Tuesday, May 28, 2013

Je AU inahujumu mahakama ya ICC?

 28 Mei, 2013

Mwenyekiti wa tume ye Muungano wa Afrika Bi Nkosazana Dlamini Zuma
Baadhi ya Viongozi wa mataifa ya Afrika wanatarajiwa kupitisha azimio linaloitaka mahakama ya kimataifa ya jinai ICC kuruhusu kesi za washukiwa wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya kurejeshwa nchini humo
Azimio hilo linaitaka mahakama ya ICC kukubali kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Uhuru Kenyatta waliohusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007/08 zisikilizwe na mahama za nyumbani Kenya.
Viongozi hao wataitaka mahakama ya ICC kusitisha kesi hizo wakisema kuwa mahakama za Kenya zina uwezo wa kusikiliza kesi hizo.
Duru zinasema kuwa marais wa nchi za Afrika wataunga mkono azimio hilo, ambalo liliidhinishwa na mawaziri wa nchi za kigeni wa Afrika mjini Addis Ababa siku ya Ijumaa.
Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto, walichaguliwa katika uchaguzi wa Machi mwaka huu huku wakikabiliwa na kesi ya junai katika mahakama ya ICC.
Wanahusishwa na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 ambapo watu 1,100, waliuawa na maelfu kuachwa bila makao.
Hata hivyo pendekezo la mataifa ya Afrika haliwezi kuathiri kisheria kesi hiyo ikiwa litapitishwa , lakini bila shaka litampa ushawishi mkubwa Rais Kenyatta barani.
Itakuwa mara ya kwanza kwa azimio kama hilo kupitishwa dhidi ya mahakama ya ICC licha ya Uhuru Kenyatta kuwa rais wa pili kukabiliwa na kesi katika mahakama ya ICC. Wa kwanza ni Rais wa Sudan,Omar al-Bashir anayekabiliwa na kesi ya jinai.
Shirika la kimataifa la Amnesty International, limekosoa hatua hiyo, likisema inatia wasiwasi kwani inanuia kuwakwepesha mkono wa sheria washukiwa hao.

No comments:

Post a Comment