Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limekubali
kuisaidia Tanzania kuanzisha benki teule ya wakulima, gazeti la Daily
News la Tanzania liliripoti Jumatano (tarehe 5 Juni).
"Ahadi yangu kwenu ni kwamba FAO itawasiliana na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa kuona jinsi tunavyoweza kusaidia kuanzisha benki,"
Mkurugenzi Mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva alimwambia Rais wa
Tanzania Jakaya Kikwete.
Da Silva alisifu jitihada za Tanzania za kuwasaidia wakulima, lakini
alisema mkazo unapaswa kuwa katika kutoa mikopo kwa wakulima kuliko
ruzuku, ambazo aliziita si endelevu.
No comments:
Post a Comment