Friday, May 17, 2013

HAYA NDO MAJINA YA WANAFUNZI WA CBE NA UDSM WALIONASWA WAKIJIUZA ( MAKAHABA)


Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi  stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.

Washitakiwa hao waliokamatwa  katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.

Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.

“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.

Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa  hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea.

Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni.

Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa.

“Msako huo ulifanyika Maisha   Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema

Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.

Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo.

Wapiganaji Boko Haram wauawa Nigeria


 18 Mei, 2013

Wanajeshi wa Nigeria

Takriban wapiganaji 30, wa waasi nchini Nigeria, wameuawa kwenye mashambulio ya anga yaliyofanywa na jeshi la serikali, Kaskazini Mashariki mwa nchini hiyo.
Msemaji wa jeshi la Nigeria, amesema, ndege za kivita na helicopta zilitumika kushambulia kambi kadhaa wa waasi hao.
Aidha ameiambia BBC kuwa ndege moja ilishambuliwa kwa kombora na waasi hao lakini ilifanikiwa kurejea salama hadi kambi yao.
Serikali ya Nigeria ilitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ya Kaskazini Mashariki, yanayoshuhudia mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram.
Kwa sasa jeshi la Nigeria, linajaribu kutwaa uthibiti wa majimbo ya Adamawa, Yobe na Borno kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram.
Wakati huo huo, milipuko na milio ya risasi imesikika usiku kucka katika jimbo la Katsina.
Raia wameiambia BBC kuwa mabenki, vituo vya polisi na magerza yaliharibiwa kufuatia mapigano makali mjini Daura karibu na mpaka wa nchi hiyo na Niger.
Wanasema wameona miili ya wanajeshi watano na mitatu ya wapiganaji wa waasi lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa.
Mawasiliano ya simu ya mkononi yamekatizwa katika maeneo mengi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Lakini afisa mmoja wa serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa mitandao ya simu ilifungwa wakati wa operesheni hiyo ya kijeshi.