Ukuwaji wa uchumi katika bara la
Afrika unakwamishwa na migogoro ya umiliki wa ardhi kubwa ya kilimo.
Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na benki ya dunia.
Bara hilo ni makao kwa nusu ya ardhi ya kilimo duniani ingawa inakabiliwa na viwango vikubwa vya umaskini.Sheria za ardhi zinapaswa kuboreshwa barani Afrika ikiwa bara hilo litaweza kufanikiwa kutumia rasilimali zake vyema na kubuni nafasi za kazi.
Makamu wa rais wa benki hiyo barani Afrika , Makhtar Diop, amesema kuwa licha ya kuwa na ardhi kubwa na madini bado ni bara maskini zaidi.
Wanawake ni asilimia sabini ya wakulima Afrika ingawa wananyimwa ardhi kutokana na mila za kitamaduni.
''Hali halisi, haikubaliki na lazima ibadilike, ili waafrika wote wanufaike na ardhi zao,'' alisema bwana Diop.
Ripoti hiyo inapendekeza kuwa serikali ziweze kuhakikisha jamii na watu binafsi kumiliki ardhi na hata kutumia teknolojia mpya kuweza kufanya utafiti na uchunguzi wa umiliki wa ardhi.
Mwandishi wa BBC Mark Doyle, anasema kuwa migogoro ya kisheria kuhusu umiliki wa ardhi, ni kawaida barani Afrika.
"ni kawaida katika maeneo ya vijijini kuwa mashamba hugawanywa miongoni mwa familia, na kusababisha hali ya mvutano kuhusu nani anamiliki nini.''
Benki hiyo imesema kuwa huu ndio wakati mwafaka kuweka vizuri sheria ya umiliki wa radhi ili waafrika wafaidike zaidi na kupanda kwa bai ya bidhaa na kuimarisha uekezaji wa kigeni.
Kwa mujibu wa usimamizi mzuri wa ardhi, pia utazuia wizi na unyang'anyi wa mashamba
Katika miaka ya hivi karibuni, waekezaji kutoka nchi tajiri zaidi wamenunua mamilioni ya hekari za mashamba na wao hudai kuwa mashamba hayo hayana wamiliki.
No comments:
Post a Comment