Gari waliokuwa wamepanda likionekana katika hali mbaya
Mmoja wa waanzilishi na wamiliki wa Jamii Forums, Maxence Melo, amepata
ajali ya gari katika barabara kuu iendayo Mwanza; kilometa chache
kutoka Nzega mjini.
Mwanzilishi mwenzie na msemaji wa Jamiiforums, Mike Mushi, amesema
Maxence na ndugu yake ambaye naye alikuwepo kwenye ajali hiyo,
walikimbizwa katika hospitali ya Rufani ya Bugando kwa matibabu na
uchunguzi zaidi.
Bw. Mushi amesema hali ya Maxence kwa sasa si mbaya sana. Haijaelezwa
Bw. Maxence melo ameumia kiasi gani, ila taarifa zinasema kuwa ndugu
yake amejeruhiwa vibaya .
Maxence na mwenzake walikua njiani kuelekea mkoani Kagera na gari walilokua wakisafiria (pichani) limeharibika vibaya.