Saturday, April 20, 2013

Balozi Seif afungua rasmi Semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Z'bar kuhusu uimarishaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

20/4/2013.

 Photo: ZANZIBAR                                                     20/4/2013

 Balozi Seif  afungua rasmi Semina ya siku moja ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Z'bar kuhusu uimarishaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Watendaji wa Jeshi la Polisi Nchini wanapaswa kuendelea kutekeleza majukumu kwa nguvu zao zote ili kuwapa fursa Wananchi kuendelea na harakati zao za kimaisha za kila siku bila ya bughdha zozote.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiifungua semina ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar iliyoandaliwa na jeshi la Polisi Nchini Tanzania kuhusu maboresho ya jeshi hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Juu wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif alisema Jamii mara nyingi hujenga hofu wakati inapokabiliwa na matokeo tofauti yanayohatarisha maisha na mali zao na hii husababishwa  na matendo mabaya ya ujambazi wanayokuwa wakiyashuhudia katika baadhi ya maeneo yao.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliyatolea mfano matukio ya hivi karibuni ya ujambazi yaliyotokea Zanzibar ambayo mbali ya kujenga hofu kwa raia lakini pia yameitia dosari Zanzibar katika harakati zake za kuimarisha Sekta ya Utalii.

Alifahamisha kwamba kitendo hicho kimeleta mshituko kwa wawekezaji wa sekta hiyo ya utalii jambo ambalo linaonekana kuhatarisha biashara ya utalii inayoweza kuporomosha mapato ya Taifa.

Alilikumbusha Jeshi la Polisi pamoja na Viongozi kuelewa kwamba wana dhima ya kulinda maisha na mali za raia na kulitaka Jeshi hilo kujizatiti katika kutumia mbinu za Kisayansi wakati wanapokabiliana na wahalifu popote pale Nchini.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa Maaskari hao kuendelea kulinda siri za raia wema wanaojilotea kutoa taarifa za watu wanaohusika na ujambazi ili wajenge imani ya kulisaidia zaidi Jeshi hilo.

Balozi Seif alisema Wananchi walio wengi hivi sasa wanashindwa kushirikiana na Jeshi la polisi kwa kuhofia nusalama wao kutokana na wahalifu wanaowatolea taarifa vituoni kurejea ma majigambo mitaani huku wakitishia usalama wa maisha yao.

“  Wahalifu wanashikwa na kupelekwa vituoni kwa kutokana na msaada wa taarifa za Raia wema lakini baada ya saa chache unawakuta wahalifu hao wamerejea mitaani na majigambo kwa kuwatambia waliopeleka taarifa hizo kituoni. Sasa tujiulize usalama wa Raia hao wanaotoa taarifa hizo uko wapi “. Aliuliza Balozi Seif.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alilipongeza Jeshi la Polisi Zanzibar kwa hatua yake ya kuanzisha mpango maalum wa kushirikisha Jamii latika Ulinzi wa  pamoja { Polisi Jamii } { Ulinzi shirikishi } ambao unaonekana kuleta mafanikio kiasi.

Balozi Seif alisema mpango huo unafaa kuendelezwa zaidi kwani zipo dalili zinazoashiria kuwepo kwa hatua kubwa ya kiulinzi ambayo inaweza kupunguza au kuondosha kabisa matukio ya uhalifu katika maeneo mbali mbali hasa zile sehemu za Vitega uchumi.

“ Tumeshuhudia ndani ya maeneo yetu tunayoishi kupunguwa kwa matukio ya wizi, unyang’anyi na hata kuwepo kwa Vijana wanaojihusisha na matumizi ya  dawa za kulevya kutokana na uanzishwaji wa Vikundi hivi kwenye shehia tofauti Nchini “. Alifafanua Balozi Seif.

Naye akitoa shukrani zake kwa niaba ya Watendaji wa Jeshi la Polisi Nchini Mkuu wa Jeshi hilo Tanzania IGP Said Mwema alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya jeshi hilo baada ya kuanzishwa  mfumo mpya wa ushirikiano { Smart Partnership } ndani ya jeshi hilo.

IGP Said Mwema alisema lengo la uanzishwaji wa mfumo huo ni kuona Jeshi la Polisi Nchini linaboreka katika harakati zake za kulinda maisha na mali za wananchi hapa Nchini.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment