25 Mei, 2013
Viongozi wa Afrika wanasherehekea miaka 50 ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Nusu karne baadae, mengi bado hayakutimizwa.
Lakini kuna matumaini, hasa kwa sababu ya uchumi kukua sana katika bara hilo na hisia kuwa baadhi ya nchi kama Rwanda, Sierra Leone na hata Somalia zinaanza kuibuka kutoka ghasia na fujo.
Sherehe zilianza kwa wimbo wa AU.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, alikaribisha viongozi:
"Katika siku hii kubwa napenda kutoa hongera ya dhati kwa Wafrika wote katika bara letu.
Kutoka Cape hadi Cairo na kutoka Djibouti hadi Dakar pamoja na watu wote wenye asili ya Afrika wanaoishi ng'ambo.
Siku hii ya kihistoria inaashiria juhudi kubwa za bara zima la Afrika kuania uhuru, ukombozi na umoja, lakini piya ni mwanzo wa kutafuta uhuru wa kiuchumi na kijamii."
No comments:
Post a Comment