Baada ya kuwaomba wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao, Inspekta
Jenreali wa Polisi, David Kimaiyo, alitangaza siku ya Jumatatu (tarehe
27 Mei) kwamba vikosi vya usalama vitaanza kampeni ya kuwanyang'anya
silaha kwa nguvu, kiliripoti kituo cha Capital FM cha Kenya.
Wakaazi wa Mandera walitakiwa kusalimisha silaha zao kwa serikali mwezi huu au kunyang'anywa kwa nguvu. Hadi sasa polisi wamepokea silaha 12 tu, licha ya kuongezwa kwa muda wa mwisho.
"Tunachosisitiza ni kwamba wakaazi wote lazima wasalimishe silaha
zao. Sote tumekubaliana na viongozi kutoka maeneo haya kwamba
wakishindwa kufanya hivyo, tutawanyang'anya kwa lazima," alisema Kimaiyo
baada ya mkutano na viongozi kutoka Wajir, Mandera na Garissa. "Ili
maendeleo yapatikane kwenye maeneo haya, lazima usalama uwepo.
Tunawatolea wito wakaazi kutupa taarifa ambazo zinaweza kusaidia
kudhibiti uhalifu."
No comments:
Post a Comment