Thursday, August 1, 2013

Uruguay kuhalalisha utumizi wa Bangi


Bangi
Bunge la Uruguay limepitisha mswada wa kuhalalisha bangi. Ikiwa mswada huu utapitishwa na Baraza la Senate, Uruguay itakuwa nchi ya kwanza kuhalalisha uzalishaji na utumiaji wa bangi.
Hatua hii inaungwa mkono na serikali ikisema itapunguza mapato na faida kubwa kwa walanguzi wa mihadarati pamoja na kuwafanya watumizi wa bangi kutotumia dawa kali za kulevya.Chini ya mswada huo ni serikali pekee itakua na kibali cha kuuza bangi.
Pia serikali itatoa utaratibu wa uzalishaji, mavuno, uhifadhi na mauazo ya nje. Wanunuzi wote watanakiliwa kwenye daftari maalum na sharti wawe wametimiza miaka 18 na zaidi. Mteja anaweza tu kununua kilo 40 kwa mwezi kutoka kwa maduka ya dawa au kukuza mimea sita ya bangi.Wageni hawatakubaliwa kununua bidhaa hii.
Wabunge 50 kati ya 96 walipitisha mswada huo. Wanaotetea kuhalalishwa kwa bangi wamesema vita dhidi ya mihadarati havijapiga hatua na ipo haja kuweka mbinu mpya.
Kwa miongo mingi kanda ya Latin America imekumbwa na ghasia za magenge ya mihadarati ambapo maelfu ya watu wamekufa. Matukio ya Uruguay yanatazamwa kwa karibu eneo hilo ikiwa yatasaidia kupunguza machafuko yanayotishia uthabiti wa mataifa mengi.

Uchaguzi 'Kichekesho Kikubwa'


 
Morgan Tchangirai
Waziri Mkuu Zimbabwe Morgan Tchangirai adai uchaguzi ni kichekesho kikubwa
Uchaguzi wa Rais nchini Zimbabwe ulikuwa ‘kichekesho kikubwa,’ Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema, akituhumu udanganyifu wa kura uliofanywa na kambi ya mpinzani wake Rais Robert Mugabe.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Tsvangirai alisema uupigaji kura wa Jumatano ulikuwa ‘upuuzi na si halali’.
Kundi kubwa la waangalizi mapema lilisema kufikia hadi watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.
Chama cha Bw Mugabe ambacho kinadai kushinda, kimekanusha tuhuma hizo kikisema upigaji kura ulikuwa shwari.
Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, alisemsa kwenye tathimini yao ya awali kuwa upigaji kura ulikuwa huru na haki.
Makundi mengine ya waangalizi yalisifia hali ya amani katika uchaguzi huo.
Kuhesabu kura ulianza kulianza usiku na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) ina siku tano za kutangaza nani mshindi katika uchaguzi huo.
Tayari polisi wameonya kuwa watachukua hatua dhidi ya yeyote atakayejaribu kuvujisha habari za matokeo. Ni kinyume cha sheria kutangaza matokeo yasiyo rasmi.
Vikosi vya ziada baadhi vikiwa na vifaa vya kupambana na waandamanaji tayari viko mjini Harare.
Hatua za kisheria huenda zikafuata sasa, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Andrew Harding akiripoti kutoka Johannesburg.
Lakini megi yatategemea iwapo majirani wa Zimbabwe watapitisha uchaguzi huo, mwandishi wa BBC anaongezi.

'Uchaguzi umekumbwa na kasoro kubwa'

Akizungumza kwenye makao makuu ya chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) mjini Harare, Bw Tsvangirai alisema: "Hitimisho letu ni kuwa uchaguzi huu ni kichekesho kikubwa.’
"Uhalali wa uchgauzi huu umeharibiwa na ukiukwaji wa sheria na shughuli za kiutawala ambazo zimeathiri matokeo yake.”
"Ni utani ambao hauonyeshi matakwa ya watu."
Bw Tsvangirai alizungumza muda mfupi baada ya mtandao wa waangalizi (Zimbabwe Election Support Network-ZESN) kusema kuwa uchaguzi huo ‘umekumbwa na kasoro kubwa".
Katika taarifa yake rasmi ZESN limesema wapiga kura muhimu kufikia asilimia 82 walizuiwa katika vituo vya kupigia kura maeneo ya mijini ambako ni ngome ya Bw Tsvangirai.
Katika maeneo ya vijijini am, ambako ni ngome ya Rais Mugabe ni asilimia 38, kundi hilo limeongeza.
Jumatano wanavijiji, mawakala wa MDC kwenye vituo vya kupigia kura na ZESN walisema kumekuwa na kasoro kadhaa katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Masvingo.
Walisema viongozi wa jadi na wakuu wa vijiji waliwapanga watu kwenye mistari na kuwalazimisha kutembea kuelekea vituo vya kupigia kura na kuwapa namba za kupigia kura kama vile kuwahakiki wamempigia kura nani.
Wanatuhumu kuwa kwenye maeneo haya baadhi ya watu wasomi walilazimishwa kujifanya hawajui kusoma na kuandika na wakasaidiwa kupiga kura ambazo zilikuwa ni kwa Zanu-PF.
Msemaji wa Zanu-PF Mtaalam wa Saikolojia Maziwisa alikanusha kuwa wapiga kura wengi wamezuiwa makusudi kujiandikisha.
Amekiri kuwa kulikuwa na kasoro kadhaa lakini akafafanua kuwa vyama vyote vimeathirika.
"Ni muhimu kumbuka kuwa hiyo kwa sehemu ilisababishwa na ukweli kuwa baadhi ya vifaa muhimu Waziri wa Fedha Tendai Biti, anayetoka chama cha MDC alikuwa," Bw Maziwisa aliiambia BBC.
"Ukiaangalia hali ya Zimbabwe utakuwa na hitimisho m
oja tu. Na hii ni juu ya zaidi ya miaka mine iliyopita tumefanya jitihada za kutosha kufanya mazingira ya Zimbabwe yawe mazuri inavyowezekana ili uchaguzi uwe huru na hali.."