62.-(1) Kila Mshirika wa Muungano atakuwa na mamlaka na
haki zote juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano, na katika utekelezaji wa
mamlaka hayo, kila Mshirika wa Muungano atazingatia misingi ya
ushirikiano na mshirika mwingine kwa kuzingatia haki na usawa kwa ajili
ya ustawi ulio bora kwa wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya
Muungano.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akipokea nakala
ya rasimu ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa
Makamu wa Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Jaji Mstaafu Joseph
Warioba akishuhudia.
62.-(2) Bila ya kuathiri mipaka iliyowekwa na Katiba hii,
kila Mshirika wa Muungano atakuwa na uwezo na uhuru wa kuanzisha
mahusiano au ushirikiano na jumuiya au taasisi yoyote ya kikanda au
kimataifa kwa mambo yaliyo chini ya mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya
Mshirika wa Muungano.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd akipokea nakala ya rasimu
ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Makamu wa
Rais Muungano Dkt Gharib Bilal, huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda
akishuhudia akishuhudia.
Pata nakala kamili ya Rasimu ya Katiba mpya hapa: Rasimu
No comments:
Post a Comment