7 Mei, 2013 - Saa 11:24 GMT
Makachero wa FBI kutoka Marekani
wamewasili nchini Tanzania kusaidia katika upelelezi wa shambulizi la
bomu lililotekelezwa katika kanisa katoliki mjini Arusha siku ya
jumapili.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza akiwa mjini
Arusha anasema makachero hao wa FBI wako Tanzania kusaidiana na Jeshi la
wananchi wa Tanzania na Polisi kutafuta undani wa tukio hili ambalo
limeishtua na kuiweka serikali ya Tanzania katika wakati mgumu.Wakati huo huo wakuu wa serikali wakishirikiana na viongozi wa kidini wameandaa mkutano utakaojumuisha viongozi wapatao 200.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq amewaambia wanahabari kuwa wamelazimika kuandaa mkutano huo wa siku mbili kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete.
Mkutano huo utajadili uhusiano bora baina ya wakrito na waislamu.
No comments:
Post a Comment