Thursday, April 18, 2013

Rais aunga mkono msamaha kwa Boko Haram

 18 Aprili, 2013 - Saa 09:20 GMT

Rais Jonathan alikuwa amepinga jambo la kuwapa msamaha wapiganaji hao
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amezindua kamati mpya itakayochunguza uwezo na utekelezwaji wa msahama kwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram.
Kamati hiyo itakuwa na siku sitini kufikia uamuzi wake wa mazungumzo na kuwapokonya silaha wapiganaji hao , kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ofisi ya rais.
Pia itaangazia nyenzo za kuwasaidia waathiriwa wa ghasia ambazo chanzo chake ni wapiganaji hao.
Boko Haram limewaacha maelfu wakiwa wamefariki kutokana na ghasia ambazo wamekuwa wakisababisha mara kwa mara tangu mwaka 2009.
Kamati hiyo ambayo wanachama wake 25 wanajumuisha maafisa wa kijeshi, wasomi na wanasiasa watajaribu kuangazia sababu zinazopelelea makundi kama Boko Haram kuafanya uasi na njia za kuwazuia.
Zaidi ya hayo, rais Jonathan ameidhinisha kuundwa kwa kamati nyingine ya serikali kuhusu kuwapokonya wapiganaji hao silaha katika jitihada zake za kuimarisha usalama na uthabiti wa nchi.

Hatua mwafaka

Viongozi wa kisiasa na kidini, kutoka Kaskazini mwa Nigeria, ambalo ndio kitovu cha uasi huo, hivi karibuni walipendekeza serikali kutoa msamaha kwa wapiganaji hao.
Rais Goodluck Jonathan alijibu kauli hiyo na mwanzoni mwa mwezi Aprili alikipa kikundi cha washauri wa usalama jukumu la kuangalia ambavyo msamaha unaweza kutolewa kwa wapiganaji hao.
Duru zinasema kuwa hoja hii ya msamaha ni muhimu kwani rais alikuwa ameipuuza mwanzoni.
Ni wazi kuwa rais ameitikia kuwa juhudi za kijeshi dhidi ya wapiganaji hao hazijazaa matunda.
Hata hivyo haijulikani ambavyo wapiganaji hao watatizama wazo la rais ikizingatiwa kuwa ni makundi mengi ya mirengo tofauti ya wapiganaji.
Wiki jana Boko Haram, ambao wanataka utawala wa kiisilamu Kaskazini mwa nchi limekataa pendekezo la msamaha kwao.


No comments:

Post a Comment