28 Mei, 2013
Waziri wa mambo ya nchi za nje
wa Uingereza William Hague amesema kuwa vikwazo vya silaha ambavyo
Muungano wa ulaya uliiwekea Syria vimeondolewa .
Akizungumza baada ya mkutano wa siku moja na
mawaziri wengine wa mambo ya nje wa muungano wa Ulaya mjini Brassels,
Bwana Hague alisema kuwa hakuna uamuzi wa moja kwa moja wa kutuma silaha
kwa waasi wa Syria , na kwamba vikwazo vingine vitaendeleaInatarajiwa kuwa wakati huo Uingereza, Ufaransa na mataifa mengine yanayotaka kuchangia silaha kwa waasi wataruhusiwa kufanya hivyo.
Uamuzi huo utategemea mkutano mkubwa wa kibalozi utakaofanywa kati ya Marekani na Urusi mwezi ujao. Hata hivyo mkutano huo hauna uhakika wa kufanyika kwa sababu muungano wa makundi ya upinzani nchini Syria haujakubaliana kama wahudhurie au wasihudhuria mkutano huo licha ya utawala ya Rais Assad kusema kuwa unakubaliana na mkutano huo.
Mwandalizi mkuu wa mkutano huo, ambaye ni Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza William Hague amesema kuwa tamko la Serikali ya Rais Assad kuwa huenda ukahudhuria mkutano huo ni la kutia moyo.
Ishara zote kutoka mashinani hadi sasa ni kuwa itachukua muda mrefu kabla ya wananchi wa kawaida kukubaliana na mapendekezo yanayotolewa na Jumuiya ya Ulaya.