POLISI Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam imeendesha oparesheni maalum ya kuwanasa machangudoa wanaofanya biashara hiyo haramu katika eneo lao na kufanikiwa kuwaweka ‘mtu kati’ makahaba kibao, wakiwemo raia wa Rwanda na Burundi...
Kamatakamata
hiyo ilichukua nafasi usiku mnene wa Alhamisi ya Mei 23, mwaka huu
kwenye danguro kubwa la makahaba lililopo Kariakoo, jijini Dar ambalo
machangu hao hutegea mingo zao kwa ajili ya kuwanasa wateja.
Katika
hali iliyowashangaza polisi, midume iliyokutwa na makahaba hao ilitimua
mbio ili kujiokoa na mtego huo wa polisi uliodhamiria kusafisha eneo la
Kariakoo kwa ukahaba uliopitiliza.
Baadhi
ya wanaume wakati wakitimua mbio walisikika wakisema kuwa wakukamatwa
na kufikishwa kwenye vyombo vya dola ni wanawake hao kwa vile wanavaa
kimitego huku wakijua binadamu anapitiwa na shetani wakati wowote.
“Sisi
kosa letu nini? Wakamateni haohao machangudoa, watavaaje kimitego mbele
yetu sisi wanaume? Shetani naye atakuwa wapi wakati huo?” alisikika
akisema mmoja wa wanaume hao huku akichanganya miguu kupita kawaida.
Awali kabla ya zoezi la kuwanasa
makahaba hao halijaanza, afande mmoja alipowauliza wanachofanya hapo,
kahaba mmoja aliuliza: Una maswali mengi kwani we ni polisi?
Mei
24, mwaka huu, makahaba hao walipandishwa kwenye Mahakama ya Jiji na
kusomewa mashitaka yao na mwendesha mashitaka, John Kijumbe mbele ya
Hakimu Timoth Lyoni.
Waliosomewa
mashitaka ni Natasha Bahati, 30 (Mrundi), Asma Athuman, 23 (Mrundi),
Niyonkuru Evelinde, 29 (Mnyarwanda), Zaimana Hawa, 20 (Mrundi) na
Wabongo 35.
Wote walikana mashitaka lakini walipelekwa Gereza la Segerea, jijini Dar baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
No comments:
Post a Comment