Serikali ya Kenya inapanga kufufua askari wa akiba wa Kenya (KPR),
programu ya kutoa mafunzo na kuwezesha vikosi vya raia, kusaidia
kupambana na wanamgambo wa al-Shabaab kutoka ndani ya jamii huko
Garissa.
Garissa imekuwa mahali
pa mashambulio makubwa ya al-Shabaab nchini Kenya baada ya vikosi vya ulinzi vya Kenya kupeleka vikosi Somalia Oktoba 2011.
Iliongozwa na Inspekta Jenarali David Kimaiyo na Katibu Mkuu wa
Usalama wa Ndani Mutea Iringo, Kamati ya Ushauri ya Taifa imekuwa
ikichunguza mfululizo wa mashambulio kama hayo mwezi Aprili. Wakati wa
mkutano wa tarehe 20 Aprili,
kamati ilipendekeza kushirikisha raia katika mji wa Garissa kwa ajili ya operesheni za kigaidi.
KPR iliundwa mwaka 1948 kusaidia polisi kudumisha sheria na kanuni nchini Kenya kote.
Mwaka 2004, aliyekuwa kamishina wa polisi Meja Jenerali Mohammed
Hussein Ali alivunja na kunyang'anya silaha KPR katika maeneo ya miji ya
Kenya baada ya maofisa wake kuhusishwa na uhalifu wa kutumia nguvu na
rushwa. Hata hivyo, aliendeleza jeshi hilo katika maeneo ya vijijini,
kupambana na wizi wa ng'ombe na ujambazi.
Kufufua askari wa akiba wa Kenya
Raia katika KPR iliyofufuliwa watasaidia kulinda usalama katika
vitongoji vya Garissa, Kamishina wa wilaya ya Garissa Maalim Mohammed
aliiambia Sabahi. Watakuwa chini ya maofisa wanaosimamia askari kanzu
wasio na sare wenye jukumu la kufichua shughuli za al-Shabaab zisizo na
ujuzi kutoka katika maficho yao na kuzuia mashambulio ya kigaidi.
Kutoka vikosi vya raia vilipopewa silaha, Mohammed alisema serikali
imekuwa ikichukua hatua kali kuepuka kutoa silaha kwa makosa kwa
wahalifu.
"Tunapaswa kupata vitu mara tu tunapoanza ili tusiongeze silaha zaidi
katika mzunguko, ambazo zitaongeza matatizo zaidi kwenye vitisho
vilivyopo vya al-Shabaab," alisema.
"Kuna hitilafu kwenye kutoa silaha kwa raia, lakini kwa kunyoosha
mambo kwa ufanisi na kuhakikisha kwamba silaha hazitolewi kwa
wasiostahili, tunachagua watahiniwa kufanyiwa uchunguzi," Mohammed
alisema.
Tunawaandikisha askari wale wanaofaulu uchunguzi wa awali ambao
watapewa kozi ya mwezi mmoja kuhusu silaha za moto, mafunzo halisi,
ukusanyaji wa taarifa kuhusu maadui na kukabili majanga ya msingi,
alisema. Serikali kwa sasa inahakiki watahiniwa 100 kwa ajili ya kupewa
nafasi katika kikosi cha maofisa wa akiba, ikiwa ni pamoja na
wafanyabiashara, wanawake na vijana.
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa mkoa wa Kaskazini Mashariki Charlton
Mureithi, viunga kumi ambavyo vilibainishwa kama vilikuwa vikiwahifadhi
al-Shabaab vitakuwa na askari kumi wa akiba kila moja.
"Baada ya mafunzo yao maalumu, wataeneza katika viunga vya jirani,
ambavyo wanavielewa vizuri, kuwafukuza magaidi na wale wote walio nyuma
ya matukio ya upigaji risasi mjini," aliiambia Sabahi. "Hatuna tarehe
maalumu watakapoenea, lakini tunatarajia kuwa itakuwa hivi karibuni kwa
sababu ya vitisho vya muda mrefu."
Kuwahakikishia usalama polisi wa akiba, shughuli zao zitakuwa
zikijulikana na viongozi wachache wa usalama. "Tunataka waongeze nguvu
katika usalama wa mji bila kutambulika. Tunaamini watakuwa kiungo muhimu
kati ya jamii na mamlaka hiyo," alisema Mureithi.
Zaidi ya kueneza jeshi la polisi wa akiba, mamlaka zitataka teksi
zote zinazofanya kazi ndani na nje ya Garissa kuwa na namba za
utambulisho zilizochorwa katika magari yao zikiwa kubwa na rahisi
kusomeka, alisema Mureithi.
"Tumegundua kwamba teksi zimekuwa zikitumika kama njia ya kupitisha
wahalifu, na ni vigumu kwa mashuhuda kushika namba kwa gari
linalotembea," alisema.
Aidha, alisema magari yote yatazuiliwa kuwa na madirisha yenye vioo vya rangi ya giza.
Wananchi walisaidia jeshi kwa tahadhari
Sheikh Abdullahi Salat, mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Kenya
huko Garissa, alipongeza jitihada za usalama, lakini alitahadharisha
kwamba serikali inapaswa kuwa makini kutoruhusu wanachama wa kitengo
kipya kufanya mauaji mengine kwa jina la kukabiliana na ugaidi.
"Wananchi waliopata mafunzo wanapaswa kufikia viwango vya juu vya
maadili ili kufanya operesheni zao ndani ya sheria zao za nchi," Salat
aliiambia Sabahi. "Kama ikiwezekana, washukiwa wanapaswa kukabidhiwa kwa
serikali kwa ajili ya hukumu ya kisheria kutawala."
Serikali inapaswa kuwajibika kama kikosi kitawadhuru watu wasiokuwa
na hatia, alisema, akiongeza kwamba serikali inapaswa pia kufafanua
jinsi inavyopendekeza kuwatuliza maofisa wa KPR mara vitisho vya ugaidi
vitakapoondoshwa.
John Chege, anayemiliki
Hoteli ya Holiday Inn huko Garissa, eneo ambalo lilitokea ghasia za mauaji mwezi uliopita, alisema alipenda kikosi kisambazwe haraka iwezekanavyo kusaidia jumuiya ya wafanyabiashara.
Wafanyabiashara wengi wanakimbia Garissa kwa sababu mashambulio ya
mara kwa mara yameharibu biashara, aliiambia Sabahi. Kwa hiyo, serikali
inapaswa kujaribu kila linalowezekana kurejesha ujasiri wa
wafanyabiashara na kueneza kukua kwa uchumi, alisema.