Tuesday, June 4, 2013

Kesi dhidi ya Ruto kusikilizwa Septemba


William Ruto ni mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya
Mahakama ya kimataifa ya ICC, imetangaza kuwa kesi zinazowakabili washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya, naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang zitasikilizwa mwezi Septemba.
Mahakama hiyo pia imependekeza baadhi ya vikao vya kesi hiyo kufanyika Tanzania au Kenya.
Ruto anakanusha kuwahi kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007 nchini Kenya, sawa na Rais Uhuru Kenyatta.
Mahakama ya ICC pia imesema kuwa ushahidi uliotolewa dhidi ya aliyekuwa rais wa Ivory Coast , Laurent Gbagbo, hautoshi kuhimili kesi dhidi ya mshukiwa.
Matangazo hayo mawili, yanakuja baada ya wiki kadhaa za shinikizo kutoka kwa nchi kadhaa za Afrika kuwa mahakama hiyo itupilie mbali kesi hizo dhidi ya Kenyatta na Naibu wake.
Mataifa ya Muungano wa Afrika yalisema kuwa mahakama ya ICC ina ubaguzi wa rangi kwa kuwa inawawajibisha viongozi wa Afrika pekee , madai ambayo yamekanushwa na kiongozi mkuu wa mashtaka Fatou Bensauda.
Daima Fatou Bensouda amekuwa akisisitiza kuwa washukiwa ghasia za Kenya lazima wawepo katika mahama hiyo wakti kesi zao zikisikilizwa.Lakini majaji wameamua kuwa haki huenda ikatendeka zaidi ikiwa wataruhusu kesi za washukiwa wawili hao kusikilizwa Kenya au Tanzania.
Upande wa utetezi pia huenda ukalazimika kutoa ombi hilo kwa niaba ya mshukiwa Uhuru Kenyatta.
Lakini pigo kubwa zaidi kwa kiongozi wa mashtaka ni ambavyo umeshughulikia ushahidi dhidi ya Laurent Gbagbo,kwani mahakama inasema hautoshi kuweza kuhimili kesi.
Mahakama inataka hilo kurekebishwa kabla ya kusikiliza tena kesi hiyo mwezi Novemba. Gbagbo amekaa ICC sasa kwa miaka miwili huku kesi yake ikiwa bado haijasikilizwa.
Moja ya sababu ya kuundwa kwa mahakama ya ICC ni kuonyesha kuwa hakuna ambaye anaweza kuhujumu sheria bila kuwajibishwa.
Kwa sasa jukumu kubwa la viongozi wa mashtaka ni kuonyesha ushahidi wa kutosha utakaoweza kuwashawishi majaji kuwa bwana Gbagbo ana kesi ya kujibu.
Kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Ujao.

Kesi dhidi ya Pistorius yaakhirishwa



Pistorius anakana kumuua mpenzi wake Reeva kwa maksudi nyumbani kwake
Kesi inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius Imeakhirishwa na mahakama hadi tarehe 19 mwezi Agosti.
Pistorius, alirejea mahakamani hii leo baada ya kupewa dhamana wakati kesi yake iliposikilizwa mara ya kwanza mapema mwaka huu.
Oscar anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi Februari.
Anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake kwa maksudi akisema alikosea kwa kudhani kuwa alikuwa jambazi kavamia nyumba yake.
Viongozi wa mashtaka wameomba muda zaidi kuweza kukusanya ushahidi dhidi ya mwanariadha huyo aliyeshiriki michezo ya Olimpiki mjini London.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa ushahidi mwingi katika kesi hiyo utatokana na uchunguzi wa kisayansi unaofanywa ndani ya bafu ambamo Reeva Steenkamp aliuawa.
Kesi hiyo kwa upana wake huenda isianze kusikilizwa hadi mwaka ujao.
Mwanariadha huiyo alichiliwa kwa dhamana na amekuwa akiishi katika nyumba ya jamaa wake mjini Pretoria

Uzinduzi Wa Rasimu Ya Katiba Mpya Ya Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionesha Rasimu ya Katiba mpya ya Tanzania
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akionesha Rasimu ya Katiba mpya ya Tanzania.
62.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na haki zote juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa mamlaka hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya ushirikiano na mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawa kwa ajili ya ustawi ulio bora kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akipokea nakala ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Jaji Mstaafu Joseph Warioba akishuhudia
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akipokea nakala ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Jaji Mstaafu Joseph Warioba akishuhudia.
62.-(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii, kila Mshirika wa Muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha mahusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Mshirika wa Muungano.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd  akipokea nakala ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda akishuhudia  akishuhudia
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd akipokea nakala ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda akishuhudia akishuhudia.
62.-(3) Mshirika wa Muungano anaweza, wa kati wa kutekeleza majukumu yake chini ya Ibara ndogo ya (2), kuomba mashirikiano kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ajili ya kufanikisha mahusiano na jumuiya au taasisi ya kimataifa au kikanda, na Serikali ya Jamhuri Muungano inaweza kutoa ushirikiano kwa mshirika huyo kwa namna itakavyohitajika. - Mamlaka ya Washirika wa Muungano
Pata nakala kamili ya Rasimu ya Katiba mpya hapa: Rasimu

Monday, June 3, 2013

Gaddafi alificha mali Afrika Kusini piya



Wizara ya fedha ya Afrika Kusini inachunguza tuhuma kwamba mali ya thamani ya kama dola bilioni moja ya Libya ilifichwa nchini humo.
Rais Zuma na Gaddafi mwezi May mwaka 2011 walipokutana Tripoli, Libya
Wakuu wa Libya wamedai kuna dhahabu, almasi na fedha taslim ambazo kiongozi wa zamani wa Libya, Kanali Gaddafi na familia yake, waliziweka Afrika Kusini.
Serikali ya Libya imekuwa ikijaribu kuzipata mali za Kanali Gaddafi katika sehemu mbali-mbali za dunia tangu alipofariki mwaka 2011.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema watu wengine wamekisia kuwa mali ya hayati Gaddafi ilioko nchi za nje inaweza kufika dola bilioni 80.

Mapendekezo ya wagombea huru TZ


Mkuu wa tume ya marekebisho ya katiba Tanzania
Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini Tanzania, imependekeza wawepo wagombea huru katika ngazi za uchaguzi mbalimbali nchini humo. Hayo ni miongoni mwa mapendekezo yaliyotangazwa jijini Dar es salaam na Mwenyeketi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Kwanza ya Katiba Mpya.
Jaji Warioba amesema pia wapo wananchi waliopendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe kugombea nafasi zote isipokuwa nafasi ya urais. Jaji Warioba amesema tume ilipitia maoni hayo na kupendekeza kwamba, wagombea huru waruhusiwe kugombea nafasi zote kuanzia ngazi ya Mwenyekiti wa Mtaa hadi nafasi ya Urais.
Kadhalika Jaji Warioba amesema, Tume pia imependekeza kwamba, mgombea yeyote wa urais ili athibitike kuwa ni mshindi atalazimika kupata zaidi ya asilimia hamsini ya kura, na kwamba endapo mgombea hatafanikiwa kupata asilimia hamsini uchaguzi utarudiwa kwa kuangalia wagombea wawili waliopata kura nyingi.
Mapendekezo mengine yaliyotangazwa na Tume ni pamoja na kuwepo kwa serikali tatu yaani ya Bara,Zanzibar na ile ya Shirikisho.
Pia tume imependekeza kuwa, Bunge la Muungano liwe na jumla ya Wabunge 75, hamsini kutoka Bara, ishirini kutoka visiwani na watano wateuliwe na Rais kutoka makundi maalum ya walemavu.
Mapendekezo mengine ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni pamoja na Rais kubakia na madaraka yake ya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu, lakini uteuzi wa ngazi za chini uachiwe Tume ya Utumishi.
Imeeleza kwamba, Rais mara baada ya kufanya uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu wakiwemo, mawaziri, manaibu waziri, jaji mkuu na naibu jaji mkuu, viongozi hao watalazimika kuthibitishwa na Bunge.

Familia ya Pistorius yashtushwa na picha


Pistorius atafikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana
Familia ya mwanariadha mlemavu nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius, wameshstushwa na picha zilizofichuliwa za bafu alimomuulia mpenzi wake mnamo mwezi Februari.
Shirika la habari la Uingereza la Sky, mnamo Ijumaa, lilionyesha picha za kuogofya zinazoshukiwa kuwa za bafu ambalo mpenzi wa Pistorius Reeva Steenkamp, aliuawa.
Polisi walisema kuwa wamechukizwa mno na kufichuliwa kwa picha hizo.
Bwana Pistorius mwenyewe anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake, kupitia mlango wa bafu alimokuwa , alisema alidhani kuwa alikuwa mwizi aliyevamia nyumba yake.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa hatua ya mahakama mwanzo kutathmini kesi siku yake Jumanne.
Pistorius ni mwanariadha mlevamu asiye na miguu yake miwili ingawa hukimbia kwa miguu bandia au vyuma. Alishiriki michezo ya Olimpiki mjini London mwaka jana.
''Familia ya Pistorius ilimuunga mkono alipokuwa anajiandaa kufikishwa mahakamani , alisema mjomba wake,'' Arnold Pistorius.
''Tunaamini maneno yake , tunampenda na tutamuunga mkono kwa kila hatua ya kesi hii,''alisema Mjombake Pistorius.
"tumeshtushwa na picha hizi za ajali iliyotokea nyumbani kwa Oscar."
Msemaji wa polisi ameelezea kuwa polisi wanachunguza nani aliyefichua picha hizo .
''Kitendo hiki hakikuhitajika na kimetuudhi kweli. Hatujui picha hizi zimetoka wapi,'' alisema polisi huyo.
Pistorius atafikishwa mahakamani Jumanne kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana, kufuatia kukamatwa kwake, kuhusu mauaji ya Steenkamp.
Kesi hiyo inatarajiwa kuakhirishwa kwani uchunguzi wa polisi ungali unaendelea.
Pistorius ameajiri baadhi ya mawaklili shupavu nchini Afrika Kusini kumtetea.
Anasema kuwa alimpiga risasi Bi Steenkamp kupitia mlango wa choo kimakosa baada ya kudhani kimakosa alikuwa mwizi.
Hata hivyo, viongozi wa mashtaka wanasema kuwa alimuua kwa maksudi baada ya wawili hao kugombana.

Mamlaka ya Zanzibar Kwanza

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wananchi waliofurika katika viwanja vya kibanda maiti kusherehea “Umoja na mshikamano wa Wazanzibari”
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wananchi waliofurika katika viwanja vya kibanda maiti kusherehea “Umoja na mshikamano wa Wazanzibari”
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameunga mkono kauli iliyotolewa na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Eddi Riyami ya kuwataka Wazanzibari wasiotaka mamlaka kamili ya Zanzibar wajitokeze hadharani kama wanavyofanya wale wanaodai mamlaka kamili ya Zanzibar.
Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF ameeleza hayo katika viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar katika mkutano wa hadhara uliolenga kusherehekea “Umoja wa Wazanzibari” ulioasisiwa kufuatia maridhiano ya kisiasa.
Wananchi waliofurika katika viwanja vya kibanda maiti wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Wananchi waliofurika katika viwanja vya kibanda maiti wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Amesema hatua ya Wazanzibari kudai mamlaka ni haki yao, na kwamba hakuna dhambi ya kudai jambo hilo.
Amefahamisha kuwa wazanzibari walio wengi wameungana kudai mamlaka ya nchi yao kwa njia ya amani na demokrasia, na kutoa wito kwa wale wasiotaka mamlaka ya Zanzibar wajitokeze hadharani.
Wananchi waliofurika katika viwanja vya kibanda maiti wakinyosha mikono na kucheza wakati wakisherehekea hotoba ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Wananchi waliofurika katika viwanja vya kibanda maiti wakinyosha mikono na kucheza wakati wakisherehekea hotoba ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.
Amewahakikishia wananchi kuwa hatorudi nyuma katika kuitetea Zanzibar kuwa na mamlaka yake, ili iweze kutambulika kimataifa na kuweza kuratibu na kushughulikia mambo yake ya nje.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Eddi Riyami,  akitoa salamu za Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hassan Nassor Moyo katika viwanja vya kibanda maiti mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Eddi Riyami, akitoa salamu za Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hassan Nassor Moyo katika viwanja vya kibanda maiti mjini Zanzibar.
Kwa upande wake Katibu wa kamati ya maridhiano Ismail Jussa Ladhu, amewaomba viongozi wa vyama vyote kushirikiana na wananchi  katika kudai mamlaka ya nchi, ili wazanzibari waweze kujikomboa kutokana na kile alichokiita ukoloni wa Tanganyika.
Katibu wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Ismail Jussa Ladhu akizungumza na wananchi katika viwanja vya Kibanda maiti.
Katibu wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar Ismail Jussa Ladhu akizungumza na wananchi katika viwanja vya Kibanda maiti.
Katika risala ya wananchi wa mikoa mitano ya Zanzibar iliyosomwa na Ameir bin Ameir kutoka Bwejuu, amesema pamoja na mambo mengine, katiba mpya izingatie uwepo wa Jamhuri ya Zanzibar na uraia wake.
Mambo mengine waliyotaka yatolewe katika orodha ya mambo ya Muungano ni pamoja na sarafu, benki kuu, mambo ya nje, vyama vya siasa, baraza la mitihani pamoja na mafuta na gesi.