Saturday, May 11, 2013

Tutu aacha kuunga mkono ANC

Askofu mstaafu wa Cape Town, Afrika Kuisni, Desmond Tutu, amesema hatapigia kura tena ANC, chama tawala cha nchi hiyo.
Desmond Tutu
Katika makala aliyoandika kwenye magazeti ya Mail na Guardian, Desmond Tutu, aliyepewa tuzo ya Nobel ya amani, alisema ANC iliongoza vema vita vya ukombozi lakini haikufanikiwa kuwa chama cha kisiasa.
Alitoa mfano wa tofauti baina ya maskini na matajiri, fujo na rushwa kuwa sababu zinazomfanya kuacha kuunga mkono chama hicho.
Zamani Desmond Tutu alikuwa mfuasi mkubwa wa chama hicho lakini katika miaka ya karibuni amekilaumu kwamba hakikushughulikia watu wa kawaida.

Hewa ya Ukaa yaongezeka duniani.

 11Mei, 2013

Moshi unaotengeneza hewa ya Ukaa

Kiwango cha hewa ya ukaa kimeongezeka na kufikia kiwango cha juu zaidi duniani.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya mwanadamu kipimo cha kiwango cha hewa ya Ukaa kuongezeka na kufikia mia nne kwa milioni moja ya sehemu za dunia.
Kwa mujibu wa takwimu za maabala ya serikali ya Marekani huko Hawaii, wamesema kiwango hicho kimekuwa kutokana na sababu mbalimbali.
Mara ya mwisho hewa na Ukaa kufikia kiwango cha juu ilikuwa miaka milioni tatu hadi milioni tano iliyopita ambapo ilikuwa chiniya mia nne kwa sehemu milioni moja za dunia(400ppm)
Wanasayansi hao wanasema pia kiwango cha joto kimezidi maradufu kuliko miaka iliyopita.
Hewa ya Ukaa inatajwa kama gesi inayotengenezwa zaidi na binadamu ambapo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa uongezekaji wa joto duniani kwa miaka mingi.
Wanaharakati wa masuala ya mazingira wamesema hatua hii ni pigo kubwa na kuonyesha wazi madhara ya mabadiliko ya tabia nchi.
Lakini wanaharakati hao wanasema vifaa vya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi vimeandiliwa na kupambana na tatizo hilo.

Pakistan yapiga kura kati ya ghasia

 11 Mei, 2013 - Saa 10:21 GMT

Wananchi wa Pakistan wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu baada ya kampeni zilizokuwa za fujo.
Wanawake wamepanga foleni kusubiri kupiga kura mjini Lahore
Na mauaji yameendelea siku ya upigaji kura; polisi mjini Karachi wanasema watu 11 wamekufa na zaidi ya 50 kujeruhiwa pale bomu liliporipuka nje ya ofisi ya chama cha Awami.
Na watu zaidi wamejeruhiwa kwenye shambulio katika mji wa Peshawar.
Lakini mwandishi wa BBC katika mji mkuu, Islamabad, anasema wapigaji kura wengi wamejitokeza na kukaidi vitisho vya Taliban kwamba watafanya fujo zaidi.
Vyama vinavyoongoza katika uchaguzi huo ni Pakistan Muslim League - cha waziri mkuu wa zamani, Nawaz Sharif - na Movement for Justice cha mcheza kriketi wa zamani, Imran Khan.