Tuesday, April 30, 2013

Al-Amriki na wapiganaji wa kigeni katika mapambano na kiongozi wa al-Shabaab .

Idadi ya matukio katika siku za karibuni yameonyesha wazi kuongezeka kwa mapambano baina ya makundi mbalimbali ndani ya al-Shabaab, na kiasi cha kuwa siku za usoni kikundi washirika wa al-Qaeda kitakabiliwa na mgogoro na kumomonyoka.
    Mpiganaji jihadi mzaliwa wa Marekani Omar Hammami alituma picha inayoonyesha damu kooni mwake kupitia akaunti yake ya Twitter hapo tarehe 25 Aprili baada ya wanausalama wa al-Shabaab kudaiwa kujaribu kumuua.  [Jalada] Sheikh Mukhtar Robow Ali (katikati), anayejulikana pia kama Abu Mansur, ni kiongozi wa juu wa al-Shabaab ambaye yuko katika msuguano na kamanda wa kikundi Ahmed Abdi Godane. Juu, Robow akisindikizwa na walinzi mjini Mogadishu mwaka 2008. [Na Mokhtar Mohamed/AFP]
  •  
  • Mpiganaji jihadi mzaliwa wa Marekani Omar Hammami alituma picha inayoonyesha damu kooni mwake kupitia akaunti yake ya Twitter hapo tarehe 25 Aprili baada ya wanausalama wa al-Shabaab kudaiwa kujaribu kumuua. [Jalada]
  •  
  • Sheikh Mukhtar Robow Ali (katikati), anayejulikana pia kama Abu Mansur, ni kiongozi wa juu wa al-Shabaab ambaye yuko katika msuguano na kamanda wa kikundi Ahmed Abdi Godane. Juu, Robow akisindikizwa na walinzi mjini Mogadishu mwaka 2008. [Na Mokhtar Mohamed/AFP]
Siku ya Jumatatu jioni (tarehe 29 Aprili), mpiganaji jihadi mzaliwa wa Marekani Omar Hammami, anayejulikana pia kama Abu Mansour al-Amriki, alionekana kuandika bandiko lake la mwisho katika mkasa uliodumu mwaka mmoja sasa ambao umemsibu yeye na wapiganaji wenzake wa kigeni dhidi ya kamanda wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, anayejulikana pia kama Mukhtar Abu Zubayr.
Katika mfululizo wa mabandiko ya kuchanganyikiwa siku ya Jumatatu jioni, al-Amriki, akitumia akaunti ya Twitter handle @abumamerican, aliuaga ulimwengu kama mpiganaji wa al-Shabaab mwaminifu kwa Gadane kwa madai kuwa amekusudia kumuua yeye na wafuasi wake.
"Pengine nisipate fursa nyingine ya kuandika lakini kumbukeni tulichokisema na kile tulichosimamia. Mungu aliniweka hai ili kutoa ujumbe kwa umma," alisema.
Hata hvyo, siku ya Jumanne (tarehe 30 Aprili), al-Amriki alianza kutuma idadi kubwa ya ujumbe mpya kuhusu maendeleo ya hali yake, na kutaja kutolewa kiungo cha fatwa inayodaiwa kuandikwa na kuungwa mkono na makamanda watatu wakubwa wa al-Shabaab wanaopingana na Godane -- Ibrahim al-Afghani (ambaye jina lake halisi ni Ibrahim Haji Jama Meeaad na ambaye pia anajulikana kama Abu Bakr al-Zaylai), Sheikh Mukhtar Robow Ali (au Abu Mansur) na al-Zubayr al-Mujahid -- pamoja na kiongozi wa Hizbul Islam Sheikh Hassan Dahir Aweys.
Fatwa ilimweleza al-Amriki na wafuasi wake kama "ndugu" ambao damu yao haikuruhusiwa kumwagika "hata kama [Godane] ataamrisha hivyo".
Iliendelea kuonya dhidi ya "utiifu wa upofu" kwa Godane, na kuelezea majaribio dhidi ya maisha ya al-Amriki na wafuasi wake kama "uzembe unaosababishwa na ujinga wa hali ya juu, au matokeo ya kufanya hila kwa dhana za kisheria kwa ajili ya masilahi ya kisiasa na kupata malengo binafsi ambayo hayahusiani chochote na sheria ya Mungu".

Jaribio la mwisho kwa maisha ya al-Amriki

Alhamisi iliyopita jioni (tarehe 25 Aprili), wakati akiwa amekaa kwenye duka la chai, wanausalama kadhaa wa al-Shabaab walidaiwa kujaribu kumuua al-Amriki, lakini wakashindwa. Masaa kadhaa kupita, al-Amriki alisema alipokea neno kutoka kwa kikosi cha al-Shabaab kwamba walikuwa wameizunguka nyumba yake.
"Abu Zubayr ameshakuwa mwendawazimu, anaanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe," al-Amriki alisema.
Baada ya kuwa kimya kwa siku kadhaa, al-Amriki alirejea kwenye Twitter kusema kwamba alikuwa anaishi anaandaa kinachoweza kuwa pambano lake la mwisho ndani ya al-Shabaab. Kutoka katika Tweets yake, inaonyesha kwamba al-Amriki na wafuasi wake sasa wanakimbia baada ya majadiliano yaliyoshinda na wapiganaji wa Godane.
"Tuliomba iwepo sharia na kukubali mambo mengi ya kuleta amani lakini wanasema sisi ni kikundi cha wasaliti hata kama [Godane] ni kiongozi wetu na hatutapigana," alielezea.
"Ni hatima ya […] mapambano yaliyokamilika dhidi ya wale wanaosema ukweli," al-Amriki aliandika, "Hata kama tutakufa, tumeshinda".

Vikundi vya al-Shabaab vyawindana

"Jaribio la mauaji ya al-Amriki toka kwa Godane ni ishara ya wazi kwamba mpasuko baina ya kiongozi wa al-Shabaab na wapiganaji wa kigeni umekuwa vita vya moja kwa moja," alisema Omar Ali Roble, aliyekuwa waziri wa upunguzaji silaha na kuwaunganisha na jamii wanamgambo wa Somalia.
"Wanawindana wao kwa wao, jambo ambalo ni ushahidi wa wazi kuwa al-Shabaab hakukuwa kikundi cha dini au jihadi, bali kikundi cha wahalifu kilichojikusanya kuua umma wa Somalia chini ya kisingizio cha dini," aliiambia Sabahi.
Kumaliza upinzani sio kitu kipya kwa Godane, kwa vile anajulikana kufanya vitendo kama hivyo dhidi ya wanachama wa kikundi au washirika wao wanaompinga, Roble alisema.
Kile kinachoonekana zaidi, Godane ameunganishwa na kifo cha Fazul Abdullah Mohammed, kiongozi wa al-Qaeda katika Afrika ya Mashariki, ambaye aliuliwa mwezi Juni 2011 wakati msafara wake uliokuwa unaongozwa na wapiganaji wa al-Shabaab, inadaiwa kwa maagizo ya Godane, ulikwenda moja kwa moja katika kituo cha upekuzi wa usalama cha Umoja wa Afrika mjini Mogadishu.
Wapiganaji wa kigeni wa al-Qaeda wenye uhusiano na viongozi wa al-Shabaab ambao wanasimama kumpinga Godane, kama vile Robow, wanawakilisha hatari kwa kamanda wa juu wa kikundi, Roble alisema. "Ndo sababu [Godane] anaanzisha mkakati wa 'kugawa na kutawala', kwa kuwaondosha viongozi wa kigeni [wa al-Shabaab] wanaopingana na mawazo yake."

Barua za wazi zatingisha misingi ya al-Shabaab

Wakati mgogoro baina ya wapiganaji wa kigeni na wanachama wa al-Shabaab watiifu kwa Godane wanajitokeza, idadi ya barua za wazi zinazopelekwa kwa utawala wa Godane zimeanza kumomonyoa kikundi kutoka ndani.
Barua ya kukosoa iliyopelekwa kwa Godane kutoka kwa al-Zubayr al-Muhajir, anayedai kuwa mmoja wa wapiganaji wa juu wa al-Shabaab, ilitumwa kwa idadi kubwa ya tovuti za wanajihadi tarehe 20 Aprili, kuonyesha kuzidi kwa kutoaminiana na kukatika kwa mawasiliano baina ya vikundi tofauti ndani ya washirika wafuasi wa al-Qaeda.
Barua ya al-Muhajir ilikuja si zaidi ya wiki mbili baada ya kamanda wa pili kwa cheo, Ibrahim al-Afghani, kutoa barua ya wazi hapo tarehe 6 Aprili Ayman al-Zawahiri, ambamo alitosa ukosaji mkubwa wa wazi kwa Godane.
Barua ya al-Afghani ilifuatiwa na nyingine iliandikwa na al-Amriki, ambaye alikuwa wa kwanza kuonyesha tatizo ya uongozi wa ndani wa al-Shabaab, kutowaamini wageni na kutokuaminiwa kwa wageni katika suala la jihadi.
Hassan Abdullahi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa ambaye anafuatilia masuala ya harakati za Kiislamu nchini Somalia, alisema barua hizo ni ishara ya mgawanyo mkubwa miongoni mwa uongozi wa kikundi hicho.
"Kwa hakika, kuna mtanziko mkubwa miongoni mwa uongozi wa kikundi hiki, Wasomali na wageni pia, na imekuwa wazi kwamba tofauti haziko tu baina ya Godane na Abu Mansur lakini pia zinajumuisha viongozi wengine wa kundi hili," Abdullahi aliiambia Sabahi.
"Wapiganaji wa nje katika kikundi hiki kwa sasa wanajua kuwa wanapuuzwa na kutengwa katika nafasi za ngazi ya juu na kwamba wako chini katika nafasi za uongozi, kwa hiyo wanatafuta kuondoka kwa usalama," alisema.
"Baada ya kuanguka kwa al-Shabaab kisiasa, kijeshi na kifedha, viongozi wa kikundi hiki wameanza kutuhumiana kuhusu nani anayehusika na kuanguka huko," Abdullahi alisema. "Isingekuwa kukuzwa katika kusema kwamba kikundi hiki kwa sasa kimeingia katika hatua nyingine ya kumomonyoka."

Kushindwa zaidi

Abdikadir Ahmed Gardiyow, ofisa usalama mstaafu wa Somalia, alitabiri hata kutoridhika zaidi ndani ya vyeo vya al-Shabaab.
"Mgogoro wa ndani katika al-Shabaab ni wa kina sana na sasa unafikia mgawanyiko na tofauti ya mawazo. Umefikia hatua ya mapigano ya moja kwa moja, mgogoro wa ndani kwa ndani na kufutwa," Gardiyow aliiambia Sabahi.
"Katika miaka kadhaa iliyopita, al-Shabaab ilijaribu kujionyesha yenyewe kwa mataifa ya nje kama ni chama chenye nguvu ambacho wanachama wake wanapigana kwa sababu moja. Hata hivyo, matukio ya hivi karibuni ya ndani na mgogoro unaoendelea miongoni mwa viongozi wake yametoa picha tofauti," alisema. "Ujumbe mbalimbali na malalamiko yanayotokea yatakuwa kali zaidi na hili litaathiri sana jitihada za kikundi za kuajiri wapiganaji wapya wa kigeni."
Hussein Mohamed, mchambuzi wa masuala ya kisiasa anayeishi Mogadishu, alitabiri kwamba matukio haya yatasababisha kutofautiana ndani ya vyeo vya al-Shabaab na kwamba kikundi kilichojitenga kingeweza kujitokeza katika siku zijazo.
"Kama mgogoro huu wa ndani katika al-Shabaab utaendelea, kikundi kilichojitenga kitajitokeza mara moja. kuna uwezekano kwamba kundi la kwanza kama hilo lililojitenga litamuunga mkono Abu Mansoor al-Amriki," aliiambia Sabahi. "Katika tukio ambapo tawi linatawaliwa na wapiganaji wa kigeni ndani ya al-Shabaab linaweza kuvunjika, hili litadhoofisha zaidi harakati na linaweza kusababisha kusambaratika kwake kwa jumla."

No comments:

Post a Comment