Tuesday, April 16, 2013

Karim Wade atiwa nguvuni kwa ulaghai

 16 Aprili, 2013 - Saa 08:07 GMT

Karim Wade
Mwanawe rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade, ametiwa nguvuni kwa kujipatia dola bilioni 1.4 wakati wa utawala wa baba yake .
Karim Wade ambaye alihudumu katika serikali ya baba yake alikuwa na nyadhifa mbali mbali wakati huo .
Wade aliwasilisha waraka wa orodha ya mali zake katika mahakama maalum ya senegali iliyopewa jukumu la kuchunguza kesi za ufisadi jana asubuhi.
Alipewa muda wa mwezi mmoja kuthibitisha kuwa alichukua zaidi ya dola dola bilioni kihalali wakati baba yake alipokuwa madarakani.
Karim Wade alipewa jina la bandia waziri wa anga na dunia , alipokuwa waziri wa miundo mbinu , mipango ya miji , usafiri wa anga na ushirikiano wa kimataifa kwa wakati mmoja.
Wakati huo pia alikuwa mkuu wa theluthi moja ya matumizi ya taifa . Mahakama ya Senegali bado haijaeleza sababu ya kumtia rumande na mawakili wa Karim Wade wamesema alichukuliwa kwa nguvu .

No comments:

Post a Comment