20 Mei, 2013
Waasi wa kundi la M23 Kaskazini
mwa Goma, Mashariki mwa DRC wamekuwa wakipigana na majeshi ya serikali
usiku wa kuamkia leo (jumatatu). Mapigano hayo yametokea katika eneo
ambalo waasi wameteka tangu Novemba mwaka jana.
Msemaji wa kundi hilo, amesema kuwa makabiliano
hayo yalifanyika umbali wa kilomita 12 Kaskazini mwa Goma, nalo jeshi la
serikali pia limeitikia kuwa makabliano yalitokea usiku wa kumakia leo
ingawa haijathibitishwa ikiwa kulikuwa na majeruhi.Mwandish wa BBC mjini Goma, Jonathan Kachelewa ameambia BBC , kuwa msemaji wa jeshi la serikali aliyeongea naye alisema waasi walianza kushambulia vituo vya jeshi katika eneo hilo, na kuwa mapigano yamekuwa yakiendelea tangu saa tisa usiku wa kuamkia leo.
Kulingana na Kachelewa, duru zinatofautiana kuhusu nani aliyeanza mapigano au nini chanzo cha mapigano yenyewe kwani waasi wanasema kuwa wao ndio walianza kushambuliwa
Pia yametokea huku kikosi cha kwanza cha wanajeshi wa UN kikitarajiwa kuwasili mwezi huu katika juhudi za kupambana na waasi hao.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, anatarajiwa kuzuru DRC Jumatano kama sehemu ya ziara yake ambapo atatembelea Goma , Kigali Rwanda na Entebbe Uganda.
Waasi hao waliuteka mji wa Goma, Novemba mwaka jana lakini wakaondoka siku kumi baadaye baada ya kuahidiwa mazungumzo na serikali ya DRC. Lakini tangu kuondoka wamekuwa wakiyateka baadhi ya maeneo karibu na mji huo
Waasi hao inadaiwa wanaungwa mkono na nchi jirani ikiwemo Rwanda na Uganda. Hata hivyo nchi hizo zimekanusha madai hayo.
No comments:
Post a Comment