Tarehe 30 Mei, al-Shabaab waliagiza kuachiwa kwa wapiganaji wake sita, waliotuhumiwa kwa kupora dola 6,000 kutoka katika duka la dawa huko Baardheere na kuhukumiwa kukatwa mikono yao ya kuume.
"Nilikusanyika na kundi kubwa kutoka mjini kushuhudia adhabu ambayo ingetolewa kwa wapiganaji sita wa al-Shabaab, kwani tulitarajia mikono yao ya kuume kukatwa," alisema Yusra Nur Abdirahman, mwenye umri wa miaka 28 na mkaazi wa Baardheere. "Cha ajabu, mwakilishi kutoka katika kundi hili [aliyekuwa anahusika kutoa hukumu] Shekhe Aadan Nuh alitangaza kwa kutumia kipaaza sauti kwamba wajahidina hao sita wangepigwa viboko 39 kama adhabu ya kosa lao."
Alisema Nuh aliagiza dola 4,900 kurudishwa kwa mfamasia huyo, ambaye ni muungaji mkono al-Shabaab .
"Uamuzi huu wa aibu na wa kuchekesha ambao kwa hakika ulinishangaza na niliuchukulia kama uliokusudiwa kudanganya na kupotosha watu na kuhimiza wanachama wa kikundi hiki kupora mali binafsi na mali za familia," Abdirahman aliiambia Sabahi.
Huu ni mfano tu wa hivi karibuni wa jinsi adhabu za al-Shabaab zisivyo na msingi maalumu na za kinafiki, kwa kuwa wapiganaji walikutwa na hatia ya makosa hawapaswi kuumia na adhabu zilizoagizwa, alisema, akiongeza kwamba wapiganaji pia wameanzisha ulipizaji kisasi dhidi ya raia wa Somalia, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara au kuwakata vichwa ndugu wa viongozi kutoka Gedo na Hiran.
Abdirahman aliviomba vikosi vya serikali ya Somalia kukomesha vitendo vya kutisha vya al-Shabaab vya kuteka nyara, kuua, kutesa na kupiga.
Kukiuka sheria ya sharia
Huko Hiran, al-Shabaab imekuwa ikitoa amri ambazo hazina uhusiano na sharia hivyo wanachama wake wanaweza kuepukana na ujambazi na uasherati, alisema mkuu wa poilisi wa Hiran kanali Isaaq Ali Abdullahi.Majaji wa Al-Shabaab hawaelewi kikamilifu falsafa ya sheria ya kiislamu na kanuni za msingi za mfumo wa sheria wa haki na usiopendelea, alisema. Uamuzi wao sio halali kwa sababu unachochewa kisiasa, una kisasi na kuzingatia mfumo wa sheria wa kula njama, alisema.
Abdullahi aliishutumu al-Shabaab kwa kumkata kichwa mzee mwanaume na kijana wa kiume tarehe 22 Mei huko Dudumo Qaris, kilometa 45 kaskazini magharibi mwa Beledweyne. Wapiganaji pia waliiba dazeni za ngamia kutoka vijijini, alisema.
"Muda umefika kuwasaka hao wasaliti kutoka al-Shabaab, ambao wanahusiana na al-Qaeda, na kuwaondoa kutoka katika miji mbalimbali na vijiji katika mkoa ili kukomesha uonevu, ukandamizaji, ubaguzi na kudharau [raia]," Abdullahi aliiambia Sabahi.
"Tumefikia katika hali ambapo tunahitaji kutambua matamanio yetu, kwa sababu hivi karibuni utambuzi wa uhuru utakuwa kwetu, ambao watu wetu wanastahili kwa sababu ya kujitoa kwa kiasi kikubwa," alisema.
Ahmed Abdullahi Osman Inji, aliyekuwa kaimu mkuu wa usalama wa Hiran, alisema waathirika wawili walikuwa mjomba wake mwenye miaka 90, Hussein Aadan Toore, na mtoto wa kiume wa Toore. Wauaji waliwakata vichwa kwa kutumia jambia kali na kuwaacha kuvuja damu hadi kifo.
Muda wowote utakaochukua, al-Shabaab siku moja watapigwa na viongozi wao watatakiwa kwenda mbele ya mahakama ya kijeshi kujibu makosa ya gizani, alisema Inji.
"Ulipuaji wa mabomu na ukataji vichwa hauwezi kuendelea," alisema Inji. "Vikosi vya serikali vinachelewa kutekeleza operesheni zao za kijeshi kuzuia njia [za al-Shabaab] zisizo na heshima zinazosababisha maumivu na ugumu kuhusu watu wa Somalia, ambao walilazimishwa kumeza machungu ya mateso na kunyimwa maisha ya kisasa."
Majaaliwa ya Wasomali 6 waliotekwa nyara bado hayajulikani
Mahali walipo wananchi hao sita bado haijulikani kwa karibia wiki mbili baada ya wapiganaji washukiwa wa al-Shabaab waliwatorosha kutoka katika Gedo tarehe 23 Mei.Utekaji nyara ulifanyika kilometa 40 kati ya El Waq na Bu Sar, alisema mkuu wa wilaya wa El Waq Sahal Malim Ali. Mamlaka baadaye zilirejesha mabaki ya gari na pikipiki iliyoungua, ambayo wanamgambo watuhumiwa walitumia katika operesheni hiyo kabla ya kuungua na kuwaacha, alisema.
Ali alisema utawala wake bado unawasaka watekaji nyara.
Al-Shabaab hawajadaiwa kuhusika na utekaji nyara huo, lakini Ali alisema njia ya mashambulizi imekuwa ni mbinu ya hivi karibuni ya al-Shabaab, ambayo inatumia utoroshaji, ukataji vichwa, na utekaji nyara wa wananchi na mali binafsi kukabiliana na woga wa wakaazi wa maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa serikali ya Somalia.
Kuyumba kutokana na kushindwa kwa jeshi, al-Shabaab inajaribu kugawanya umaarufu kwa kuanzisha mapigano na machafuko ya kikabila dhidi ya serikali, alisema, akiongeza kwamba watu wa Somalia hawatakubali kutishiwa.
Hakuna sheria za sharia wala sheria za kimataifa zinazoruhusu utekaji nyara, alisema Ali. Katika migogoro, sheria za ushirikishwaji wa muda wa vita zitatumika kukamata maadui, lakini kuwashikilia raia kama mateka ni kinyume cha sheria na ni mbinu zisizokubalika kwa kushurutisha, alisema.
No comments:
Post a Comment