Thursday, April 18, 2013

Karim Wade matatani kwa ufisadi

 18 Aprili, 2013 - Saa 12:06 GMT

Alikuwa waziri wa wizara nyingi hadi akaitwa waziri wa ardhi na anga
Mwanawe rais wa zamani wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade amezuiliwa na polisi baada ya kushtakiwa kwa kosa la ufisadi ambalo limehusishwa na mali anayomiliki.
Karim Wade amekanusha madai kuwa alijipatia takriban dola bilioni 1.4 kinyume na sheria wakati wa utawala wa babake.
Karim mwenye umri wa miaka 44 alikuwa waziri wakati wa utawala wa babake kutoka mwaka 2000 hadi 2012, na aliwajibika na wizara ya miundo mbinu pamoja na miradi ya kawi.
Bwana Wade anadaiwa kumiliki makampuni ya kigeni kwa njia haramu.
Alikamatwa Jumatatu, saa chache kabla ya mawakili wake kutoa stakabadhi za umiliki wa mali yake mahakamani.

'Waziri wa ardhi na anga'

Wendesha mashtaka walitangaza kuanzisha uchunguzi dhidi ya bwana Wade na mawaziri wengine watano wa zamani mwaka jana.
Hali hii ilianza kujitokeza baada ya Abdoulaye Wade kushindwa na rais Macky Sall katika uchaguzi wa Machi mwaka 2012 ambaye aliahidi kuangamiza ufisadi.
Wakati wa utawala wa miaka 12 wa Abdoulaye Wade, Karim Wade alishikilia nyadhifa kadhaa za waziri ikiwemo waziri wa miundo mbinu na usafiri wa angani.
Nyadhifa hizi zote alizoshikilia zilisababisha watu kumuita waziri wa anga na ardhi na pia ilimwezesha kusimamia kiwango kikubwa cha bajeti ya serikali

No comments:

Post a Comment