Idadi ya matukio katika siku za karibuni yameonyesha wazi kuongezeka
kwa mapambano baina ya makundi mbalimbali ndani ya al-Shabaab, na kiasi
cha kuwa siku za usoni kikundi washirika wa al-Qaeda kitakabiliwa na
mgogoro na kumomonyoka.
Siku ya Jumatatu jioni (tarehe 29 Aprili), mpiganaji jihadi mzaliwa
wa Marekani Omar Hammami, anayejulikana pia kama Abu Mansour al-Amriki,
alionekana kuandika bandiko lake la mwisho katika
mkasa
uliodumu mwaka mmoja sasa ambao umemsibu yeye na wapiganaji wenzake wa
kigeni dhidi ya kamanda wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, anayejulikana pia kama Mukhtar Abu Zubayr.
Katika mfululizo wa mabandiko ya kuchanganyikiwa siku ya Jumatatu
jioni, al-Amriki, akitumia akaunti ya Twitter handle @abumamerican,
aliuaga ulimwengu kama mpiganaji wa al-Shabaab mwaminifu kwa Gadane kwa
madai kuwa amekusudia kumuua yeye na wafuasi wake.
"Pengine nisipate fursa nyingine ya kuandika lakini kumbukeni
tulichokisema na kile tulichosimamia. Mungu aliniweka hai ili kutoa
ujumbe kwa umma," alisema.
Hata hvyo, siku ya Jumanne (tarehe 30 Aprili), al-Amriki alianza
kutuma idadi kubwa ya ujumbe mpya kuhusu maendeleo ya hali yake, na
kutaja kutolewa kiungo cha fatwa inayodaiwa kuandikwa na kuungwa mkono
na makamanda watatu wakubwa wa al-Shabaab wanaopingana na Godane --
Ibrahim al-Afghani
(ambaye jina lake halisi ni Ibrahim Haji Jama Meeaad na ambaye pia
anajulikana kama Abu Bakr al-Zaylai), Sheikh Mukhtar Robow Ali (au Abu
Mansur) na
al-Zubayr al-Mujahid -- pamoja na
kiongozi wa Hizbul Islam Sheikh Hassan Dahir Aweys.
Fatwa ilimweleza al-Amriki na wafuasi wake kama "ndugu" ambao damu
yao haikuruhusiwa kumwagika "hata kama [Godane] ataamrisha hivyo".
Iliendelea kuonya dhidi ya "utiifu wa upofu" kwa Godane, na kuelezea
majaribio dhidi ya maisha ya al-Amriki na wafuasi wake kama "uzembe
unaosababishwa na ujinga wa hali ya juu, au matokeo ya kufanya hila kwa
dhana za kisheria kwa ajili ya masilahi ya kisiasa na kupata malengo
binafsi ambayo hayahusiani chochote na sheria ya Mungu".
Jaribio la mwisho kwa maisha ya al-Amriki
Alhamisi iliyopita jioni (tarehe 25 Aprili), wakati akiwa amekaa kwenye duka la chai,
wanausalama kadhaa wa al-Shabaab walidaiwa kujaribu kumuua al-Amriki,
lakini wakashindwa. Masaa kadhaa kupita, al-Amriki alisema alipokea
neno kutoka kwa kikosi cha al-Shabaab kwamba walikuwa wameizunguka
nyumba yake.
"Abu Zubayr ameshakuwa mwendawazimu, anaanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe," al-Amriki alisema.
Baada ya kuwa kimya kwa siku kadhaa, al-Amriki alirejea kwenye
Twitter kusema kwamba alikuwa anaishi anaandaa kinachoweza kuwa pambano
lake la mwisho ndani ya al-Shabaab. Kutoka katika Tweets yake,
inaonyesha kwamba al-Amriki na wafuasi wake sasa wanakimbia baada ya
majadiliano yaliyoshinda na wapiganaji wa Godane.
"Tuliomba iwepo sharia na kukubali mambo mengi ya kuleta amani lakini
wanasema sisi ni kikundi cha wasaliti hata kama [Godane] ni kiongozi
wetu na hatutapigana," alielezea.
"Ni hatima ya […]
mapambano yaliyokamilika dhidi ya wale wanaosema ukweli," al-Amriki aliandika, "Hata kama tutakufa, tumeshinda".
Vikundi vya al-Shabaab vyawindana
"Jaribio la mauaji ya al-Amriki toka kwa Godane ni ishara ya wazi
kwamba mpasuko baina ya kiongozi wa al-Shabaab na wapiganaji wa kigeni
umekuwa vita vya moja kwa moja," alisema Omar Ali Roble, aliyekuwa
waziri wa upunguzaji silaha na kuwaunganisha na jamii wanamgambo wa
Somalia.
"Wanawindana wao kwa wao, jambo ambalo ni ushahidi wa wazi kuwa
al-Shabaab hakukuwa kikundi cha dini au jihadi, bali kikundi cha
wahalifu kilichojikusanya kuua umma wa Somalia chini ya kisingizio cha
dini," aliiambia Sabahi.
Kumaliza upinzani sio kitu kipya kwa Godane, kwa vile anajulikana
kufanya vitendo kama hivyo dhidi ya wanachama wa kikundi au washirika
wao wanaompinga, Roble alisema.
Kile kinachoonekana zaidi, Godane ameunganishwa na kifo cha Fazul
Abdullah Mohammed, kiongozi wa al-Qaeda katika Afrika ya Mashariki,
ambaye aliuliwa mwezi Juni 2011 wakati msafara wake uliokuwa unaongozwa
na wapiganaji wa al-Shabaab, inadaiwa kwa maagizo ya Godane, ulikwenda
moja kwa moja katika kituo cha upekuzi wa usalama cha Umoja wa Afrika
mjini Mogadishu.
Wapiganaji wa kigeni wa al-Qaeda wenye uhusiano na viongozi wa
al-Shabaab ambao wanasimama kumpinga Godane, kama vile Robow,
wanawakilisha hatari kwa kamanda wa juu wa kikundi, Roble alisema. "Ndo
sababu [Godane] anaanzisha mkakati wa 'kugawa na kutawala', kwa
kuwaondosha viongozi wa kigeni [wa al-Shabaab] wanaopingana na mawazo
yake."
Barua za wazi zatingisha misingi ya al-Shabaab
Wakati mgogoro baina ya wapiganaji wa kigeni na wanachama wa
al-Shabaab watiifu kwa Godane wanajitokeza, idadi ya barua za wazi
zinazopelekwa kwa utawala wa Godane zimeanza kumomonyoa kikundi kutoka
ndani.
Barua ya kukosoa iliyopelekwa kwa Godane kutoka kwa al-Zubayr al-Muhajir, anayedai kuwa mmoja wa wapiganaji wa juu wa al-Shabaab,
ilitumwa kwa idadi kubwa ya tovuti za wanajihadi tarehe 20 Aprili,
kuonyesha kuzidi kwa kutoaminiana na kukatika kwa mawasiliano baina ya
vikundi tofauti ndani ya washirika wafuasi wa al-Qaeda.
Barua ya al-Muhajir ilikuja si zaidi ya wiki mbili baada ya kamanda wa pili kwa cheo,
Ibrahim al-Afghani, kutoa barua ya wazi hapo tarehe 6 Aprili Ayman al-Zawahiri, ambamo alitosa ukosaji mkubwa wa wazi kwa Godane.
Barua ya al-Afghani ilifuatiwa na nyingine
iliandikwa na al-Amriki,
ambaye alikuwa wa kwanza kuonyesha tatizo ya uongozi wa ndani wa
al-Shabaab, kutowaamini wageni na kutokuaminiwa kwa wageni katika suala
la jihadi.
Hassan Abdullahi, mchambuzi wa masuala ya kisiasa ambaye anafuatilia
masuala ya harakati za Kiislamu nchini Somalia, alisema barua hizo ni
ishara ya mgawanyo mkubwa miongoni mwa uongozi wa kikundi hicho.
"Kwa hakika, kuna mtanziko mkubwa miongoni mwa uongozi wa kikundi
hiki, Wasomali na wageni pia, na imekuwa wazi kwamba tofauti haziko tu
baina ya Godane na Abu Mansur lakini pia zinajumuisha viongozi wengine
wa kundi hili," Abdullahi aliiambia Sabahi.
"Wapiganaji wa nje katika kikundi hiki kwa sasa wanajua kuwa
wanapuuzwa na kutengwa katika nafasi za ngazi ya juu na kwamba wako
chini katika nafasi za uongozi, kwa hiyo wanatafuta kuondoka kwa
usalama," alisema.
"Baada ya kuanguka kwa al-Shabaab kisiasa, kijeshi na kifedha,
viongozi wa kikundi hiki wameanza kutuhumiana kuhusu nani anayehusika na
kuanguka huko," Abdullahi alisema. "Isingekuwa kukuzwa katika kusema
kwamba kikundi hiki kwa sasa kimeingia katika hatua nyingine ya
kumomonyoka."
Kushindwa zaidi
Abdikadir Ahmed Gardiyow, ofisa usalama mstaafu wa Somalia, alitabiri hata kutoridhika zaidi ndani ya vyeo vya al-Shabaab.
"Mgogoro wa ndani katika al-Shabaab ni wa kina sana na sasa unafikia
mgawanyiko na tofauti ya mawazo. Umefikia hatua ya mapigano ya moja kwa
moja, mgogoro wa ndani kwa ndani na kufutwa," Gardiyow aliiambia Sabahi.
"Katika miaka kadhaa iliyopita, al-Shabaab ilijaribu kujionyesha
yenyewe kwa mataifa ya nje kama ni chama chenye nguvu ambacho wanachama
wake wanapigana kwa sababu moja. Hata hivyo, matukio ya hivi karibuni ya
ndani na mgogoro unaoendelea miongoni mwa viongozi wake yametoa picha
tofauti," alisema. "Ujumbe mbalimbali na malalamiko yanayotokea yatakuwa
kali zaidi na hili litaathiri sana jitihada za kikundi za kuajiri
wapiganaji wapya wa kigeni."
Hussein Mohamed, mchambuzi wa masuala ya kisiasa anayeishi Mogadishu,
alitabiri kwamba matukio haya yatasababisha kutofautiana ndani ya vyeo
vya al-Shabaab na kwamba kikundi kilichojitenga kingeweza kujitokeza
katika siku zijazo.
"Kama mgogoro huu wa ndani katika al-Shabaab utaendelea, kikundi
kilichojitenga kitajitokeza mara moja. kuna uwezekano kwamba kundi la
kwanza kama hilo lililojitenga litamuunga mkono Abu Mansoor al-Amriki,"
aliiambia Sabahi. "Katika tukio ambapo tawi linatawaliwa na wapiganaji
wa kigeni ndani ya al-Shabaab linaweza kuvunjika, hili litadhoofisha
zaidi harakati na linaweza kusababisha kusambaratika kwake kwa jumla."