jenerali Sejusa kwa wakati huu anachunguzwa kutokana na barua anayodaiwa kuiandika.

TAHARUKI YAJITOKEZA IBADANI KKKT KIJITONYAMA  BAADA YA MSHARIKA MMOJA KUDONDOKA GHAFRA MEI 19/05/2013
 





Taharuki waumini wakati wa ibada

Watu wa maombi wakitoa msaada



Tukio hilo lilitoka wakati ibada ya mahubili ikiendele katika kanisa hilo ambapo mtu ambaye hatukufanikiwa kupata jina lake alidondoka ghafra.Kutokana na kutokuwa na mtu wa karibu ambaye alikuwa  naye mwandishi wtu hakufanikiwa kujua ni nini kilichomtokea
  

Sheria ya wanawake Afghanistan yapingwa
Wabunge wa Kiislamu wenye msimamo mkali nchini Afghanistan wamezuia mjadala wa bunge kuhusu sheria ya kuwalinda wanawake na dhulma.
Wanawake wa Afghanistan

Mjadala huo ulikwama baada ya dakika 15 katika mabishano makali, pale wanasiasa wasiotaka mabadiliko walipotaka sheria hiyo ifutwe - sheria iliyoanzishwa na Rais Hamid Karzai miaka mine iliyopita bila ya idhini ya bunge.
Walimshutumu Bw. Karzai kwamba amekiuka sharia za Kiislamu.
Mamia ya watu, hasa wanaume, wamefungwa kufuatana na sheria hiyo ambayo inapiga marufuku utumiaji nguvu dhidi ya wanawake, ndoa za watoto na ndoa za lazima.

Mapigano kati ya wapiganaji wa Mali

Mapigano yamezuka kaskazini mwa Mali baina ya kundi kuu la wapiganaji wa kabila la Tuareg, MNLA, na wapiganaji Waarabu wa kanda hiyo.
Wapiganaji wa MNLA walipokuwa mjini Kidal awali mwaka huu
Msemaji wa MNLA, Moussa Ag Assarid, alieleza kuwa wapiganaji wao walishambuliwa katika mji wa Anefis na wapiganaji wa Kiislamu hapo jana na kwamba mapambano yanaendelea.
Waandishi wa habari wanasema ghasia hizo zinaonesha vipi wapiganaji waliokimbia mashambulio yaliyoongozwa na kikosi cha Ufaransa dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu na Watuareg, bado wanachafua juhudi za kurejesha amani nchini Mali kabla ya uchaguzi wa mwezi July.

HUYU NDO MBUGE ALIYEDONDOKA JANA BUNGENI

MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Mwanamrisho Taratibu Abama  jana asubuhi aliugua  na  kuanguka ghafla katika viwanja vya Bunge na kukimbizwa hospitali....
 
Tukio hilo lilitokea wakati akienda  kuhudhuria semina ya wabunge kuhusu  Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa nguvu   na  kudondoka  na  kisha kusaidiwa na wenzake  kumkimbiza kwenye zahanati ya Bunge. 
 
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza bungeni, gari la wagonjwa lilimkimbiza Hospitali  ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako amelazwa. 
 
Kwa mujibu wa waliomshuhudia, mbunge  huyo  alianza kwa kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa karibu  walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa dripu  kabla ya kupelekwa  hospitalini.
Kaimu Mganga Mkuu wa  Hospitali ya Dodoma,  Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo.

MFANYABIASHARA ALIYEFUMANIWA NA MWANAFUNZI GESTI APIGWA FAINI YA 640,000

   
Mfanyabiashara akiwa ndani baada ya kushtukiziwa
YULE mfanyabiashara  wa jijini Dar ambaye hivi karibuni alifumaniwa gesti akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili, huenda akapandishwa kizimbani siku yoyote.....

Kwa mujibu wa dada wa mwanafunzi huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe , baada ya mfanyabiashara huyo kufumaniwa na binti huyo mwenye umri wa miaka 16, aliahidi kutoa fedha za Kimarekani dola 400 (zaidi ya Sh. 640,000) kama faini kwa kitendo hicho.


Hata hivyo, pamoja na kukubali kutoa kiasi hicho, mfanyabishara huyo hakutimiza ahadi yake na kuamua kuingia mitini.
 

Dada wa mwanafunzi huyo amedai  kuwa   mfanyabiashara huyo anasakwa ili wamburuze mahakamani kutokana na mwisho wa mwezi uliopita kushindwa kutimiza ahadi yake.
 

“Aliandika kwa mkono wake kwamba atamlipa huyu mwanafunzi fedha hizo kama fidia ili akalipie ada ya kuendelea na masomo, lakini mpaka leo hii hajaonekana na wala simu yake ya mkononi haipatikani, tukimkamata tutamburuza mahakamani kwa sababu sheria hapa Bongo hazifuatwi kabisa kwani tulitarajia vyombo husika vingeingilia kati lakini hakuna lolote,” alisema dada huyo.

Aidha, dada huyo alisema kuwa wanatarajia kwenda kuchukua hati ya kumkamata mfanyabiashara huyo ‘RB’ katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ili waweze kumsaka.

“Ushahidi tunao tena wa uhakika kabisa, kaandika kwenye karatasi na katia saini yake, tena mwandishi naomba na zile picha alizopigwa akiwa chumbani na mdogo wangu ili zinisaidie katika ushahidi wa mahakamani,” alisema dada huyo huku akionesha karatasi ambayo waliingia makubaliano ya kulipwa dola hizo 400 na mfanyabiashara huyo.

Jumatano ya Aprili 24, mwaka huu mfanyabiashara huyo alifumaniwa na denti huyo katika chumba namba 107 ndani ya gesti moja iliyopo Kinondoni, Dar BAADA YA KUWEPO HOFU YA MAANDAMANO, MJI WA MTWARA WATAWALIWA NA UKIMYAA, SHUGHULI ZA SIMAMA, ULINZI KILA KONA
Hakukuwa na hali yeyote ya uvunjifu wa amani
Ulinzi umeimarishwa kila kona

Hali ya usalama ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ni tete. Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi. 
 
Usafiri wa Pikipiki unapatikana katika baadhi ya maeneo machache ya mji, huku maneo makuu ya biashara yakiwa wazi bila ya pilikapilika za watu kama ilivyo kawaida.
 
Polisi wakiwa kwenye magari wameonekana katika maeneo mbalimbali ya mji, na wengine kuweka makambi madogo katika maeneo yanayoaminika kuwa na msongamano wa watu katika siku za kawaida. 
Soko Kuu, kituo kuu cha mabasi na maduka yamefungwa tangu asubuhi.

Mwandishi  wetu ameshuhudia magari ya polisi yakiwa na askari katika maeneo ya Bima, Soko kuu ambako pia kulikuwa na gari la kumwaga maji ya kuwasha, Magomeni, Skoya na Majengo.
MADUKA YA BIMA YOTE CLOSED:
JUCTION YA BIMA HAINA WATU KABISA, HATA NMB IMEFUNGWA:
KWA MBALI UTALIONA GARI YA ASKARI IKIRANDARANDA...KOKOBICHI, KIMYA KABISA 
 
Hata hivyo hadi kufikia saa 7 mchana hakukuwa na hali yeyote ya uvunjifu wa amani, makundi ya vijana walionekana wakijadiliana mambo katika maeneo mengi ya mji.

 Hali hiyo imejitokeza kufuatia kusambazwa kwa vipeperushi na ujumbe wa simu za mkononi na watu wasiojulikana ukiwataka wafanyabishara kusimamisha shughuli za biashara kwa siku ya leo ili kutoa fursa kwa wananchi hao kusikiliza bajeti ya Nishati na Madini iliyotarajiwa kuwasilishwa leo Bungeni mjini Dodoma. 
 
Hata hivyo bajeti hiyo itawasilishwa Bungeni Mei, 22, mwaka huu.Sehemu ya kipeperushi hicho kilichopambwa na picha ya mtoto aliyeshikia kombora kinasomeka
 
 “Wote kwa pamoja siku ya tarehe17.05.2013 (Ijumaa saa 3 asubuhi) tusikilize bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini (Bungeni) ili kujua mustakabali mzima wa gesi yetu na ili kuonyesha kilio, msimamo wetu kwa serikali wa kutaka maendeleo kwa mikoa ya kusini, siku hiyo huduma zote za jamii zisimamishwe”
 
Licha ya polisi mkoani hapa kuwasihi wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa jeshi hilo litaimarisha ulinzi bado wananchi wameonesha kutokubaliana na wito huo.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Linus Sinzumwa ameliambia amesema kuwa hali ni shwari na kwamba jeshi lake limeimarisha ulinzi.
“Hali ni shwari, wapo madereva Bodaboda wanaendelea na kazi zao, wananchi wanatembea kama kawaida, ispokuwa baada ya maduka yamefungwa” alisema Sinzumwa

Cyclone Mahasen threatens Bangladesh


A cyclone shelter in Cox's Bazar  
Scores of people have taken refuge at a cyclone shelter in Cox's Bazar

Related Stories

Hundreds of thousands of people are being evacuated from coastal areas of Bangladesh threatened by Cyclone Mahasen.
The Bangladeshi authorities have raised the danger level to seven out of 10 for low-lying areas around Chittagong and the coastal district of Cox's Bazar.
It is estimated that the cyclone, heading north-east through the Bay of Bengal, will reach land on Thursday.
Burma is also threatened and evacuation efforts are under way there.
Tens of thousands of Rohingya Muslims living in camps in low-lying areas of Burma's Rakhine state are feared to be at risk.
They were displaced by ethnic violence last year and many are reluctant to move from the camps.

 

HEMED PHD ANUSURIKA KUTANDIKWA MAKOFI JUKWAANI NA MREMBO ALIYEMTOMASA NA KUMPULIZIA PERFUME KINYEMELA


Ni usiku wa jana wakati PHD akizindua wimbo wake wa Rest of my life ambapo hit maker huyo wa Mama kimbo aliingia kwa stayle ya kuspray perfume kwa fans wake na kwa bahati isiyo nzuri kwa PHD alispray perfume kwa mwanadada wa kitasha aliyekuwa akishout kwa kumwita hemed on stage.....

Hemed alikosea  kwa kudhani kuwa mwanadada naye anataka apigwe unyunyu...Alimfuata  na  "tomasa toma style"  alafu  akamtandika  unyunyu  na hiyo ikawa ndiyo mistake kwa mkali huyo wa music na bongo movie... kumbe bi dada alimaindi...!!!

Alisubiri mpaka hemed alipomaliza kufanya yake on stage , then akamfuata backstage na   kutaka  kumnasa  makofi  huku  akitema  cheche.

Tazama video hapo chini  jinsi mwanadada alivyokuwa akimkoromea PHD

FLORA BAHATI LYMO NI MWANAMKE ANAYEDAI KUBAKWA NA MBUNGE WA TANZANIA


BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda kuwa amembaka...
 
Katika uchunguzi wake, hivi karibuni ,Uwazi lilielezwa kuwa kuna habari ya kashfa nzito inayomtafuna mbunge huyo anayetokea Kanda ya Kaskazini lakini haikufafanua kwamba inahusu nini.
Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa mahakamani huko London nchini Uingereza.


Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu’ hivyo uwazi likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London kikazi.
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
 
“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).


Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: “Nikiwa kwenye mkutano….(jina la mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi waliohudhuria mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo ili ionekane mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza) wengi.
 
“Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka kunipa kadi ya chama chake  nikakataa, ndipo akadai kwamba mimi nilitumwa kwenye mkutano huo na balozi na rais kwa ajili ya ushushushu.


“Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa naondoka kurudi nyumbani kwangu, mbunge huyo na wenzake nao walitoka. 
Tukiwa njiani wenzake walikwenda kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba akajisaide nyumbani kwangu, nilimkubalia. 
Alipofika ndani, bila kujua kila kitu kinaonekana kwenye kamera alinibadilikia kama vile adui vitani, ona sasa wema wangu ukawa umeniponza.


Alinirukia, akaniburuza hadi kitandani kwangu. Nilipokuwa mkali na kwa namna nilivyokuwa nimechanganyikiwa sishikiki ndipo akanivamia maungoni, akanichania nguo zangu akitaka nimwachie atimize lengo lake la kuniingilia kimwili kwa nguvu.
 
“Nilijitahidi ili asifanikiwe, nikamwambia amekwisha kwani lazima nimwanike ndipo akanipiga nusu aniue akisisitiza kuwa kama nitauanika uovu wake huo au kuchukua hatua zozote ataniua.
 
“Inaniuma sana, kunibaka anibake halafu atishie kuniua, unyama gani huu?”
Flora anaendelea kusema:
“Katika purukushani hiyo, nilipopata mwanya kidogo tu, nikapiga namba ya polisi 999 kuomba msaada. Alipoona hivyo alitoka na kutokomea kusikojulikana. Polisi walipofika hawakufanikiwa kumkamata.”

Flora alisema polisi walimchukua na kila kitu cha ushahidi zikiwemo nguo zake hadi kituoni, wakamhoji kwa kumrekodi sauti, wakampa namba ya jalada la kesi inayosomeka; 4621279/2012-UBAKAJI/KUTISHIA KUUA ambapo hadi leo mbunge huyo anasakwa na Polisi wa London, akikanyaga tu Uingereza lazima akamatwe akajibu tuhuma za ubakaji na kutishia kuua.
 
Flora akaongeza: “Ukweli ni kwamba hakufanikiwa kukamatwa kwa sababu alikuwa na passport za kidiplomasia ambazo nyingine hakutumia jina lake halisi.
“Kesho yake nilisikia alikimbilia Ujerumani, nikawaambia polisi lakini walikumbana na tatizo lile kwani majina niliyowapa siyo aliyotumia kuingia Ulaya.
 
“Januari mwaka huu nilipotaka kurudi nyumbani Kilimanjaro, mahakama ya hapa (Uingereza) ilinipa barua ambayo nilipofika niliipeleka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi nikafunguliwa faili Namba Mos/RB/17127/12 kwa ajili ya ulinzi chini ya R.C.O Ramadhan Ng’anza.

“Niliwaeleza kuwa mtu anayetaka kuniua ni mbunge huyo. Kweli waliahidi kunisaidia, nilipoondoka kurudi London niliwasiliana na polisi Kilimanjaro lakini niliona kama kuna kitu au mbunge huyo yupo juu ya sheria kwani walikana kunifahamu.
“Sitachoka kutafuta haki na kutetea wanawake wanaobakwa kila siku wanaona aibu kusema, naamini aibu haipo kwa mbakwaji bali kwa mbakaji, yule …. (anataka jina) ni mbakaji.
 

“Nimesharipoti mashirika mengi ya haki za binadamu ya Uingereza. Kuna siku nilishinda mahakamani, kule ni yeye tu anasubiriwa atiwe mbaroni akasimame kizimbani ndipo dunia itajua ninachokisema.”


Flora allisema kama kweli mbunge huyo ni mwanaume aende tena jijini London kama hatasimamishwa kizimbani na kuozea jela.”
 

Chanzo: Gazeti la uwazi

WANAFUNZI WA SHULE YA MANZESE WAKUMBWA NA "POPO BAWA"....30 WAMEANGUSHWA CHINI MUDA HUU

Wanafunzi wa shule ya secondary manzese zaidi ya 30 muda huu wanaanguka hovyo na kusema a maneno yasiyoeleweka kutokana na kinachohisiwa kuna nguvu za Giza zimetanda shuleni hapo huku wakijibamiza kwenye miti:

Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese aliyeanguka na kuweweseka.

Mpaka sasa haijafahamika chanzo cha wanafunzi wa shule hiyo kukimbia ovyo,kuanguka na kuweweseka. Wadau  wa  mambo ya giza wanadai  ni  NGUVU ZA KICHAWI

Picha/Habari Zainab Chondo -ITV

WAARABU WATATU WALIOHUSISHWA NA MLIPUKO WA BOMU KANISANI WAMEACHIWA HURU

Raia watatu wa UAE waliokuwa wamekamatwa wakikuhusishwa na tukio la mlipuko wa Bomu huko Arusha wameachiwa  huru  na  wamesharejeshwa  nchini  mwao...
Taarifa  zinadai  kwamba, Raia  hao  hawahusiki  na  mlipuko wa bomu  hilo.Kilichotokea  ni  kwamba, siku ya tukio walikuwa  karibu na  eneo la kanisa  na  ndo  maana walikamatwa...
Raia hao  wameachiwa  kwa ushirikiano  mkubwa  wa  ubalozi  wa UAE na Tanzania
Unaweza  kutembelea  hii  link kwa  ripoti  kamili: 
<< Tanzania frees 3 Emiratis held after bombing: Report>>

MAJINA YA WATUHUMIWA WALIOACHIWA HURU PAMOJA NA RIPOTI YA POLISI KUHUSU BOMU LA ARUSHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA MAENDELEO YA UPELELEZI WA TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH – OLASITI JIJINI ARUSHA LILILOTOKEA TAREHE 05/05/2013
Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba mara ya mwisho nilipokutana nanyi niliwaahidi kwamba nitaendelea kuwapa mara kwa mara taarifa juu ta maendeleo ya upelelezi wa tukio la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu joseph mfanyakazi parokia ya olasiti tarehe 05/05/2013 na kusababisha vifo vya watu watatu(3) na wengine kudhaa kujeruhiwa.
Kama nilivyowaeleza hapo awali, baada ya tukio hilo jumla ya watuhumiwa tisa(9) walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani. Watuhumiwa haoa ni victor Ambros Kalist, (20), dereva wa bodaboda na mkazi wa kwa Morombo; Yusuph Lomayani Josee (18) mwendesha bodaboda mkazi wa kwa Morombo na George Bathlomeo Silayo (23) mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti.
Watuhumiwa wengine waliokamatwa ni raia watatu toka nchi za falme za kiaruabu (UAE) Abdul Aziz Mubrak (30) mfanyakazi wa mamlaka ya mapato katika falme za kiarabu, Fouad Saleem Ahmed Al Hareez Al Mahri (29) mfanyakazi wa kikosi cha zimamoto katika Falme za Kiarabu, Saeed Abdulla Saad (28) askali polisikitengo cha traffic katika falme za Kiarabu, pamoja na raia mmoja wa Saudi Arabia Al-Mahri Saeed Mohseens (29)
Rai hao wa kigeni walikamatwa pamoja na wenyeji wao wawili ambao ni raia wa tanzania wenye asili ya Yemen.  Majina ya watanzania hao ni Mohamed Suleiman Saad, (38) mkazi wa ilala jijini Dar es Salaam na Jasm Mubarak (29) mkaazi wa mtaa wa Bondeni jijini Arusha.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na timu ya upelelezi ukihusisha taaasis nyingine za upelelezi FBI pamoja na INTERPOL kuhusiana na tukio hilo la mlipuko wa bomu kanisani umebaini kuwa raia hao wanne wa kigeni hawakuhusika katika shambulio hilo. 
Baada ya jalada la tukio hilo kufikishwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali Arusha – divisheni ya mashtaka imeelekeza kuwa watuhumiwa hao wakabidhiwe ofisi za idara ya uhamiaji mkoa wa arusha ili kuona kama kuna taratibu zozote za kiuhamiaji ziikiukwa na wageni hao wakati walipoingia nchini ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa dhidi yao. 
Pia ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imeandaa mashitaka dhidi ya victor S/O Ambros kalisti na amefikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za mauaji na kujaribu kuua. Uchunguzi dhidi ya watuhumiwa waliosalia unaendelea kwa sasa tunao wataalamu kutoka kenya na Uganda ambao tunashirikiana nao katika upelelezi wa shauri hilo.
Aidha, hadi sasa idadi ya majeruhi wa tukio hilo la mlipuko wa bomu wanaoendelea kupata matatibabu katika hospitali mbalimbali ni 31 ambao kati yao 19 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mount Meru arusha, 4 katika hospitali ya St. Elizabeth arusha na wengine 8 katika hospitali ya taifa muhimbili jijini dar es salaam na taarifa zinaonyesha hali zao zinaendelea kuimarika.
Hata hivyo jeshi la polisi linaendelea kufuatilia taarifa za watuhumiwa wengine wanaohusishwa na tukio hilo ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani pia jeshi la polisi linaendelea kuwaomba wananchi au raiayeyote mwenye taarifa zitakazowezesha kubaini mtandao wa kigaidi nawatuhumiwa wengine wanaohusika na tukio hilo wajitokeze na kuwasilisha taarifa hizo; tayari mkuu wa jeshi la polisi (IGP) amekwishaahidi zawadi nono ya Tshs. 50,000,000/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa hizo za siri kwa kukamatwa kwa watu hao.
 ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
LIBERATUSI SABAS – ACP
TAREHE 13/05/2013.

Waondoka katika makao ya wizara Libya

 13 Mei, 2013 

Watu waliokuwa wamejihami na ambao wanataka washirika katika utawala wa aliyekuwa rais Muamar Gaddafi, kufurushwa kutoka serikalini, hatimaye wameondoka katika makao ya wizara mbili za serikali mjini Tripoli.
Waziri wa sheria Salah al-Marghani alithibitishia BBC kuwa watu hao waliweza kuondoka kutoka ofisi za wizara hizo, ile ya mambo ya nje na na ile ya sheria.
Watu hao walizingira majengo hayo wiki mbili zilizopita wakiwa wamejihami kwa zana nzito za kivita.
Bunge ilipitisha sheria mpya wiki jana inayozuia waliokuwa washirika wa Gaddafi kutoshikilia nyadhifa zozote za kisiasa.
Takriban watu 1,000 waliandamana nje ya makao ya wizara ya mambo ya nje mnamo siku ya Ijumaa lakini baadhi walishambuliwa na kuchapwa , huku mabango yao yakiraruliwa na watu hao waliokuwa wamejhihami.

Ombi la Waziri

Bwana Marghani alisema kuwa wizara yake sasa iko chini ya polisi wa idara za mahakama na kuwa wafanyakazi walirejea kazini siku ya Jumamosi kwa masaa machache.
''Tunatumai kuwa hili halitatokea tena na kuwa ni funzo kwetu kuwa hatupaswi kuingilia shughuli za taasisi za kitaifa,'' alisema waziri huyo.
Alisema kuwa mwafaka umefikiwa kuwa wizara ya mambo ya nje itaweza kukabidhiwa kwa maafisa wakuu ifikapo Jumapili.
Nia ya watu hao ilikuwa kutaka serikali kuwatenga waliokuwa washirika wa Gaddafi na kutowapa nyadhifa kuu serikalini.
Tangu kutokea kifo cha Gaddafi, mji wa Tripoli pamoja na miji mingine, imekumbwa na ghasia pamoja na makabiliano.
Serikali imekuwa ikijaribu kuvunja magenge ya wahalifu ambayo yaliundwa wakati wa vita vilivyoiangusha serikali ya Muamar Gaddafi.
Mswaada uliopitishwa na bunge ulikosolewa kwa kutokuwa ingawa imekubalika kuwa sheria na huenda ikaathiri mamafisa kadaa wa serikali wanaohudumu kwa sasa.

" HAKUNA KANISA LILILOSHAMBULIWA KWA BOMU JIJINI DAR LEO "...HII NI KAULI YA KAMANDA KOVA

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema Taarifa zilizoenea kwamba Bomu limelipuka katika Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania (KKKT), Kunduchi jijini Dar es Salaam zimeenea ndivyo sivyo na kwamba askari walikuwa wanapambana na majambazi.

Wakati taarifa zikiwa zimesambaa katika mitandao ya kijamii na mitaani kwamba kuna kanisa la KKKT limeshambuliwa na bomu hivi punde, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kova amesema kwamba taarifa hizo sio za kweli na kwamba askari wa jeshi la polisi walikuwa wanapambana na majambazi karibu na eneo la kanisa hilo. 


Katika mapambano hayo polisi waliwarushia majambazi hayo bomu ili kuyakamata.

"Wakati askari wetu wanapambana na majambazi hayo- waumini wa kanisa hilo wamejitokeza kuwasaidia askari wetu. Naomba unisaidie kukanusha siyo kweli, nitazungumza na vyombo vingine vya habari kuweka sawa," amesema Kamanda Kova hivi Punde.


May 11, 2013
Guatemala's Rios Montt found guilty of genocide
Former Guatemalan leader Efrain Rios Montt in court. 10 May 2013 Efrain Rios Montt denied the charges against him

Related Stories

A court in Guatemala has found former military leader Efrain Rios Montt guilty of genocide and crimes against humanity.
A three-judge tribunal sentenced the 86-year-old to 80 years in prison.
Rios Montt was convicted of ordering the deaths of 1,771 people of the Ixil Maya ethnic group during his time in office in 1982 and 1983.
Survivors described horrific abuses committed by the army against those suspected of aiding left-wing rebels.

Analysis

When the Guatemalan Peace Accords were signed in 1996 after a civil war in which 200,000 people were killed, very few ever thought this moment would be reached.
In blisteringly critical language, Judge Jazmin Barrios said that as de facto president it was logical that Rios Montt knew of what was happening in the country, but did nothing to stop it.
Hunger, systematic rape and forced displacements were all used as tools of war against the Ixil people for whom merely being a member of the indigenous group was a "mortal offence" in the military government's brutal pursuit of left-wing guerrillas.
Judge Barrios's summary and subsequent sentencing of Rios Montt was everything that human rights organisations and victims' families' groups in Central America had been hoping to hear for decades. Now the 86-year-old former general is facing the rest of his life in prison, though he is almost certain to appeal on the grounds of his age.
The retired general had denied the charges, saying he neither knew of nor ordered the massacres while in power.
He is expected to appeal against the court's decision on the grounds of his age.
Rios Montt's former chief of military intelligence, Mauricio Rodriguez Sanchez, who was on trial with him, was acquitted.
It is the first time a former head of state had been found guilty of genocide by a court in his or her own country.
Other genocide convictions have been handed down by international courts.
Relatives and indigenous leaders cheered when the sentence was read out by Judge Jazmin Barrios in Guatemala City.
Rios Montt was sentenced to 50 years for genocide and 30 years for crimes against humanity.
"The Ixils were considered public enemies of the state and were also victims of racism, considered an inferior race," Judge Barrios said.
People celebrate conviction of Rios Montt. 10 May 2013 There were cheers in the court as the verdict was read out
"The violent acts against the Ixils were not spontaneous. They were planned beforehand."
The BBC's Central America correspondent Will Grant says it is a historic decision and a huge breakthrough for human rights in the region.
During the nearly two-month trial, dozens of victims gave harrowing testimony about atrocities committed by soldiers.
An estimated 200,000 people were killed in Guatemala's 1960-1996 civil war, the vast majority of them indigenous Mayans.
Prosecutors said Rios Montt presided over the war's bloodiest phase. They said he turned a blind eye as soldiers used rape, torture and arson against those suspected of supporting leftist rebels.
The trial has been beset with delays, legal loopholes and a temporary suspension.

PONDA AANZA UCHOCHEZI TENA....ANATAKA SERIKALI IANZE KUUA WAKRITO NA AMEDAI NECTA HUWAFELISHA WAISLAMU


Wakizungumza kwenye msikiti wa mtambani Kinondoni mara baada ya swala, Sheikh ponda na ustaadh mukadam  wameapa kupambana hadi dakika ya mwisho. 
Mukadam amemsifia Allah kwa kuwapa adhabu ya ugonjwa,watu kadhaa akiwemo  mkubwa mmoja  alie mahututi Afrika kusini(wanadai  eti alihusika kuwatengenezea mashtaka),na afisa mwingne wa jeshi kufarik ajalini baada ya kuwanyanyasa selo!
KAULI ZA SHEIKH PONDA.

Alitamka  kuwa :"Nitapambana hadi mwisho' huku watu wakisema takbir alah akbar! Amesema Wakristo wanapendelewa na serikali. Serikali ilisema aliekojolea kuran ni mtoto,wakati yeye kawakuta watoto jela akiwemo wa miaka 10,aliyekwapua mkoba.,ila yule mkristo wa miaka 14 serikali ilisema mtoto na haikumchukulia hatua zozote!


Pia kasema ana CD zikionyesha jinsi serikali inavyoua na kupanga kukandamiza uislamu. Kampongeza sana Zitto kabwe kwa mchango wake wa kutetea uislamu bungeni na kamponda yule aliepeleka cd alizoita za uchochezi bungeni! 


Karudia tuhuma za kuwa NECTA kuna udini na Waislamu wanafelishwa! Kasema serikali inapendelea na kuendeshwa na wakristo. Pia kuhusu bomu la Arusha kasema, wamekamatwa waarabu ,mbona hawajakamata wazungu? Anasema huo ni mpango wa kuonea waarabu na uislamu!

Ponda  kasema wakristo hajawahi kuuawa na serikali,ila waislamu yu ndo wanauawa! Mwembechai waliuawa, Pemba waliuawa. Anadai hata Pemba Waislamu waliuawa na serikali ikitumwa na Kanisa! 



Amehoji,mbona hatujawahi kusikia mchungaj au padri 
kauawa?kasema pemba kuna helcopter zilikua zinalipua majahazi ya waislamu(wakiwa baharini) wakati wanakimbilia Mombasa naTanga.!

Pia kasema,nchi hii hakuna udini,ila kuna mapambano ya waislamu kudai haki zao na redio iman imefungiwa kuwaonea waislamu wasipate pakusemea



 May 9, 2013
MASHOGA YAFUMANIWA GESTI YA TANDIKA JIJINI DAR YAKIFANYA UCHAFU

MWANAUME aliyefahamika kwa jina la baba Salome, mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alimdhalilisha mkewe (mama Salome) baada ya kufumaniwa gesti akiwa na mwanaume mwenzake ambapo madai yalisema, walikuwa katika hatua za mwisho za kuingiliana kimwili...
 
Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam. Awali ilidaiwa kuwa, mwanaume huyo na baba Salome mwenye mke na watoto wawili wanaomtegemea kwa kila kitu, walionekana wakiingia kwenye gesti moja ambayo pia ipo maeneo hayo hali iliyozua maswali kwa watu waliokuwa wakiwafahamu. 
 
“Unajua tatizo lilianzia wapi? Baba Salome na yule mwanaume mwenzake walionekana wakiingia gesti moja kisha wakatoka, wakaingia nyingine pia wakatoka, ndipo watu wanaowafahamu wakajiuliza kulikoni wawili hao kutembelea gesti siku hiyo, wakawafuatilia,” alisema mnyetishaji mmoja. 
Akaendelea: Lakini watu waliwafahamu kwa namna mbili tofauti, baba Salome ni mtulivu, mwadilifu, mwenzake watu wanasema ana ‘katabia’ ka kutaka kuwa faragha na  wanaume wenzake bila kujulikana nini anakitaka katika usiri huo. 
 Madai zaidi yakawekwa wazi kwamba, baadhi ya watu walikwenda kwenye gesti walizokwenda wawili hao na kuulizia nini walikuwa wanakitaka, ndipo siri ikawekwa wazi kwamba wanatafuta chumba cha kupumzika kwa siku hiyo lakini kwa sheria za Jiji la Dar es Salaam (kama siyo za nchi nzima), wanaume wawili hawaruhusiwi kulala chumba kimoja.
  
Chanzo kikasema: Wambeya wakawaona wakiingia kwenye gesti ya tukio, wakapewa chumba. Ndipo wakakimbia nyumbani kwa baba Salome na kumtonya mkewe, mama Salome kwamba mumewe ameingia gesti. 

Kichekesho zaidi kinaangushwa kwamba, baada ya kuambiwa mumewe amezama gesti, mama Salome ambaye ndiyo kwanza alikuwa amefika kutoka  kwenye mikopo ya Finca, alitoka mbio huku akisema anakwenda kumtoa sikio la kulia Kidawa akiamini mumewe ameingia gesti na mwanamke huyo. “Watu walimwambia mumewe hakuingia gesti na Kidawa bali mwanaume mwenzake. Kwanza mama Salome aliomba asitaniwe juu ya hilo, lakini akasisitiziwa,” alisema mtoa habari huyo. 
Akizungumza kwa jazba na waandishi wetu nje ya gesti hiyo, mama Salome alisema kwamba alipata taarifa siku nyingi mumewe ana ukaribu na mwanaume huyo ambaye mitaani watu wanasema  anajihusisha na vitendo vya ushoga. 
 
“Nilipozipata taarifa hizi sikuziamini, nilidhani ni Kidawa ndiyo kaingia gesti na mume wangu, maana Kidawa ndiye mbaya wangu,” alisema mwanamke huyo kisha akazama ndani ya gesti akiwa na polisi ambao haikujulikana walikotokea. 
Huku mumewe na mwanaume mwenzake wakiwa hawana hili wala lile kule chumbani, mlango ulisukumwa na kufunguka ambapo mwanamke huyo aliwakuta wawili hao wakiwa wameshavua baadhi ya nguo. 
Wote walishtuka kuona wameingiliwa!  “Yaani roho inauma sana, sijui ni kitu gani umekosa kwangu mpaka unakuja kwa mwanaume mwenzako jamani baba Salome,” alisema huku akilia mama Salome. 
Baada ya kugundua wamenaswa, mwanamke aliyekuwa na baba Salome aliangua kilio huku  akiomba kusamehewa kwa vile yeye ni mume wa mtu, lakini kilio chake hakikusikika kwa polisi ambapo waliwafunga pingu na kuwataka kuelekea katika kituo cha polisi. 
Wakati wakitoa maelezo kwenye kituo cha polisi, mwanaume aliyekuwa na baba Salome alijitambulisha kwa jina la  Julius Mwita, mkazi wa Devi’s Corner ana  mke na watoto wawili na aliwaomba sana waandishi wamhifadhi kwani wakwe zake wakimuona ‘itakula  kwake’. 
“Jamani nipo tayari kwa lolote naomba sana tuyamalize hapahapa, mimi ni mume wa mtu, wakwe zangu wananiheshimu na kunithamini sana,” alisema Mwita.  
Hata hivyo, pamoja na kilio hicho mwanaume huyo aliishia kuswekwa lupango na baadaye kuhamishiwa katika Kituo cha Polisi cha Chang’ombe kwa hatua zaidi. 


May 9, 2013
WAZEE WATATU WAKICHOMWA MOTO HADHARANI KWA MADAI KWAMBA NI WACHAWI

Hii ni marudio na ni kumbukumbu ya unyama waliotendewa vikongwe watatu na wanakijiji kwa madai kwamba ni wachawi.... 
Vikongwe hao walipewa adhabu kali ya kuchapwa hadharani na kisha kuchomwa moto..... 
Itazame video ya tukio hilo la kinyama.  

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA



DSCN2227 
Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
DSCN2220 
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
DSCN2228 
Ulinzi umeimarishwa
DSCN2252 
Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
DSCN2246 
Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
DSCN2282 
Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
DSCN2258 
Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
DSCN2273 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa. Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
DSCN2236 
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao wakiwa ni majeruhi.
DSCN2251
DSCN2267 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
DSCN2276
DSCN2255
DSCN2281
DSCN2225
DSCN2222
DSCN2215
DSCN2218
DSCN2219

BREAKING NEWS: KANISA KATOLIKI LALIPULIWA NA BOMU JIJINI ARUSHA WAKATI MISA IKIENDELEA


Taarifa  zilizotufikia  hivi  punde  ni  kwamba  bomu  limelipuka  katika  kanisa  katoliki, parokia  mpya  ya Olasisi  iliyokuwa  inazinduliwa  leo  jijini  arusha.....


Bomu  hilo  limelipuka  wakati  waumini  wa  kanisa  hilo  wa  wakijiandaa  na  misa  ya  uzinduzi  wa  parokia  hiyo....
 
Mpaka  sasa  haijajulikana  idadi  kamili  ya  watu  waliojeruhiwa  ama  kupoteza  maisha  lakini taarifa  za  awali  zinasema  kuwa  baadhi  ya  majeruhi  wamekimbizwa  hospitali

Chanzo  cha  mlipuko  huo  inasemekana   kuwa  kuna  gari  ndogo  ilifika  kanisani  hapo  na  kusimama....


Baadae  alishuka  mtu  aliyekuwa  amevalia  vazi  mithili  ya  kanzu  na  kurusha  kitu  kuelekea  kanisani  ambacho  ndicho  kilichosababisha  mlipuko  huo..


Mgeni rasmi   katika  uzinduzi   huo  alikuwa  ni   balozi wa Vatican nchini Tanzania.Yupo  baada  ya kunusurika  katika  mlipuko huo

Hizi ni taarifa za awali tu. Taarifa kamili itawekwa itakapopatikana. Tafadhali endelea kusikiliza Redio Maria Tanzania (inasikika pia online muda huu wakiwa wanatangaza kuhusu tukio hili )

Sir Alex Ferguson astaafu!

 8 Mei, 2013 - Saa 09:56 GMT
Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza, Premier League ,Manchester United, wametangaza kwamba, Sir Alex Ferguson atastaafu kama meneja wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Sir Alex anatajwa kuwa ndiye meneja mwenye mafanikio makubwa katika historia ya soka la Uingereza.
Tangu alipojiunga na klabu hiyo mnamo mwaka 1986, ameshinda mataji mawili ya Klabu Bingwa Barani Ulaya, mataji kumi na tatu ya Ligi Kuu na Kombe la FA mara tano.
Katika taarifa yake, Sir Alex amesema ni muda muafaka kwake kustaafu wakati klabu ikiwa imejizatiti katika nafasi nzuri. Atabakia Manchester United kama mmoja wa wakurugenzi na balozi.

Waasi wa PKK waanza kuondoka Uturuki

 8 Mei, 2013 - Saa 13:06 GMT

Waasi wa PKK wa Uturuki

Wapiganaji waasi wa Kikurdi wameanza kuondoka kusini mashariki mwa Uturuki kwenda kwenye ngome zao nchini Iraq chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano, kimeeleza chanzo cha habari cha Wakurdi.

"Tunafahamu kwamba, wameanza kuondoka," Selahattin Demirtas, mwanasiasa wa Kikurdi aliyeshiriki katika mchakato wa amani ameliambia shirika la habari la AFP.

Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi (PKK) kilitangaza mwezi uliopita kwamba, wapiganaji hao wataondoka kwa awamu kuanza mapema Mei .

Zaidi ya watu 40,000 wameuawa katika mapigano ya miaka 30 ya kuipinga Uturuki.

Gultan Kisinak, ambaye ni naibu kiongozi wa Chama cha Amani na Demokrasia (BDP) pamoja na Bwana Demirtas waeliambai shirika la habari la Associated Press kwamba, kundi la kwanza la wapiganaji limeanza kuelekea upande wa kaskazini mpakani na Iraq.

Inaaminika kwamba, chama cha PKK kinawapiganaji wanaofikia 2,000 ndani ya Uturuki na itawachukua muda wa miezi minne kwa wote kuondoka kabisa nchini humo.

Wanatarajiwa kuvuka mpaka kwa miguu na kuelekea kwenye ngome zao katika milima ya Qandil nchini Iraq.

Abdullah Ocalan kiongozi mkongwe wa PKK aliyeko gerezani nchini Uturuki, aliamuru kuondoka kwa wapiganaji wake mwezi Machi kama sehemu ya majadiliano ya amani na serikali ya Ankara.

Msemaji wa PKK, Bakhtiyar Dogan, ameliambia gazeti la Uturuki la Hawlati kwamba, kati ya wapiganaji 200 hadi 500 wataondoka siku ya Jumatano.

Amesema wapiganaji hao wataondoka kutoka maeneo ya Semdinli na Sirnak ya Uturuki wakiwa katika makundi matatu.

Kwa mujibu wa AFP, wapiganaji wa PKK walilalamika kuwa katika kilele cha siku ya kuondoka kwao, Uturuki iliongeza idadi ya wanajeshi wake eneo la mpakani na ilikua ikirusha ndege za doria.
Wamedai kuwa vitendo kama hivyo vinachelewesha mchakato wa amani na kuchochea uchokozi na mapigano.

Hata hivyo jeshi la Uturuki halijathibitisha iwapo hatua za ziada zimechukuliwa lakini limesema mapambano yake dhidi ya ugaidi yanaendelea.

Kaimu kiongozi wa PKK, Murat Karayilan, Aprili mwaka huu alionya kuwa wapiganaji wake watajibu na shughuli ya kuondoka ingesitishwa endapo wangeshabuliwa.

Wakati wa kuondoka mwaka 1999, jeshi la Uturuki liliwashambulia waasi hao na kuwaua wapiganaji wake 500.

Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, mara kadhaa ameahidi kuwa, jeshi halitamshambulia mpiganaji yeyote wa PKK atakayekuwa anaondoka.

Siku ya Jumanne, Bw. Erdogan alisema kuwa, kuweka silahachini ndio kiwe kipaumbele cha kwanza ili mchakato wa amani uweze kufanikiwa.

Askari wa Umoja wa Mataifa auawa DRC

 8 Mei, 2013 


Majeshi ya Umoja wa Mataifa wanaohudumu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Askari ambaye ni raia wa Pakistan katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,(DRC), ameuawa katika shambulio la kushtukiza.
Msafara wa Umoja wa Mataifa ulishambuliwa na watu wasiojulikana mashariki Kusini mwa jimbo la Kivu Jumanne jioni, msemaji wa UN Martin Nesirky amesema.
Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki – Moon ameshutumu shambulio hilo akisema mauaji ya askari huyo wa kulinda amani ni uhalifu wa kivita.
Kuna askari wapatao 19,000 wa UN nchini DRC ambako vikundi kadhaa vyenye silaha vinaendesha shughuli zake katika eneo la mashariki lenye utajiri mkubwa wa madini.
Katika taarifa yake, Bw. Nesirky amesema Bwana Ban ameshutumu vikali mauaji hayo na kueleza kuwa yanashtakiwa chini ya sheria za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Ameongeza kuwa, Katibu Mkuu wa UN ameitaka serikali ya DRC kuwachukulia sheria wahusika wa mauaji hayo.
Mnamo Machi mwaka huu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha mpango wa kupeleka kikosi cha askari 2,500 mashariki mwa DRC kusimamia amani na kuvinyang’anya silaha vikundi vya waasi.
Mapigano ya hivi karibuni ya kikundi cha waasi cha M23 yalianza mwaka mmoja uliopita Kaskazini mwa mkoa wa Kivu na kusababisha watu wapatao 800,000 kuyakimbia makazi yao.

Nigeria:watu 55 wauawa katika shambulio

 8 Mei, 2013 - 

Shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na wafuasi wa Boko Haram
Jeshi nchini Nigeria limesema watu hamsini na watano wameuawa huko kaskazini mashariki mwa Nigeria katika mashambulio yaliyofanywa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.
Taarifa zinasema, wafungwa 105 walitoroshwa katika shambulio hilo mapema alfajiri lililotokea katika jimbo la Bama, Borno.
Aidha, mashahidi na jeshi linasema kituo cha polisi cha Bama, majengo ya serikali na kambi za kijeshi ziliteketezwa kwa moto.
Habari zinasema, mashambulio ya makundi yenye msimamo mkali ni ya kawaida katika jimbo hilo lakini kiwango cha umwagaji damu kilichotokea katika shambulio la sasa ni cha kutisha.
Mwandishi wa BBC jijini Lagos, Will Ross, anasema shambulio hilo linafuatia mashambulio mengine mabaya siku za nyuma linakinzana na taarifa kwamba, operesheni za kijeshi dhidi ya wanamgambo hao zimepunguza tishio la Boko Haram.
Rais Goodluck Jonathan ameunda kamati itakayopitia masharti ya msamaha kwa waasi hao lakini kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, mpaka sasa amekataa wazo hilo.
Msemaji wa jeshi, Musa Sagir, aliyeko mji wa Maiduguri takriban kilomita 70 kutoka Bama, amedai kuwa, shambulio hilo siku ya Jumanne katika mji huo mdogo lilianza baada ya watu 200 wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Boko Haram wakiwa na silaha nzito kuwasili katika mabasi na magari madogo saa 11 alfajiri.
Msemaji huyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, baadhi ya watu hao wenye silaha walishambulia kambi za jeshi lakini walirudishwa ambapo kumi kati yao waliuawa na wawili kukamatwa.

Polisi pia wauwa

“Lakini watu hao walivamia gereza , na kuwaachilia wafungwa 105, na kuwauwa walinzi wote wa gereza waliokuwa nje isipokuwa wale waliojificha ndani ya stoo ya ya kuhifadhia vyombo vya kupikia,” ameongeza.
Baadhi ya washambuliaji hao walivalia sare maalum za kijeshi na walishambulia kwa takriban saa tano.
Maafisa wa polisi 22, walinzi 14 wa gereza, wanajeshi wawili na raia wane inasemekana wameuawa katika shambulio hilo pamoja na wafuasi 13 wa Boko Haram.
Kamanda wa polisi wa Bama, Abubakar Sagir amekaririwa akisema kuwa, miongoni mwa raia hao walikuwemo watoto watatu na mwanamke mmoja.
Kama linavyofahamika, kundi la Boko Haram, lina mizizi yake katika mkoa huo wa Nigeria. Linapigana kuipindua serikali ili kuunda taida la Kiislamu.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, jeshi la Nigeria lilianzisha mashambulizi ya kuwasaka wanamgambo hao katika majimbo ya Baga na Borno, baada ya wapiganaji wa Boko Haram kushambulia msafara wa kijeshi.
Watu wapatao 200 waliuawa katika msako huo na maelfu ya majengo kuharibiwan hali iliyosababisha makundi ya kutetea haki za binadamu kudai kuwa, jeshi lilitumia nguvu kupita kiasi. Jeshi lilitangaza kuwa watu waliokufa walikuwa 37.

"TUNALAZIMIKA KUTUMIA 0718 TUKIWA KATIKA SIKU ZETU HUKU POLISI NAO WAKITUINGILIA KWA NGUVU"....MAKAHABA

Jana CLOUDS FM iliripoti kuhusu kushamiri kwa Biashara ya Ngono katika Maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam  na  jinsi  serikali  inavyolishughulikia  tatizo  hilo  linalokua  kwa  kasi....

Wakihojiwa  kwa  nyakati  tofauti, baadhi ya wasichana wanaojishughukisha na biashara hiyo wameelezea changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kazi hiyo hususani nyakati za usiku.

Wakizungumzia adha wanazokutana nazo Wasichana hao wamesema kuwa licha ya kukabiliwa hali ngumu ya maisha iliyopelekea kuingia katika biashara hiyo, bado wamekuwa wakikutana na matukio mabaya ikiwemo kukamatwa na kuingiliwa kinguvu na baadhi ya watu wanaojitambulisha kwao kuwa ni askari wa Polisi jamii.
Mbali na hilo Wasichana hao wamesema hali ngumu ya Maisha imekuwa ikiwalazimu kufanya mapenzi kinyume na maumbile wanapokuwa kwenye Hedhi, pasipo kujali hatari ya kukumbwa na maradhi yoyote.


Hivi karibuni Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni lilitangaza mpango wa kuwaondoa wasichana wamaojishughulisha na Biashara ya ngono mitaani na kuwashtaki kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya uvunjifu amani na ukiukwaji wa maadili.




Wakizungumza baadhi ya wadau kutoka mashirika na Taasisi mbalimbali za kutetea haki za Binadamu nchini, ambapo kituo cha Sheria na haki za Binadamu pamoja na taasisi ya kutetea haki za Binadamu ya Chuo Kikuu cha Tumaini, kimesema kuwa kitendo cha kuwakamata wasichana hao hakiwezi kuwa suluhisho la kutokomeza Biashara ya ngono nchini.

 
Eneo la MANZESE Uwanja wa Fisi ni miongoni mwa Maeneo ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam limeliainisha kuwa limekuwa likikithiri kwa Biashara hiyo.


No comments:

Post a Comment