Msaidizi wa rais wa Misri
ameomba radhi kwa kukosa kuonya wanasiasa kuwa mapendekezo yao kuhusu
jinsi ya kuizuia Ethiopia kujenga bwawa katika mto Nile,ikiwemo kuchukua
hatua za kijeshi yalikuwa, yalikuwa yakipeperushwa moja kwa moja
kupitia televisheni.
Msaidizi huyo Bakinam al-Sharqawi, aliomba radhi
kwa aibu yoyote waliyopata viongozi hao ambayo huenda ilitokana na
kitendo hicho.Rais Mnorsi aliitisha mkutano huo kutathmini athari za ujenzi wa bwawa la Ethiopia katika sehemu ya maji ya mto Nile yanayomilikiwa na Misri.
Washiriki wa mkutano huo hawakujua kuwa walikuwa wanatizamwa kwenye runinga wakati wakitoa matamshi yao bila ya kujali.
Mapendekezo yao yalikuwa pamoja na kuonya Ethiopia kuwa inatutumia nguvu za kijeshi dhidi yake ikiwa itaendelea na mpango wake wa ujenzi wa Bwawa kwenye mto Blue Nile.
Moja wa wanasiasa, alipendekeza kutuma kikosi maalum kuharibu bwawa hilo, mwingine akisema kuwa watatuma ndege za kivita kutisha Ethiopia wakati wa tatu akisema kuwa wangeunga mkono waasi wanaopambana na serikali ya Ethiopia.
Misri ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu Mashariki ya Kati na hutegemea sana maji ya mto Nile ambao ndio mto mrefu zaidi duniani.