Mwanawe rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade,
ametiwa nguvuni kwa kujipatia dola bilioni 1.4 wakati wa utawala wa baba
yake .
Alipewa muda wa mwezi mmoja kuthibitisha kuwa alichukua zaidi ya dola dola bilioni kihalali wakati baba yake alipokuwa madarakani.
Karim Wade alipewa jina la bandia waziri wa anga na dunia , alipokuwa waziri wa miundo mbinu , mipango ya miji , usafiri wa anga na ushirikiano wa kimataifa kwa wakati mmoja.
Wakati huo pia alikuwa mkuu wa theluthi moja ya matumizi ya taifa . Mahakama ya Senegali bado haijaeleza sababu ya kumtia rumande na mawakili wa Karim Wade wamesema alichukuliwa kwa nguvu .
No comments:
Post a Comment