Askari
wa vikosi vya Ulinzi na Usalama kisiwani Pemba, wakiwa katika zoezi la
kuondoa miili ya Marehemu waliopoteza maisha katika ajali ya kuangukiwa
na ukuta wa tangi la maji Machomanne Chake Chake Pemba
Tangi la maji lilipo Machomane Chake Chake Pemba ambalo lilikuwa
kwenye harakati za kuangushwa na kujengwa upya, limeanguka na kuelemea
mafundi waliokuwa juu ya tangi hilo ambapo hadi jana watu watatu
wameripotiwa wamefariki dunia na tisa kujeruhiwa.
Miongoni mwa
waliofariki wametambuliwa kuwa ni Salumu Muhidini (35) Juma Rashid mkazi
wa Chanjani, na mmoja aliyejulikana kwa jina la maarufu la Golo (35).
Kwa mujibu wa taarifa za watu wakaribu wanasema ajali hiyo imetokea
kutokana na vifaa duni visyivokuwa na uwezo wa kufanyia kazi hiyo
ambayvo walikuwa wakivitumia mafundi hao.
Wananchi
mbali mbali wakiwa katika hospitali ya Chake Chake Pemba, wakitizama
miili ya ndugu zao waliopoteza maisha na majeruhi baada ya kuangukiwa na
mnara wa tangi la maji Machomanne Pemba
Wananchi
mbali mbali wakiuangalia mnara wa Tangi la maji Machomanne, ulioanguka
na kupoteza maisha ya wananchi watatu jana asubuhi huko Machomnne, Chake
Chake Pemba
Daktari
Bingwa kutoka Quba anayefanya kazi zake kisiwani Pemba, (jina
halikufahamika) akimtibu mmoja kati ya majeruhi waliolazwa katika
hospitali ya Chake Chake, kufuatia ajali ya kuangukiwa na ukuta wa mnara
wa tangi la maji Mchomanne Pemba
Picha zote kwa hisani ya Voice of Zanzibar(VoZ) na Abdi Suleiman wa Pemba
No comments:
Post a Comment