23 Aprili, 2013 - Saa 10:13 GMT
Kwa mara ya kwanza kabisa Israel
imeituhumu Syria hadharani kuwa inatumia silaha za kemikali kupigana
dhidi ya waasi nchini humo.
Mkuu wa idara ya utafiti wa kijasusi nchini
Israel Brigadier Itai Baron ameliambia kongamano kuhusu usalama kwamba
silaha hizo zimetumika mara kadhaa , ikiwa ni pamoja na shambulizi
lililotekelezwa tarehe kumi na tisa mwezi uliopita wa Machi, ambalo
maafisa wa Syria walisema lilitekelezwa na wanamgambo.Amesema silaha hizo za kemikali huenda zinajumuisha sumu hatari ya Sarin.
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kutumika mrundiko wa silaha za kemikali zilizopo nchini humo katika mzozo uliopo nchini humo ambao unaingia katika mwaka wake wa tatu.
No comments:
Post a Comment