KUMRADHI KWA PICHA HIIKijana Ismai Mayoba(31)anaefanya kazi Bar ya Mangrove, mkaazi wa Jamhuri, Manispaa ya Lindi, akiwa katika ward namba 6 hospital ya Sokoine -Lindi baada ya kuchomwa moto na vibaka
Na Abdulaziz Lindi
Kijana
Ismai Mayoba (31) anaefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Jamhuri
Manispaa ya Lindi ambaye amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la
Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto amelazwa katika
Hospital ya Sokoine Mjini humo.
Kufuatia
tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mmoja
kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo
la Mtaa wa Congo.
Akithibitisha
kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndg Ally
Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na
atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa
kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie moto huku
akijua ni kosa kisheria.
Aidha
Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa
wengine 6 waliohusika na tukio hilo Taarifa zaidi tutawaletea kuhusiana
na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment