Saturday, May 4, 2013

Kazi za uokozi zasimamishwa Darfur

 4 Mei, 2013 - Saa 13:53 GMT


Kazi za uokozi zilizokuwa zikifanywa Darfur, Sudan, kutafuta wafanyakazi 100 walionasa kwenye mgodi wa dhahabu ulioporomoka Jumatatu zimesimamishwa.
Darfur
Walioshuhudia tukio hilo wanasema msako katika mgodi wa Jebel Amir umesimamishwa kwa sababu ni hatari kuendelea na kazi za uokozi.
Hapo jana waokozi tisa piya walinasa kwenye mgodi huo.
Hakuna aliyenusurika.
Inaarifiwa kuwa migodi midogo-midogo ya Sudan ilitoa dhahabu ya thamani ya zaidi ya dola bilioni-mbili mwaka jana.
Madini hayo yanaipatia Sudan sarafu za kigeni ambazo zilipungua sana baada ya Sudan Kusini kujitenga mwaka wa 2011 na kubaki na visima vingi vya mafuta.

No comments:

Post a Comment