22 Aprili, 2013 - Saa 09:34 GMT
Ripoti za awali zilionya kuwa Dzhokhar Tsarnaev, ambaye ana majeraha ya risasi kwenye shingo lake, huenda asitoe ushahidi kwa kuongea na majasusi hao.
Wakati huohuo, viongozi wa mashtaka wanaanda kesi dhidi ya mshukiwa wa pili wa mashambulizi ya Boston Marathon Dzhokhar Tsarnaev huku maelezo zaidi kuhusu kukamatwa kwake yakijitokeza.
Ikiwa atashtakiwa kwa kutumia silaha za maangamizi kwa lengo la kuwaua watu, huenda akakabiliwa na hukumu ya kifo.
Tsarnaev yuko hospitalini akiwa hawezi kuongea kwa sababu ya jeraha katika shingo lake.
Serikali imesema kuwa majasusi hao watamhoji mshukiwa bila ya kumweleza haki zake ambazo zinamruhusu akae kimya hadi atakaposhauriana na wakili wake. Hata hivyo majasusi walikanusha ripoti kuwa walimhoji.
Awali meya wa Boston, Tom Menino, alisema kuwa hawana uhakika ikiwa wataweza kumhoji mshukiwa"Tuna maswali mengi na yote yanahitaji kujibiwa," alisema gavana wa Massachusetts Deval Patrick,akinukuliwa na shirika la habari la Reuters.
Mshukiwa alikamatwa jioni Ijumaa baada ya msako mkali dhidi yake wakati ambapo nduguye mkubwa na mshukiwa mwingine waliuawa.
Polisi wanaamini kuwa Dzhokhar huenda alimuua nduguye mwenyewe kwa kumgonga na gari alipokuwa anatoroka polisi Alhamisi usiku.
Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya kijana mmoja mwenye umri wa miaka minane na wanawake wawili na kisha kuwajeruhi wengine wengi ikikisiwa kuwa walikuwa zaidi ya 180.
No comments:
Post a Comment