Watu wanaochochea mgawanyiko ndani ya al-Shabaab na wanaompinga
kiongozi wa kundi hilo, Ahmed Godane, lazima wauawe, alisema ulamaa na
muungaji mkono mkubwa wa al-Shabaab, Sheikh Hassan Hussein Aadan,
iliripoti Redio RBC ya Somalia siku ya Jumanne (tarehe 28 Mei).
"Nimesikia kuwa kuna migawanyiko ndani ya wapiganaji wa jihadi.
Anayetengeneza migawanyiko hiyo lazima auawe," alisema Aadan, ulamaa wa
Kenya mwenye asili ya Somalia anayeishi Nairobi. "Naamini mtu
anayejaribu kuzuia jihad lazima auawe."
Aadan amewahimiza watu kwenda mstari wa mbele na kujiunga na kile alichokiita "jihad" nchini Somalia.
Kauli ya Aadan imekuja baada ya kiongozi wa juu wa al-Shabaab, Hassan Dahir Aweys, kumkosoa vikali Godane
katika mahojiano yaliyorushwa tarehe 16 Mei na televisheni ya Somali
Channel, akimtuhumu kwa udikteta, kulitekaji nyara kundi hilo ili
kutanua himaya yake na kupuuzia maoni ya viongozi wengine wa al-Shabaab.
No comments:
Post a Comment