21 Mei, 2013 - Saa 12:29 GMT
Wachimba migodi kumi
wamejeruhiwa nchini Afrika Kusini baada ya walinzi kuwafyatulia risasi
za mipira wafanyakazi wa migodini. Taarifa hii ni kwa mujibu wa duru za
polisi.
Msemaji wa polisi Thulani Ngubane amesema kuwa wachimbaji migodi hao tayari wamepelekwa hospitalini.Uhusiano kati ya wafanyakazi na wamiliki wa migodi umedorora hasa baada ya polisi kuwaua wafanyakazi 34 wa migodini katika mgodi wa Marikana mwaka jana.
Wiki jana wafanyakazi katika kampuni ya Lonmin waligoma kwa siku mbili.
Wachimba mgodi wa Lanxess chrome, walifanya mgomo ambao haukuwa umepangwa baada ya kutofautiana na waajiri wao kuhusu marupurupu yao.
Inaarifiwa kuwa hali imetulia baada ya kufyatuliwa riusasi za mipira katika mgodi wa Rustenburg Kaskazini mwa Johannesburg, na kuwa hakuna yeyote miongoni mwa waliojeruhiwa yuko katika hali mbaya.
No comments:
Post a Comment