27 Mei, 2013
Baada ya sherehe za Jumamosi
mjini Addis Ababa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa
Afrika, viongozi wa Afrika sasa wanajadili baadhi ya matatizo
yanayokabili bara hilo.
Tena majadiliano yakahusu pendekezo la kuyafanya mahakama ya jinai ya kimataifa, ICC, yaache hatua za kumfikisha mahakamani rais mpya wa Kenya na makamo wake kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.
Wanabalozi wanasema viongozi wa Afrika wamegawika kuhusu swala hilo.
Mawaziri wa Mashauri ya Nchi za Nje walikubaliana Alkhamisi, kabla ya viongozi kukutana, kwamba AU iiombe ICC kupeleka jukumu la kesi za Rais Uhuru Kenyatta na makamo wake Wiliam Ruto kwa mahakama ya Kenya.
No comments:
Post a Comment