29 Aprili, 2013 - Saa 07:33 GMT
Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika, amepelekwa mjini Paris Ufaransa kwa matibabu baada ya kupatwa na kiharusi.
Bwana Bouteflika, mwenye miaka 76, alipata tatizo la mshipa wake wa damu kuziba kwa muda, hali ambayo inasemekana kuwa kiharusi.Bwana Bouteflika anapokea matibabu katika hospitali ya kijeshi ya Val de Grace ambayo huwapokea wagonjwa mashuhuri kutoka ndani na nje ya Ufaransa.
Aidha daktari wake Rachid Bougherbal, alisema kuwa hali aliyokuwa nayo mgonjwa wake haikudumu kwa muda mrefu na inaweza kutibika. Aliongeza kuwa hali yake sio mbaya na anaendelea kupata nafuu.
Ripoti kuhusu Saratani
Waziri mkuu Abdelmalek Sellal alirejelea wito wake kwa wananchi kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu rais huyo.Bwana Bouteflika, ambaye kawaida huwa haonekani hadharani sana alifanyiwa upasuaji mjini Paris Miaka michache iliyopita.
Kulingana na taarifa ya madaktari ni kuwa alikuwa na vidonda vya tumbo , lakini taarifa iliyofichuliwa baadaye ilisemekana kuwa alikuwa na saratani ya tumbo.
Licha ya umri wake na hali yake duni ya kiafya, kunao wanaoamini kuwa bwana ,Bouteflika huenda akawania muhula wake wa nne wa urais katika uchaguzi utakaofanyika mwaka ujao.
Yeye ni mmoja wa viongozi wakongwe ambao wamekuwa wakiongoza Algeria, tangu nchi hiyo kujipatia uhuru miaka hamsini iliyopita.
No comments:
Post a Comment