Friday, May 31, 2013

Neno La Leo: Katika Kila Tulifanyalo Tusiwasahau Watoto..




c1 88419

Ndugu zangu,

Picha hiyo nimeipiga jana nje kidogo ya kijiji cha Bungu, Rufiji. Macho ya mtoto huyu anayetuangalia yanatukumbusha pia wajibu wetu. Yale mema tunayopaswa kuifanyia nchi yetu tuliyozaliwa.

Maana, muda wetu wa kuishi hapa duniani ni mfupi sana. Tukitanguliza ubinafsi ina maana ya kuwaandalia mazingira mabaya ya kuishi, mtoto huyu na mamilioni ya watoto wa nchi hii. Hawa ni Watanzania Watu Wazima wa kesho na keshokutwa.

Jiulize, kama wazee wetu waliotangulia nao wangekuwa ni wabinafsi sana leo tungeikuta nchi ya namna gani? Tafakari.

No comments:

Post a Comment