Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi
wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,kamishna msaidizi wa polisi
kanda maalum ya Dar es Salaam DCP Ally Mlege,amesema katika hali ya
kushangaza baada ya kukamatwa kwa baadhi ya watuhumiwa waliokuwa
wakijihusisha na matukio ya ujambazi,hatimaye baada ya kubanwa na jeshi
la polisi walikubali na kusema kiwanda hicho kilichopo maeneo ya Kawe
Mzimuni kinatumika katika kutengeneza na kukarabati vifaa na silaha
mbalimbali zinazotumika katika matukio ya uporaji na unyang'anyi ambavyo
vilitumika na kusabisha mauaji mengi sehemu mbalimbali.
Aidha tapeli hatari bwana Mfaume Omary maarufu kwa jina la
Mau(29)mkazi wa Magomeni Kagera,ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa
la kutumia namba tofauti za mitandao ya simu na majina ya watu maarufu
ikiwemo viongozi wa serikali na viongozi wa dini kwa lengo la kujipatia
fedha kwa kuvaa uhusika wa mtu husika bila wanaombwa fedha hizo
kugundua.
Jeshi la polisi limekanusha vikali kuhusu habari zilizoripotiwa na
vyombo vya habari kuwa mbunge wa jimbo la Ubungo Mh John Mnyika amekoswa
na bomu na kumjeruhi moja ya wafuasi wake kuwa ni la huzushi,na ukweli
ni kwamba bomu hilo lililipuka ndani ya gari la polisi Pt .1902 wakati
askari dcp Julius alipokuwa ndani ya gari akisogeza box lenye mabomu ya
machozi na kwa bahati mbaya bomu hilo lililipuka ndani ya gari hilo
lakini halikuleta madhara kwa askari polisi yeyote wala raia waliokuwa
katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment