Wednesday, May 29, 2013

North Korea allows business from the South to re-enter Kaesong industrial park

North Korea says South Korean businessmen can enter a jointly run industrial park in the North that has been emptied since April after tensions between the two countries soared.

North Korea has urged foreigners living in South Korea to consider evacuating, saying there was a risk of “thermo-nuclear war” breaking out on the Korean peninsula.
Cars packed full of electronic products cross the border after leaving North Korea's Kaesong joint industrial complex  Photo: AP Photo/Kyodo News
In a statement carried by the North's official media today, the government agency in charge of relations with Seoul said Pyongyang is ready to talk about reopening the Kaesong complex if the business owners visit.
South Korea's Unification Ministry urged North Korea to have talks with the government not civilians. It had no further comment.
Kaesong, run with cheap North Korean labor and South Korean funds and knowhow, was a last remaining symbol of inter-Korean cooperation until the North barred entry from the South in April and pulled some 50,000 workers.
Many managers and officials have asked to return to check up on their machinery, as well as stocks of raw materials and finished goods they were forced to leave behind.
Born out of the "Sunshine Policy" of inter-Korean conciliation initiated in the late 1990s by South Korean president Kim Dae-Jung, Kaesong has been a crucial hard currency source for the impoverished North, through taxes and revenues, and its cut of worker wages.

Jeshi la Kenya kuwanyang'anya silaha kwa nguvu wakaazi wa Mandera

Baada ya kuwaomba wakaazi wa Mandera kusalimisha silaha zao, Inspekta Jenreali wa Polisi, David Kimaiyo, alitangaza siku ya Jumatatu (tarehe 27 Mei) kwamba vikosi vya usalama vitaanza kampeni ya kuwanyang'anya silaha kwa nguvu, kiliripoti kituo cha Capital FM cha Kenya.
Wakaazi wa Mandera walitakiwa kusalimisha silaha zao kwa serikali mwezi huu au kunyang'anywa kwa nguvu. Hadi sasa polisi wamepokea silaha 12 tu, licha ya kuongezwa kwa muda wa mwisho.
"Tunachosisitiza ni kwamba wakaazi wote lazima wasalimishe silaha zao. Sote tumekubaliana na viongozi kutoka maeneo haya kwamba wakishindwa kufanya hivyo, tutawanyang'anya kwa lazima," alisema Kimaiyo baada ya mkutano na viongozi kutoka Wajir, Mandera na Garissa. "Ili maendeleo yapatikane kwenye maeneo haya, lazima usalama uwepo. Tunawatolea wito wakaazi kutupa taarifa ambazo zinaweza kusaidia kudhibiti uhalifu."

Ulamaa wa Kenya ataka adhabu ya kifo kwa wanachama wa al-Shabaab wanaopinga uongozi

Watu wanaochochea mgawanyiko ndani ya al-Shabaab na wanaompinga kiongozi wa kundi hilo, Ahmed Godane, lazima wauawe, alisema ulamaa na muungaji mkono mkubwa wa al-Shabaab, Sheikh Hassan Hussein Aadan, iliripoti Redio RBC ya Somalia siku ya Jumanne (tarehe 28 Mei).
"Nimesikia kuwa kuna migawanyiko ndani ya wapiganaji wa jihadi. Anayetengeneza migawanyiko hiyo lazima auawe," alisema Aadan, ulamaa wa Kenya mwenye asili ya Somalia anayeishi Nairobi. "Naamini mtu anayejaribu kuzuia jihad lazima auawe."
Aadan amewahimiza watu kwenda mstari wa mbele na kujiunga na kile alichokiita "jihad" nchini Somalia.
Kauli ya Aadan imekuja baada ya kiongozi wa juu wa al-Shabaab, Hassan Dahir Aweys, kumkosoa vikali Godane katika mahojiano yaliyorushwa tarehe 16 Mei na televisheni ya Somali Channel, akimtuhumu kwa udikteta, kulitekaji nyara kundi hilo ili kutanua himaya yake na kupuuzia maoni ya viongozi wengine wa al-Shabaab.

Mkutano wa waekezaji Somalia wafanyika Kenya

 29Mei, 2013

Bandari ya Kismayo ikemuwa ikitumika tangu Al Shabaab kufurushwa
Mkutano wa kikanda kuhusu uekezaji na ukarabati nchini Somalia umeanza hii leo, mjini Nairobi, Kenya.
Waandalizi wa mkutano huo, wanasema kuwa lengo la mkutano ni kuangazia nafasi za uekezaji nchini Somalia kwani nchi hiyo sasa imeanza kuonekana kuwa thabiti
Mkutano wenyewe unahudhuriwa na wanasiasa wa kikanda na wa kimataifa , wafanyabiashara na wataalamau wa maswala ya kiuchumi.
Mapema mwezi huu , wafadhili katika mkutano wa kimataifa wa wafadhili mjini London, waliahidi kuchangisha dola milioni miamoja na thelathini.
Waekaji wamezungumzia maswala ya usalama na changamoto nyinginezo ambazo zinaweza kuwakabili waekezaji walio na moyo wa kufanya biashara nchini Somalia.
Licha ya mazingira kuwa bora kuliko siku za nyuma, watu nchini Somalia wangali wanakumbwa na visa vya utobu wa usalama hasa katika mji mkuu Mogadishu.
Wanamgambo wa Al Shabaab walifurushwa kutoka mji huo kufuatia juhudi za majeshi ya Muungano wa Afrika kwa kusaidiana na jeshi la Kenya na Somalia kupambana dhidi ya wanagmbao hao.
Kwa sasa wangali wanadhibiti maeneo yaliyoko nje ya mji mkuu ambako hufanya mashambulizi ya kuvizia.
Licha ya changamoto hizi, kunao waekezaji wa Somalia ambao wamerejea nchini humo kutoka mfano Uingereza na Marekani kuja kufanya biashara. Maisha mjini Mogadishu pia yameweza kubadilika kwani mji huo una taa nyakati za usiku na maisha huendalea kama kawaida huku mikahwa na vilabu ikiwa wazi kwa wanaopenda maisha ya kujitumbuiza nyakati hizo.