Polisi nchini Ghana wanawahoji
wazazi walioshtakiwa kwa kuwafungia nyumbani wanao walio kati ya umri wa
miaka minne na minane tangu kuzaliwa kwao.
Polisi walivamia makao yao yenye vyumba vinne
mjini Accra,siku ya Ijumaa na kuwaokoa watoto hao , mvulana mmoja na
wasichana wawili.Watoto hao sasa wamepelekwa katika makao ya kuwatunza watoto huku kukiwa na hofu kuwa wazazi wao huenda ni wagonjwa wa akili.
Mwandishi wa BBC mjini Accra anasema kuwa kisa hicho kimewashangaza sana watu mjini humo.
Inaarifiwa watoto hao walifungiwa nyumbani tangu kuzaliwa kwao na hawamkujua yeyote isipokuwa wazazi wao.
Aidha watoto hao waliishi katika chumba kimoja, huku Kondoo na kuku wakiwa katika vyumba viwili huku wazazi wao wakilala katika chumba chao kwenye nyumba hiyo iliyikuwa imejaa uvundo.
Nyumba ilionekana kama isiyoishi watu na licha ya kuwa haikuwa imesafishwa kwa miaka mingi, kuta zake zilikuwa na michoro.
Polisi walivamia nyumba hiyo baada ya jirani mmoja mwenye shauku kuwaarifu .
Wazazi wa watoto hao wanahojiwa na polisi pamoja na madaktari wa magonjwa ya kiakili mjini Accra, huku watoto hao wakipewa malezi na familia moja.
Msemaji wa polisi alisema kuwa wazazi wa watoto hao hawakuwahi kuruhusiwa kutoka nje ya nyumba yao.
Watoto waliwaarifu polisi kuwa baba yao ambaye hakuwa na ajira, aliwasomesha hesabu na kiingereza nyumbani kwao.
No comments:
Post a Comment