Saturday, May 18, 2013

MAALIM SEIF AFUNGUA RASMI MRADI MPYA WA MAJI NUNGWI.


maji

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amewataka wananchi wa Nungwi kuulinda na kuuenzi mradi wa maji safi na salama katika eneo hilo ili uweze kuwa endelevu.

Amesema mafanikio ya mradi huo yatachangia maendeleo ya kiuchumi katika eneo hilo na kuwa mfano kwa maeneo mengine ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Maalim Seif ametoa wito huo katika sherehe za ufunguzi wa mradi wa maji safi na salama unaotokana na mabadiliko ya tabianchi katika shehia ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema mradi huo ambao ni wa kihistoria katika eneo hilo unapaswa kulindwa na kuenziwa ili usiharibiwe na n kuweza kudumu kwa muda mrefu.
Amefahamisha kuwa mradi huo ni mkombozi kwa wananchi wa vijiji vya Nungwi hasa wanawake, na kwamba umeondoa kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi wa maeneo hayo.
Aidha Maalim Seif amewata watendaji wa Mkoa huo kutowaone muhali waharibifu wa mazingira wakiwemo wale wanaochukua mchanga katika maeneo ya fukwe na maeneo mengine yasiyoruhusiwa, wanaofanya uvuvi haramu pamoja na ukataji wa miti ovyo.
Ameeleza kuwa zaidi ya maeneo 148 ya kilimo Zanzibar yameainishwa kuvamiwa na maji ya chumvi na kuathiri shughuli za kilimo katika maeneo mbali mbali sambamba na kupungua kwa eneo la ardhi ya visiwa vya Unguja na Pemba.
Mara baada ya kufungua mradi huo, Makamu wa Kwanza wa Rais aliukabidhi kwa Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati ili aweze kuundeleza kwa maslahi ya wananchi hao.
Kwa upande wake Mwakilishi wa UNDP Tanzania Njeri Kamau amewapongeza wananchi wa Nungwi kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa mradi huo, na kuwataka kuendeleza umoja na mshikimano katika kutekeleza miradi mengine ya maendeleo.
Amesema ametiwa moyo na mafanikio yaliyopatikana kutokana na mradi huo na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali pamoja na wananchi wa Zanzibar katika kutekeleza miradi mbali mbali.
Nae Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Mhe. Ramadhan Abdallah Shaaban, amesisitiza kuwa mradi huo ni kwa ajili ya wananchi wa Nungwi na sio kwa shughuli za mahoteli.
Aidha amesema wanakusudia kuweka “stabilizers” katika vituo vya mradi huo ili kuepusha uunguaji wa pampu za maji unaotokea mara kwa mara, hali inayosababishwa na hitilafu za umeme.
Mapema akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Omar Dadi Shajak, amesema mradi huo ni mkubwa zaidi na umekuwa wa mwanzo kufunguliwa kati ya miradi minne unayotekelezwa chini ya mradi wa Mpango wa Mabadiliko ya Tabia nchi Afrika, African Adaptation Program AAP nchini Tanzania.
Amesema mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha lita thelathini elfu (30,000) kwa saa ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano (500), umefadhiliwa na serikali ya Japan kupitia ubalozi wake nchini Tanzania, UNDP chini ya usimamizi wa AAP.
Akisoma risala kwa niaba ya wananchi wa Nungwi, mwalimu Hassan Jani Massoud ameishukuru serikali kwa kuwapelekea mradi huo ambao utapunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Amesema kabla ya kuja kwa mradi huo, miradi mbali mbali ya maji ilianzishwa lakini haikuleta ufanisi, lakini mradi huo umeonesha kuleta mafanikio, na kwamba wananchi wa Nungwi wataondokana na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu.

CD ZA UAMSHO NA ZILE ZA SHEIKH ILUNGA ZAPIGWA MARUFUKU....


Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar inayoongozwa na Dr Shein na Makamu  wake Maalim Seif kupitia Jeshi la Polisi wamepiga marufuku rasmi CD  zote za mawaidha ya Kiislam za UAMSHO,MUJAHID ABOUD ROGO na SHEIKH ILUNGA.
 

Agizo hilo lilitolewa na OCD  wa  zamani Murtad MKADAM ambae kwa  sasa yupo ofisi kuu ya polisi kitengo cha madawa ya kulevya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif.

Alisema cd hizo za kiislam ni chanzo cha uvunifu wa amani hapa nchini na ndio zinazosababisha uchochezi baina ya dini ya ukiristo na uislam.


OCD alibainisha kuwa mpaka sasa wameshawakamata watu kadhaa wanaojihusisha  na  kuuza cd hizo na kuwaonya wale wote ambao huweka kuzisikiliza maana watachukuliwa hatua kwani serikali ina mkono mrefu.
...

Akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa kwamba waliowakamata hawawaoni kuwa wamewadhulumu kwa kufanya biashara halali ya uzaji cd, Ocd alijibu cd zile za mawaidha ni Haram wala sio riziki ya halali kwa upande wa serekali kwani zinapelekea uvunjifu wa Amani katika nchi.

Ajali ya mgodi watu 20 wafariki Congo

 18 Mei, 2013 
Ramani ya DRC
Zaidi ya watu 20 wamefariki dunia wakati mgodi mmoja uliporomoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mamlaka za Congo zinasema mgodi huo ulioko karibu na kijiji cha Rubaye katika mji wa Masisi Kaskazini mwa jimbo la Kivu uliporomoka siku ya Alhamisi Asubuhi.
Meya wa Masisi, Dieudonne Shishuku ameiambia BBC kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Amesema bado wanasubiri waokoaji maalumu wa vifaa vya kufukua ardhini waanze kazi ya ukoaji ambapo mgodi huo unakadiriwa kufikia mita 30 kwenda chini.
Shughuli zote za uchimbaji wa madini zimesimamishwa mjini humo.
Kumekuwa na shughuli za uchimbaji haramu wa madini kwenye mji huo ambao una utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu, madini ya chuma na coltan yanayotumiwa kwa simu lakini eneo hilo limekuwa na mapigano ya muda mrefu.
Faida inayotokana na mauzo ya madini nchini humo, yanaaminika kuchangia pakubwa katika mzozo unaokumba Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo wakiwa masikini.

Wapenzi wa jinsia moja wabaguliwa Ulaya


18 Mei,

Wapenzi wa jinsia moja huhofia kuripoti kwa polisi visa vya dhulma dhidi yao
Muungano wa Ulaya umetoa ripoti kuonyesha kuwa zaidi ya robo ya wapenzi wa jinsia moja waliohojiwa wameshambuliwa ama kutishwa katika miaka mitano iliyopita.
Ripoti hiyo iliandaliwa na wataalamu wa muungano huo kuboresha sera zinazoelekea kutenga watu kutokana na hulka zao za mapenzi.
Watu elfu tisini na tatu wanaoishi Ulaya walihojiwa kuhusu namna wapenzi wa jinsia moja wanavyochukiwa na kutengwa. Majibu yao yaliyowasilishwa kwenye mtandao yalionyesha katika miaka mitano zaidi ya robo walishambuliwa ama kutishwa.
Na shuleni wanafunzi wawili kati ya watatu waliohojiwa walisema kuwa walificha kuwa wao ni wapenzi wa jinsia moja.
Kinachotia wasiwasi ni kuwa zaidi ya nusu yao hawako radhi kuripoti visa vya kushambuliwa kwa polisi kwa sababu wanaamini kuwa hakuna kitakachofanyika.
Wanasiasa na watunga sera mia tatu wanakutana Hague Uholanzi kujadili njia mpya za kuwalinda watu na kuhakikisha kuwa hawashambuliwi hata wakipendelea mapenzi ya jinsia moja.

Serikali yafuta kinyemela mtihani wa somo la Islamic


natoka Uk. 1
Afisa huyo akasemakuwa wao kama Bakwatawameshangaa na kushtukasana.Akasema kuwa pamojana kuwa hawakushirikishwawanakuja kupewa tu taarifa,lakini wanashangaa pia kwasababu hata walipopewataarifa na Kamishna waElimu, wameambiwa jambohilo liwe siri.Jambo hili linafanywa“SIRI, je Serikali inatakaWaislamu wasiambiwe?Kwanini? Kun                                                             agenda gani?Amehoji afisa huyo ambayehata hivyo hakutaka kutaja jina lake akisema kuwa yeyesio msemaji wa Bakwata.Awali taarifa juu ya kikaocha Wakristo na Wizara juu ya mitihani ya dini,zilianza kuvuja kupitia kwaWakristo waliohudhuriaambao walipokutana nawadau kutoka upande waWaislamu waliwalaumu nikwa nini hawakuhudhuriawakasaidiana kupinga uamuzihuo wa Serikali.Hata hivyo, wadau haokutoka Islamic EducationPanel waliwafahamishawadau hao wa Kikristo kuwa Ni rai yetu kwamba,madhali serikali imeonyeshania ya dhati katika kuletaumoja na upendo kwawananchi wake kidini, basifursa hiyo pia itumike kwakuwaacha Waislamu. Iachekurasimisha kuwa msemajiwa Waislamu ni Bakwata.Kama kuna jambo linahitajimawazo ya Waislamu, basimawazo yao hayawezikuwasilishwa na BAKWATA pekee. Lazima taasisi nyinginezinazowakilisha Waislamuzisikilizwe.Tunayasema hayatukizingatia kauli za baadhiya Wabunge hivi karibuniambao kauli zao zinaonyeshakuwa hueda Muislamu akiwanje ya Bakwata, anatafsiriwakama muhalifu au kavunjasheria za nchi.Lakini tunayasema haya pia tukizingatia kauli zawale waliosema kuwa hatuaya Serikali ya kuwadhibitiWaislamu chini ya Bakwata,na kwa namna moja aunyingine, kuingilia utendajiwa Baraza hilo, ikiwa ni pamoja na kuhusika katikakuweka viongozi wa ngaziza juu, ni ukandamizaji nakinyume cha sheria kwasababu haifanyi hivyo kwataasisi za dini nyingine.Wakataka Waislamuwaachwe.

Friday, May 17, 2013

HAYA NDO MAJINA YA WANAFUNZI WA CBE NA UDSM WALIONASWA WAKIJIUZA ( MAKAHABA)


Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi  stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.

Washitakiwa hao waliokamatwa  katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.

Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.

“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.

Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa  hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea.

Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni.

Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa.

“Msako huo ulifanyika Maisha   Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema

Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.

Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo.

Wapiganaji Boko Haram wauawa Nigeria


 18 Mei, 2013

Wanajeshi wa Nigeria

Takriban wapiganaji 30, wa waasi nchini Nigeria, wameuawa kwenye mashambulio ya anga yaliyofanywa na jeshi la serikali, Kaskazini Mashariki mwa nchini hiyo.
Msemaji wa jeshi la Nigeria, amesema, ndege za kivita na helicopta zilitumika kushambulia kambi kadhaa wa waasi hao.
Aidha ameiambia BBC kuwa ndege moja ilishambuliwa kwa kombora na waasi hao lakini ilifanikiwa kurejea salama hadi kambi yao.
Serikali ya Nigeria ilitangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ya Kaskazini Mashariki, yanayoshuhudia mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram.
Kwa sasa jeshi la Nigeria, linajaribu kutwaa uthibiti wa majimbo ya Adamawa, Yobe na Borno kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram.
Wakati huo huo, milipuko na milio ya risasi imesikika usiku kucka katika jimbo la Katsina.
Raia wameiambia BBC kuwa mabenki, vituo vya polisi na magerza yaliharibiwa kufuatia mapigano makali mjini Daura karibu na mpaka wa nchi hiyo na Niger.
Wanasema wameona miili ya wanajeshi watano na mitatu ya wapiganaji wa waasi lakini hakuna taarifa yoyote kuhusu idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa.
Mawasiliano ya simu ya mkononi yamekatizwa katika maeneo mengi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Lakini afisa mmoja wa serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa mitandao ya simu ilifungwa wakati wa operesheni hiyo ya kijeshi.