12 Mei, 2013 - Saa 09:44 GMT
Kiongozi wa chama cha Pakistan
cha Muslim League, Nawaz Sharif, amezungumza na wenzake chamani kuhusu
namna ya kuunda serikali yake mpya baada ya uchaguzi mkuu wa Jumamosi.
Bwana Sharif, ambaye amewahi kuwa waziri mkuu mara mbili kabla, alisema kuwa watu wameonesha wanaamini kuwa chama chake kinaweza kuleta mabadiliko.
Mcheza kriketi maarufu wa zamani, Imran Khan, ambaye huenda akawa kiongozi wa upinzani, aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi; lakini alisema taarifa za udanganyifu kwenye kura zinavunja moyo.
Chama tawala cha PPP inaelekea kuwa kimeshindwa vibaya.
No comments:
Post a Comment