20 Mei, 2013
Polisi katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, wametumia moshi wa kutoza machozi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe.
Waandamanaji hao ni wa chama cha Waislamu wa
msimamo mkali, Ansar al-Sharia, ambao wakijaribu kufanya mkutano wa
hadhara uliopigwa marufuku.Jumatano chama tawala cha Waislamu wa msimamo wa wastani, Ennahda, kilisema mkutano mkuu wa Ansar al Sharia umepigwa marufuku kwa sababu kundi hilo halikupata kibali.
Lakini Ansar al Sharia iliahidi kusonga mbele na mkutano.
No comments:
Post a Comment