Saturday, June 1, 2013

Waandamanaji wavamiwa kanisani Zambia

 31 Mei, 2013 
Serikali inaodnoa ruzuku ili kupunguza matumizi ya pesa zake
Wafuasi wa chama tawala nchini Zambia, wamevamia kundi la waandamanaji waliokuwa ndani ya kanisa katika mji mkuu Lusaka
Waandamanaji hao waliokuwa wamepanga kufanya maandamano kupinga kuondolewa kwa ruzuku kwa bidhaa muhimu, walikusanyika kanisani baada kuzuiwa na polisi kuandamana.
Aidha wawili kati yao wamelazwa hospitalini baada ya kujeruhiwa vibaya, kwa mapanga na silaha zengine za kijadi.
Hatua ya serikali kuondoa rukuzu kwa bidhaa muhimu , imepokelewa kwa ghadhabu na watu nchini Zambia.
Waandamanaji walikuwa wameomba kibali cha kuandamana lakini wakanyimwa na polisi kwa sababu za kiusalama.
Kwa hivyo walilazimika kuhamishia maandamano yao kanisani, kwa sababu hawahitaji kibali cha kukusanyika kanisani
Uamuzi wa serikali wiki mbili zilizopita kufutilia mbali ruzuku kwa Unga wa mahindi, imesababisha kilio kutoka kwa wananchi ambapo asilimia 60 ya wananchi ni maskini, wakiwa wanaishi kwa dola tatu kwa siku.
Hatua hiyo hata hivyo ilinuia kupunguza matumizi ya pesa za serikali.
Serikali pia imesema kuwa waliokuwa wanafaidika zaidi na ruzuku ni maajenti wala sio watu maskini.

No comments:

Post a Comment