62.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na
haki zote juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa
mamlaka hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya
ushirikiano na mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawa kwa ajili
ya ustawi ulio bora kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya
Muungano.
62.-(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii,
kila Mshirika wa Muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha
mahusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au
kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya
Mshirika wa Muungano.
62.-(3) Mshirika wa Muungano anaweza, wa kati wa kutekeleza majukumu
yake chini ya Ibara ndogo ya (2), kuomba mashirikiano kutoka Serikali ya
Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au
taasisi ya kimataifa au kikanda, na Serikali ya Jamhuri Muungano inaweza
kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itakavyohitajika. - Mamlaka ya Washirika wa MuunganoPata nakala kamili ya Rasimu ya Katiba mpya hapa: Rasimu
No comments:
Post a Comment